Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,592
- 11,831
Amesema Rais Magufuli huku akiwa ameshatangazwa kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM kwenye Uchaguzi wa Oktoba 2020 ametoa rushwa Wilayani Kibiti kwa mujibu wa Fomu ya Kuweka Mapingamizi dhidi ya Mgombea Urais Amesema Rais Magufuli alipokuwa akigawa fedha kwa ajili ya madawati na shule alikiuka sababu ya 16 kwenye Fomu hiyo inayosema Mgombea Urais anaweza kuwekewa pingamizi iwapo atakiuka Makatazo yaliyotatwa kwenye sheria ya gharama za Uchaguzi
Mhe. Tundu Lissu mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA ameendelea kusisitiza kuwa hawezi kufungwa kwa kesi alizo nazo Mahakamani na kwamba haziwezi kumzuia kugombea Urais.
“Hafungwi mtu hapa” “Nina kesi sita Kisutu na zote ni za uchochezi.” Baraza Kuu la chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, limemchagua Tundu Lissu kuwa mgombea wake wa Urais katika Uchaguzi Mkuu 2020.
Mhe. Lissu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa si yeye tu anayeweza kuwekewa pingamizi la kugombea Urais bali hata Mhe. Rais Magufuli pia anaweza kuwekewa pingamizi.
"Nani aliyesema kwamba CCM hawawezi kuwekewa mapingamizi? Nani aliyesema mgombea urais wa CCM, John Magufuli hawezi kuwekewa mapingamizi? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa CHADEMA"
Kwenye fomu ya mapingamizi, kwenye sababu 16, la 16 Magufuli amekiuka Mambo yaliyokatazwa moja wapo ni rushwa maana ukishaingia kwenye uchaguzi huruhusiwi kutoa rushwa, Magufuli akiwa anatoka kumzika Mkapa Lupaso, alifanya nini Kibiti? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa
CHADEMA
Lissu amesema kitendo cha Rais kutoa fedha Kibiti, kununua jogoo kwa Laki Moja ni rushwa wakati wa uchaguzi.
Mhe. Lissu katika moja ya sera zake amesema iwapo atashinda basi atakuwa na jukumu kubwa la kurudisha uhusiano wa nchi kimataifa.
"Tukishinda urais wa Tanzania, mimi nitakuwa Rais wa Katiba mpya. Kama tunataka mfumo mzuri wa utawala, mahali pa kuanzia ni Katiba mpya. Hii ndilo tutaanza nalo. Haina maana hatutajenga shule, kuboresha Sekta ya Afya '
MY TAKE: Bado tutandelea kushuhudia matamko mengi kwenye Uchaguzi huu ni juu yetu watanzania kumpima kila mgombea ili tupate kiongozi bora kwa maslahi mapana ya Taifa letu.