Tundu Lissu: Richmond ni ya Rais Kikwete

inaonyesha tundu lisu hana maadili na si mkweli. ni mpotoshaji mkubwa, ndo maana dr. slaa alionyesha wasiwasi katika ugwiji wa sheria wa tundu lisu coz reasoning capacity yake iko low mnoooo hasa kwenye taaluma yake.
What is your reasoning capacity?? hata kuandika hujui.
 
Huyu fisadi hachomoki mwaka huu ngoja mahakama ya mafisadi ianze.

Nani wa kuianzisha hiyo mahakama? Thubutuu...sio Magufuli wala Lowassa au Mbowe. Hakuna katika nchi hii kiongozi yoyote mwenye uthubutu huo. Kwanza atafunga wangapi? Yeye mwenyewe ataponea wapi? Kwa usafi gani alionao Magufuli? Kwa baraka gani za watangulizi wake? Akianzisha tu ajue Mkapa na J.K watakua viranja wa hilo gereza la mafisadi.

Nchi hii inanuka rushwa kuanzia ofisi kuu Ikulu hadi ofisi za vijiji. Wote wala rushwa. Wamehalalisha kabisa rushwa. Hawana aibu. Leo wanakuja kutuambia wataanzisha mahakama za mafisadi. Zilizopo zina kasoro gani hadi zishindwe kuwashitaki mafisadi? Kesi gani ilishindikana huko hadi tuanzishe mahakama mpya? Taasisi za maadili kama Takukuru zimefanya nini cha maana hadi sasa? Takukuru imemkamata nani mwenye nguvu hadi leo hii?

Wanasiasa wa Tanzania wanajua wananchi 80% ni majuha. Hawana elimu. Hawajui wajibu wala haki zao. Hawana uwezo wa kukumbuka ahadi hata moja mwezi mmoja tu baada ya uchaguzi. Hawana ubavu wa kukemea maovu hata yakitendeka machoni mwao. Wanatucheka na kutung'ong'a. Wanatutumia watakavyo.

Ushauri wangu wewe ambaye kidooogo umefungukiwa. Nchi hii inahitaji mfumo utakaoruhusu mihimili ya dola ifanye kazi bila kuingiliana. Mfumo utakaompunguzia raisi madaraka. Mfumo utakaolazimisha uwajibikaji. Mfumo utakaoruhusu kujikagua na kujiwajibisha. Mfumo utakaowaweka matajiri na masikini katka mizania sawa. Mfumo utakaotetea Watanzania waliojaaliwa kila kitu lakini ni masikini wa kutupwa. Tuna jukumu la kuwezesha mfumo huo uanze hapa Tanzania. Utachukua muda lakini lazima tuanze siku moja; mapema iwezekanavyo. Kwa kuanza tuanze kwa kuimarisha bunge. Bunge litakaloisimamia serikali kwelikweli. Hii ni rahisi sana kwani tuna nafasi ya moja kwa moja. Bunge imara litawezekana kama lina wabunge wa upinzani ni wa kutosha. Wabunge wa upinzani watatosha tu kama utawapigia kura. Wapiga kura ni mimi na wewe. Amka kijana. Badilika
 
Yeah, that's Tanzania for you. Suala la Richmond limeshageuzwa komedi! JK angekuwa anatafuta ushauri maridhawa kabla ya kuanzisha malumbano na "vichaa" kama Lissu. Huyo lofa hana cha kupoteza. Kwake yeye kushoboka ndio asili yake. Sasa keshazibuka; JK atajibu nini? Akimtaja huyo mhusika wa Richmond basi papo kwa papo, bila kulisubiri swali dhahiri la nyongeza, atajikuta akitakiwa kuchukua hatua kama mkuu wa serikali! Mwenyewe anamjua Lissu kama fyatu tangu zamani (rejea mlinganisho aliomtolea na Slaa enzi zile - 2010). Sijui ndio kusahau.
 
Msajili wa Makampuni nchini(BRELA) na Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC) hawana taarifa sahihi za nani hasa ni mmiliki wa Richmond?

Kama taarifa za nina hasa ni mmiliki wa Richomond zina utata, ni kwanini Taasisi zinazohusika kutoa taarifa haziwajibiki au kwajibishwa?

Hivi waandishi wa habari kazi yenu ni kuripoti tu malumbano ya JK na Lissu juu ya mmiliki wa kampuni hii?

Ndugu waandishi,kwanini msifanye utafiti upya juu ya jambo hili?

Hivi na hapa tunawahitaji wataalamu kutoka nje kutusaidia kupata ukweli katika hili?!
 
Swali langu ni hili,Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa kashfa ya Richmond ndg Harrison Mwakyembe aliposema ikiwa watatoa taarifa yote ya kamati juu ya Richmond serikali ingeanguka alikuwa ana maana gani?kumbuka kwamba Waziri Mkuu Mh Lowassa alikwishajiuzulu,sasa ni serikali iliyo chini ya nani ingeakuka?ni kigogo yupi mkubwa zaidi ktk serikali aliyeachwa kutajwa na tume?Na kwanini Mwakyembe aseme Lowassa anawajibika si kwasababu yeye alikosa ila anawajibika kwavile uzembe ulifanywa na walio chini yake?Nenda kawadanganye wale mashabiki wenu vichwa vitupu mnaowaongopeaga kule vijijini,hapa JF kila mtu ni mjuaji.
Kwa madai ya uwongo kusema richmond ya kikwete si kweli richmond ni ya marekani alioileta richmond waziri mkuu ni mtendaji mkuu wa serikali kwa kujifanya kujua kutokuelewa utaratibu wa kazi shida watu kama tundu lisu richmond akamuuzia dowans sasa atutajie ni ya nani.

Kama rais angekua anajua yake asingemtaka Tundu Lissu amtaje mwenye Richmond.
 
Kwa madai ya uwongo kusema richmond ya kikwete si kweli richmond ni ya marekani alioileta richmond waziri mkuu ni mtendaji mkuu wa serikali kwa kujifanya kujua kutokuelewa utaratibu wa kazi shida watu kama tundu lisu richmond akamuuzia dowans sasa atutajie ni ya nani.

Kama rais angekua anajua yake asingemtaka Tundu Lissu amtaje mwenye Richmond.
Du Tz full vituko,Yaani hii ndiyo akili za watanzania harafu tunatejemea nchi iendelee,Yaani maswali ya kuuliza serikali una muuliza Lissu
 
Tangu liishe sakata la zitto na chadema lissu kapoteza umakini kutokana na hilo wanaikungi hatumchagui safari hii
vipi kuhusu matokeo ya serikali za mitaa ? kuna neno la uswahilini linasema hivi , UKIWA MUONGO JITAHIDI KUWA NA KUMBUKUMBU .
 
Wanabodi,
Ni siku kama nne zilizopita, Mh. Tundu Lissu aliuliza na kumtaka rais Kikwete aseme hadharani, Je Richmond ni ya nani?
Hazikupita siku nae rais Kikwete akatoa jibu japo la kimafumbo, ambayo sie hatuyataki tena bali tulitegemea kama angeamua kumtaja "Mwenye Richmond" angemtaja kwa jina lake badala ya kuendelea kuweka mafumbo kwamba "Mwenye Richmond" ni yule anayeongozana na Lissu! Haya nasikitika kuyaita ni majibu ya kiubabaishaji ambayo hutumiwa zaidi na watu wanaobahatisha kitu wasichokuwa na uhakika nacho, kama Waganga wa kienyeji wafanyavyo.
Swali hapa linalonitatiza mie Buldoza, ni kama mmoja wa Wanaoongozana na Tundu Lissu ndiye mwenye Richmond na rais analijua hilo, ni kwanini alikataa kuuvunja mkataba wa Richmond huku akijua wazi kwamba ni mkataba wenye maslahi ya mtu fulani (Yaani kulikuwa na mtu ana personal interest)? Mbona hiyo ilikuwa ni sababu tosha ya kuuvunja huo mkataba?
Pili mbona mkataba na Richmond, serikali iliendelea nao hata baada ya Waziri mkuu na mawaziri wa Nishati na Madini kujiuzulu?
Je ni nani aliyekuwa anamzuia rais asiuvunje huo mkataba?
Je Richmond ni ya nami ambaye ana nguvu kuliko za Rais?
 
Yule aliyesema haijui Richmond na baadaye kuitakatisha kwenda Symbion kwa hisani ya ufunguzi wa Obama naona ndiye muongo! Hujui mali ya nani halafu unaitakatisha!!

Wewe unayoyajuwa leo ndiyo hayo hayo uliyokuwa unayajuwa miaka minane iliyopita? huna ulichokiongeza katika kujuwa kwako hata kidogo?

Amma kwa hakika Tanzania hii wapumbavu ni wengi.
 
Kama ambavyo Dr. Slaa alivyowatoa pangoni kama Nyoka na kuja porojo za hapa na pale huku wakijisahau kuwa hawakujua ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA ulianzia wapi, ndivyo walivyokuja na porojo tena baada ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, JAKAYA MRISHO KIKWETE alipomwambia LISSU ANATEMEBEA NA MWENYE RICHMOND KWENYE KAMPENI MIKOANI.

Mbatia anakuna porojo za kukemea maneno yasiyostahili kwenye kampeni yanayotumiwa na CCM na kujivika UPOFU na UKIZIWI na kujifanya hajui maneno ya UDINI na UKABILA na kejeli kedekede kutoka kwa Wagombea wao. Hizi ni porojo tu, tena porojo za kuwa msemaji wa CHAMA CHA CHADEMA, UKAWA haupo tena. Hatuwasikii viongozi wa CUF na NLD, watanzania wanajua sasa MBATIA anaongea kama mwana wa KANDA na siyo mwana UKAWA.
ETI anaomba mdahalo wa WENYEVITI WA VYAMA, kwani JK , MBATIA na JK ndo wanagombea urais? Kwanini wasimlete FISADI wao kwenye mdahalo na TINGATINGA?

LLISSU naye eti RICHMOND ni ya JK , Lowassa alijiuzulu kumuokoa. Wakati wanasema ni FISADI? Na kwa nini asijibu LOWASSA mwenyewe? Porojo tu hizi, wanatapatapa.
 
Lakini naona JK anajichafua mwwnyewe kwa kujibizana na Lissu na kutupa majibu mepesimepesi bila haya. Kama kweli Richmond ilikuwa ya Lowassa kwa nn Lowassa alipoona mkataba ni mbovu na uvunjwe mamlaka ya juu ilikataa kufanya hivyo?

Kama leo JK anajitokeza na kusema yeye atamtaja, je alikuwa wapi siku zote kama sio kulindana?

Je kama anampa Lissu kazi ya kumtaja hivi haoni hatutendei haki watanzania kutunyima haki na uhuru wa kumjua mwizi?

Kwa nn ripoti ya mwakyembe ilisema ile ilikuwa ni sehemu tu na km angesoma yote basi serikali ingeanguka?

Je hiyo serikali ni ipi ukimuacha Lowassa?

Je mwakyembe alitutendea haki watanzania?

Leo wanapokuja na ngonjera zao za kuongea kwa mafumbo jukwaani ndio tuwaeleweje?

MIMI NATAKA MABADILIKO.
 
Generator za richmond zenye utata ziliuziwa Dowans chini ya Pinda, wakati Lowassa keshajiuzulu, share-holder mkuu wa wa Dowans akiwa Brigadier Gen mstaafu Sulaiman Mohammed Yahya al Adawi wa Oman.
Baadae hizo hizo generator zika milikiwa na kampuni ya Symbion Power Africa ya marekani, inaosimamiwa na watu wenye rekodi mbaya ya kufyonza mali asili za waafrika.

Wakati mitambo ya Richmond ikiuzwa kwa Dowans and Symbion Lowassa hakuwepo madarakani, sasa kwa nini mitambo iliyokuwa feki kutoka kampuni feki iendelee kutumika kuzalisha umeme tanzania??, ni dhahiri kwamba mhusika mkuu wa richmond sio Lowasa aliyeondoka madarakani ila ni mmoja wa hao waliobaki ndani ya ccm wakiwa bado na nguvu na mamlaka ya kuendeleza dili la richmond jinsi walivyotaka wao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom