Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Tundu Lissu akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na Wananchi wasio na itikadi ya chama chochote mkoani Dodoma ametoa hoja kali ambazo CCM hawana uwezo wa kuzijibu zaidi ya kupanic na kukimbilia kwenye vyombo vya habari viwahurumie wasirushe mikutano ya Tundu Lissu.

Mosi, amezungumza kuwa jipya na la ajabu kwenye utawala huu ni Rais kujenga uwanja mkubwa Chato wakati marais waliopita hawakufanya maajabu haya, amesisitiza Tundu Lissu.

Pili, ni kitendo cha Rais kupeleka mbuga Chato. Hili ni ajabu kuu ambalo halijawahi kufanyika amesisitiza Tundu Lissu.

Tatu, Lissu amesisitiza kuwa watu wamedhalilishwa, hasa viongozi wa serikali na akina Mama kwa kauli chafu zinazotolewa.

Lissu amesisitiza hii nchi sio kila mtu ni mjinga na unaweza kuwadanganya kirahisi. Kuna watu werevu na wanakwenda kuwaambia wananchi kwa miaka mitano madudu yaliyofanyika.

Je, haya maajabu ni kweli yamefanyika huko Chato?

Je, wakazi wa Lindi, Dodoma, Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro mnafahamu maajabu haya ya huko Chato?

Kwa hoja hizi ambazo hata mimi sikuzijua kwa miaka mitano, sasa nimeamshwa usingizini.

Hoja haipigwi rungu, bali hujibiwa kwa hoja. Hii ni kauli ya Dkt Jakaya Kikwete

CCM oyeee oyeeee oyeeee, jibuni hoja hizo!
Kuna uwongo mwingi sana kwenye hotuba za huyu jamaa... Mfano ni swala la magufuli kuua utalii ambalo ameliongelea wakat anahojiwa na radio ya kenya.... Tuwe wa kweli serikali ilipandisha kodi za utalii mkasema inaua utalii na hakuna wageni watakao kuja ila watalii wameendela kuongezeka kila uchwao. Kipind hichi kutali umedondoka sababu ya corona na we were expecting kupokea 1.8M tourist..
Na kama sio best stratergy za kupambana na corona bado tungekuwa tunashangaa tuu kwenye utalii ila leo watu wa arusha furaha inaanza kurejea kwan watalii wanaanza kuingia tumeona ndege kubwa zikiingia nchini recently kuleta watalii.....
Swala la corona ndugu lisu anajikaanga nalo mwenyewe. Imagine tungekuwa tumefungiwa ndani hali yetu ingekuwaje mpaka leo kikubwa ni kumshukuru Mungu madhara ya corona kwetu sio makubwa kiasi hicho, ugonjwa kama huu haufichiki.
Magu anamapungufu yake mengi tuu lakin amefanya mambo mengi na mazuri japo mabaya yapo tuyaseme ila sio kwa maudhui ya kupotosha
Mtu kama lisu ukiulizwa kwa miaka uliyokuwa mbunge umelifanyia nn jimbo lako... Kuna hata kisima kimoja cha maji umechimba... Lema umeifanyia nn arusha mjini cha kukukumbuka... Bungeni umeisemea nn arusha.. vijana wa arusha ambao ndio wengi wanakuchagua umewafanyia nn...
 
Ndugu Mbegu ya shambani, Tundu Lissu ni kweli watu wote sio wajinga, kwa hivyo naye TL ajue ni hivyo sie sio wajinga. Tokea amekuja na kuchaguliwa kupeperusha Bendera ys Chadema, hakuna Jipya alilokuja nalo, ila ni lile lile la kumshutumu na kumuandama Magufuli.

TL kama anajiona ni mbadala wa Rais Magufuli, atupe kisomo cha atakacho tufanyia tofauti na Magufuli, Maendeleo gani katuletea, Amezunguka Ulaya na USA, lipi lenye manufaa kwa wananchi alilolipata, zaidi ya kufuatilia ya Magufuli.

Pia ajue kuwa yeye ndiye aliyeamshwa kutoka usingingizini, sie tuko macho, tumeyaona mazuri na mabaya aliyoyafanya Magufuli, yeye alikuwa ughaibuni, sisi tumeyaishi.

Hapa hakuna hoja, bali kuna malalamiko na kilio. WATANZANIA WENGI WANOGOPA MWENDO WA LISSU ULIVYO, ANAONYESHA KUJIWEKEZA ZAIDI KWENY KULIPIZA KISASI, ZAIDI YA KUWALETEA WALALA HOI MAENDELEO.
Ngojea kampeni zianze utayapata tu
 
Kosa lingine kwa Tundu lissu,

Lissu hatakiwi kumshambulia Magufuli.

Lissu anatakiwa atuambie atafanya Nini,kukomaa na Magufuli ni sawa na kuzidi kujipunguzia kura tu.

Hivi kujenga hospital kubwa 69 sio maajabu.

Kukarabati shule za sekondari ambazo haziguswa toka mkoloni si maajabu.

Chadema mjipange sana na lissu wenu mtajikuta mmeishiwa maneno baada ya wiki moja tu toka kuanza kampeni.
Lissu anatumia mbinu ya adui yako mtaje kwa jina ili likitokea la kutokea watu wajue, mchawi mpe mwanao alee!
 
Naomba risit zake ili nikujibu vizur kama hauna risit ka kimya usilete porojo za vijiwe vya kahawa
Lete kwanza risiti za kununulia zile ndege halafu tueleze ni kwa nini mahesabu ya Atcl hayakaguliwi na CAG.
 
Wewe una mapungufu kichwani. Uliyoyataja, yote hayo yalikwishafanywa na watangulizi wake. Maajabu pekee nadhani ni hayo ua upendeleo na ubinafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Lissu akiongea majinga yanakariri bila kufikiria... Sawa waliopita walishafanya kilakitu huyu tulionaye hajafanya jambo!! Lissu tuu ndiye mwenye akili yakufanya vitu!!
 
haoni reli? Haoni madini? haioni Dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bure, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Majizi anayafukuza halafu anayarudisha inamaana na yeye ni mwizi
 
Mmeanza kumezeshwa maujinga kichwani na tundu? Chato hainahaki kujengwa uwanja wa ndege? Mbona KIA Ipo vijijini? Endeleeni kumskiliza huyo mropokaji asiyeweza kuona mazuri ya wengine.
Wakati wa utawala wa Daniel Moi kuna mgombea wa Eldoret alisema lami ni mambo ya kawaida tu hata mkoloni alijenga, baada ya uchaguzi Moi alipeleka greda likakwangua lami yote na walikaa na barabara ya vumbi hadi uchaguzi uliofuata. Nasisi naona kuna wajinga wanasema barabara daraja ni mambo ya kawaida na watu wanawashangilia,

Uhuru wakumchagua unaye mtaka unao ila uhuru wamaendeleo unayoyataka huo haupo ni walioko Bungeni na baraza la mawaziri ndio watakao amua upate maji barabara umeme zahanati ambulence madawati shule. Ngojeni msipompa kura JPM tunakwangua lami yote na tusisikie mtu akilalamika barabara na hivi ni lala salama hamna mtakachotufanya.
 
Back
Top Bottom