Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli alitoa rushwa Kibiti Mil. 5 na akanunua jogoo laki moja wakati kashapitishwa kugombea Urais. Nitamuwekea pingamizi

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,830
Amesema Rais Magufuli huku akiwa ameshatangazwa kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM kwenye Uchaguzi wa Oktoba 2020 ametoa rushwa Wilayani Kibiti kwa mujibu wa Fomu ya Kuweka Mapingamizi dhidi ya Mgombea Urais Amesema Rais Magufuli alipokuwa akigawa fedha kwa ajili ya madawati na shule alikiuka sababu ya 16 kwenye Fomu hiyo inayosema Mgombea Urais anaweza kuwekewa pingamizi iwapo atakiuka Makatazo yaliyotatwa kwenye sheria ya gharama za Uchaguzi



Mhe. Tundu Lissu mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA ameendelea kusisitiza kuwa hawezi kufungwa kwa kesi alizo nazo Mahakamani na kwamba haziwezi kumzuia kugombea Urais.

“Hafungwi mtu hapa” “Nina kesi sita Kisutu na zote ni za uchochezi.” Baraza Kuu la chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, limemchagua Tundu Lissu kuwa mgombea wake wa Urais katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Mhe. Lissu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa si yeye tu anayeweza kuwekewa pingamizi la kugombea Urais bali hata Mhe. Rais Magufuli pia anaweza kuwekewa pingamizi.

"Nani aliyesema kwamba CCM hawawezi kuwekewa mapingamizi? Nani aliyesema mgombea urais wa CCM, John Magufuli hawezi kuwekewa mapingamizi? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa CHADEMA"

Kwenye fomu ya mapingamizi, kwenye sababu 16, la 16 Magufuli amekiuka Mambo yaliyokatazwa moja wapo ni rushwa maana ukishaingia kwenye uchaguzi huruhusiwi kutoa rushwa, Magufuli akiwa anatoka kumzika Mkapa Lupaso, alifanya nini Kibiti? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa
CHADEMA

Lissu amesema kitendo cha Rais kutoa fedha Kibiti, kununua jogoo kwa Laki Moja ni rushwa wakati wa uchaguzi.

Mhe. Lissu katika moja ya sera zake amesema iwapo atashinda basi atakuwa na jukumu kubwa la kurudisha uhusiano wa nchi kimataifa.

"Tukishinda urais wa Tanzania, mimi nitakuwa Rais wa Katiba mpya. Kama tunataka mfumo mzuri wa utawala, mahali pa kuanzia ni Katiba mpya. Hii ndilo tutaanza nalo. Haina maana hatutajenga shule, kuboresha Sekta ya Afya '

MY TAKE: Bado tutandelea kushuhudia matamko mengi kwenye Uchaguzi huu ni juu yetu watanzania kumpima kila mgombea ili tupate kiongozi bora kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
 
NEC. hawatampatia fomu maana ana kesi za kujibu lakini pia ana zuio la maadili ya utumishi wa umma. Lkn ningeshauri wampe.
Si huwa kuna viambatanisho na uthibitisho wa kutokuwa na kesi za /kushitakiwa na Jamhuri?

Vyama vya siasa vingeliorganize ili vimteue mgombea asiye na shaka wala mawaa. Hii ingeliwasaidia sana, tatizo lao kubwa ni ubinafsi wa madaraka.

Siku zijazo wananchi watachoka kiasi ya kuacha kupiga kura kwa kuwa hakuna ushindi bila umoja.

Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, cha kushangaza uwa wanakumbuka tayari kwisha kucha.
 
Kwenye sifa za mgombea zimeainisha aina ya makosa yayomfanya apoteze sifa ya kugombea siyo makosa yote istoshe yeye ni mtuhumiwa tu katika hizo kesi zote sasa hawezi kunyimwa haki ya kugombea sababu ni mtuhumiwa tu.
 
Si uwa kuna viambatanisho na uthibitisho wa kutokuwa na kesi za /kushitakiwa na Jamhuri? Vyama vya siasa vingeliorganize ili vimteue mgombea asiye na shaka wala mawaa...
Unayoyasema umesimliwa au umeota? Hayo unayoyasema hayapo. Mgombea yeyote aliyepitishwa na chama ni lazima NEC impe form. Haina uwezo wala mamlaka ya kuzuia.

Uwezo wa Tume upo kwenye kumpitisha mgombea. Na haiwezi kuacha kumpitisha kama hakuna pingamizi kutoka kwa wagombea wenzake.

Kwwnye form unajaza tu kiapo chako kuwa hujawahi kufungwa kwa kosa la jinai au kukwepa kodi.
 
Ni kweli tutaendelea kusikia mengi Ila:

IMG_20200804_210728_515.jpg


kwa dhati kabisa, huyo ndiye aliye kiongozi bora kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom