Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli alitoa rushwa Kibiti Mil. 5 na akanunua jogoo laki moja wakati kashapitishwa kugombea Urais. Nitamuwekea pingamizi

Namshauri apunguze kuchomeka kingereza kwenye hotuba. Sisi wengine anatuchanganya.

Pia aelezee mipango ya kiuchumi kulegeza vyuma pamoja na masuala ya ajira aliyonayo kwa vijana. Wengi tumejaa kitaaaaani.

Tundu Lissu pokea maoni.

Wengine wenye maoni endeleeni kuyatoa.
 
Anazungumzia chama na mtu aliyeko madarakani. Lazima aonyeshe wameshindwa wapi.
Endelea kumsikiliza
 
Binafsi nshindwa kuelewa kwanini mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo kila akipanda jukwaani ni CCM mpaka anamaliza hotuba yake.

Anatumia muda wote kuiongelea CCM na serikali yake. Tumia jukwaa kutuambia unaenda kutufanyia nini Watanzania ambacho serikali zote za CCM zilishindwa...
Vijana bhana walio CCM nawaonea huruma sana
 
Wale walinzi wa serikali pale kwenye makazi ya viongozi siku Lissu anashambuliwa walikuwa wapi?
 
Amesema Rais Magufuli huku akiwa ameshatangazwa kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM kwenye Uchaguzi wa Oktoba 2020 ametoa rushwa Wilayani Kibiti kwa mujibu wa Fomu ya Kuweka Mapingamizi dhidi ya Mgombea Urais Amesema Rais Magufuli alipokuwa akigawa fedha kwa ajili ya madawati na shule alikiuka sababu ya 16 kwenye Fomu hiyo inayosema Mgombea Urais anaweza kuwekewa pingamizi iwapo atakiuka Makatazo yaliyotatwa kwenye sheria ya gharama za Uchaguzi



Mhe. Tundu Lissu mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA ameendelea kusisitiza kuwa hawezi kufungwa kwa kesi alizo nazo Mahakamani na kwamba haziwezi kumzuia kugombea Urais.

“Hafungwi mtu hapa” “Nina kesi sita Kisutu na zote ni za uchochezi.” Baraza Kuu la chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, limemchagua Tundu Lissu kuwa mgombea wake wa Urais katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Mhe. Lissu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa si yeye tu anayeweza kuwekewa pingamizi la kugombea Urais bali hata Mhe. Rais Magufuli pia anaweza kuwekewa pingamizi.

"Nani aliyesema kwamba CCM hawawezi kuwekewa mapingamizi? Nani aliyesema mgombea urais wa CCM, John Magufuli hawezi kuwekewa mapingamizi.? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa CHADEMA"

Kwenye fomu ya mapingamizi, kwenye sababu 16, la 16 Magufuli amekiuka Mambo yaliyokatazwa moja wapo ni rushwa maana ukishaingia kwenye uchaguzi huruhusiwi kutoa rushwa, Magufuli akiwa anatoka kumzika Mkapa Lupaso, alifanya nini Kibiti? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa
CHADEMA

Lissu amesema kitendo cha Rais kutoa fedha Kibiti, kununua jogoo kwa Laki Moja ni rushwa wakati wa uchaguzi.

Mhe. Lissu katika moja ya sera zake amesema iwapo atashinda basi atakuwa na jukumu kubwa la kurudisha uhusiano wa nchi kimataifa.

"Tukishinda urais wa Tanzania, mimi nitakuwa Rais wa Katiba mpya. Kama tunataka mfumo mzuri wa utawala, mahali pa kuanzia ni Katiba mpya. Hii ndilo tutaanza nalo. Haina maana hatutajenga shule, kuboresha Sekta ya Afya '

MY TAKE: Bado tutandelea kushuhudia matamko mengi kwenye Uchaguzi huu ni juu yetu watanzania kumpima kila mgombea ili tupate kiongozi bora kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
TAKUKURU HAWAMSIKII LISU?
 
Rais ndio amekuwa nominated na CCM kugombea nafasi ya Urais.

Ila Bado hatupo kwenye Campaign process ambapo ndipo vyama huuza sera baada ya wagombea wake kuidhinishwa na NEC.

Pia hatupo kwenye Election. (Uchaguzi).

Rais yupo kwenye majukumu yake ya kawaida kabisa.

Hivyo Hawa wapiga kelele hawana hoja.
Utopolo
Screenshot_20200806-223932_Twitter.jpeg
 
Mkuu acha kuweweseka,mwaka huu mnapenda kushitaki wapi? Uchaguzi wa mwaka 2015 mlikimbilia CCJ mwaka huu MNA mawakli wa Amsterdam, hivi ni vituko.

Kila Mara twawambieni huyu lissu hafai anawapotosheni ninyi hapana kuelewa.

Lissu hafai anapaswa kupingwa na kila mtanzania mpenda amani naaendeleo.

Fool you
 
Hayo yamesemwa na Mwanasharia nguli duniani na mgombea Urais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzani kupitia Chadema ndugu Tundu Lissu!

Tundu Lissu amesema kitendo cha Rais Magufuli kupewa jogoo huko Kilwa na kulipa shilingi laki moja ni kitendo cha utoaji wa rushwa kwa wapiga kura kwani bei ya jogoo inajulikani ni shilingi elfu kumi tu.

Pamoja na malipo hayo makubwa kwa jogoo, Lissu amesema hata ile milioni tano aliyotoa Rais Magufuli kwa ajili ya shule pia ni rushwa kwani matendo hayo yamefanyika wakati rais Magufuli akijua yeye ni Mugombea!

Kwa kuwa vitendo hivyo vinakatazwa na sheria za Uchaguzi, Lissu anakusidia kumuwekea pingamizi Rais Magufuli asiteuliwe n Tume ya Uchaguzi kupeperusha bendera ya CCM.

Ushauri wa bure kwa CCM wabadili gia haraka, kwani kuna uwezekano mkubwa Rais Magufuli asiteuliwe na Tume kwa makosa aliyofanya ya kukiuka sheria za Uchaguzi!



Tume ipi unayosemea😁😁 husikii kila siku tunalilia tume huru
 
Back
Top Bottom