Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, sauti ya wale waliokosa Jukwaa la kuongelea matatizo yao

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,572
9,808
Sote tu mashahidi ya kwamba cheche za hoja zenye mashiko ya nguvu na zikishadadishwa na mantiki za kimdahalo, na hata kuibua mijadala yenye tija ktk kuhamasisha na kuwalazimisha makada wa CCM walazimike kumjibu TAL. Hii ni kuashiria cha wazi ni YEYE ndiye mwenye kuwakilisha wapinzani makini wa serikali iliyopo madarakani.

Mwaka 2015 ingawaje ENL aliwakilisha "icon" ya UKAWA lakini alikuwa ni kiongozi dhaifu kuweza kusimamia dhuluma ya kidemokrasia iliyofanyika dhidi ya maamuzi halali ya umma ya kuikataa CCM. Mwaka huu kimeeleweka, nasema tena kimeeleweka. Huku Tanganyika tunaye TAL na kule Zanzibar ndio tu Maalim Seif.

Upuuzi wowote ule wa kutaka kuchakata matokeo ya uchaguzi yatapatiwa tiba mbadala. Umefika wakati muhimu sasa, kumbukumbu zote za CCM zikatafutwe kule jumba la makumbusho ya taifa.
 
Na wabunge wa Chadema wangefanya kama rais Kondebkumpiga waziri wake aliyetafuna hela Mbowe asingekula tena billion 8 ya michango ya wabunge.
Mkuu Elitwege, matongotongo yamewatoka Watanzania waliokuwa wengi kutokana na kutokuwepo kwa ushirikina utakanao na mbio za mwenge kwa mwaka huu. Watu wamefumbuliwa akili zao kwa mpango wa Mungu.

Twege, it is honour to be part of patriotic movement for the sake of our nation, equally it is not honour to cling with violent criminals like as CCM's admirers..
 
Lissu leo ameongeza kashfa mpya ya shamba la maelfu ya ekari huko Karagwe kama ilivyo kashfa ya Mayanga hio nayo haina majibu
Hoja ya serikali za majimbo inazidi kubamba sana. Fuko la hazina ya taifa ni lazima liwe na sauti na mikononi mwa Watanzania wote, na siyo kwa mtu mmoja mbinafsi na aliyekuwa na upendeleo wa wazi wa kikanda na kikabila tofauti na wenzake wote walimtangulia, tena asiyeaminika na pia mwenye mashaka mengi kwa kigezo cha maadili ya uongozi.
 
He came to this Land to guide and teach his fellow men.

Lissu amefanya na waandhishi wa habari wamepumua. Maana angalau wanamuogopa ogopa. Huyu Lissu ndio mtu pekee anaweza kumlaza jpm na viatu. Mifano ni mingi hadi anaogopa na kutaka kumpa ka kaI kadogo. Leo anasema Lissu anachakata video za 2015. Kashikwa vibaya.
 
Hoja ya serikali za majimbo inazidi kubamba sana. Fuko la hazina ya taifa ni lazima liwe na sauti na mikononi mwa Watanzania wote, na siyo kwa mtu mmoja mbinafsi na aliyekuwa na upendeleo wa wazi wa kikanda na kikabila tofauti na wenzake wote walimtangulia, tena asiyeaminika na pia mwenye mashaka mengi kwa kigezo cha maadili ya uongozi.
Kale ka Hazina ka Dotto James na mjomba wake. Katakuwa hakana nguvu tena. Yaani nchi hii kodi zinapigwa na wajanja tu. Sera ya majimbo ndio mwarobaini na mafisadi watapinga tu.
 
Back
Top Bottom