Tundu Lissu: Profesa wetu wa sheria hajui sheria zetu?

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,459
2,000
PROFESA WETU WA SHERIA HAJUI SHERIA ZETU???

Tundu AM Lissu, MP
Tienen, Ubelgiji

Nimemsikia Waziri wetu mpya wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi akifokea na kutishia watu anaodai wanaisema vibaya na 'kuibagaza' nchi yetu.

Profesa Kabudi anatakiwa afahamu kwamba Watanzania sio tena watu wa kufokewa na kutishiwa kama watoto wa shule wa zamani.

Pili, kwa vile ni profesa wa sheria anayeelekea kutokufahamu au kuamini matakwa ya Katiba na Sheria za nchi yetu, nawaombeni mmwambie Profesa Kabudi mambo yafuatayo:

1. Kwamba, kwa mujibu wa Katiba yetu, kuna tofauti kubwa kati ya 'nchi' na 'Serikali.'

(a) 'Nchi' ya Tanzania ni ile inayotamkwa kwenye ibara ya 1 na 2(1) ya Katiba kuwa "... ni Jamhuri ya Muungano (inayojumuisha) ... eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo."

(b) Kwa upande mwingine, 'Serikali' ya Tanzania imefafanuliwa katika ibara ya 6 ya Katiba kuwa "... ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali za mitaa na pia mtu anayetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote."

(c) Matendo maovu ya vyombo vya usalama kama Jeshi la Polisi au Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi; au ya viongozi wa serikali kama Rais, Mawaziri au Wakuu wa Mikoa na Wilaya; au watendaji wake wengine, sio matendo ya 'nchi' bali ni matendo ya 'Serikali.'

Matendo haya ya 'Serikali' yanaweza yakapingwa, kubezwa, kubagazwa, kusemwa vibaya au kuchafuliwa bila kuichafua au kuibeza au kuibagaza 'Nchi.'

2. Kwamba kuisema Serikali vibaya, au kuibagaza, au kuichafua - ndani au nje ya nchi - kwa sababu ya matendo yake maovu - sio kosa bali ni wajibu wa kila mtu na hasa kila raia wa Tanzania.

(a) Kwa mujibu wa ibara ya 3(1) ya Katiba yetu, Tanzania "... ni nchi ya kidemokrasia ... yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa." Nchi yetu sio ya Chama kimoja kama ilivyokuwa zamani, kwa hiyo kuipinga au kuikosoa Serikali iliyoko madarakani sio kosa, bali ni kutekeleza matakwa ya Katiba.

(b) Kwa mujibu wa ibara ya 8(1)(a) "... wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi...."

Aidha, ibara ya 8(1)(c) inasisitiza kwamba "Serikali itawajibika kwa wananchi." Kwa maana hiyo, sisi wananchi ndio tuko juu ya Serikali.

Kuipinga, kuisema vibaya, kuibagaza au kuichafua Serikali hiyo kutokana na matendo yake maovu, hakuwezi kuwa kosa hata kidogo, bali ni sehemu ya kuiwajibisha kwetu.

3. Mwambieni Profesa Kabudi kwamba Serikali yetu ina wajibu mbele ya jumuiya ya kimataifa wa kuheshimu haki za binadamu zilizoainishwa kwenye Katiba yetu.

(a) Ibara ya 9(f) ya Katiba inaitaka "... Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote ... kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha ... kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu."

(b) Serikali yetu imesaini mikataba mbali mbali ya kimataifa na ya kikanda inayotulazimu kuheshimu haki za binadamu za wananchi wetu.

(c) Serikali yetu imekubali, kwa kusaini Mkataba wa Roma unaounda Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, kwamba itawajibika kwa jumuiya ya kimataifa kwa vitendo vyovyote vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyokatazwa na Mkataba wa Roma.

(d) Kama sehemu ya uwajibikaji wetu mbele ya jumuiya ya kimataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu, Serikali yetu inatakiwa kupeleka taarifa ya utekelezaji wa wajibu wake huo kwenye vyombo vya uwajibikaji vya kimataifa, kama vile Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa. Hivi ndivyo alivyofanya Profesa Kabudi mwenyewe wiki iliyopita kule Geneva, Uswisi.

Kwa sababu hiyo, kuisema vibaya Serikali yetu nje ya Tanzania, kwa sababu ya matendo yake maovu dhidi ya Watanzania, ni sehemu tu ya kuitaka Serikali yetu iwajibike kwa jumuiya ya kimataifa kwa mambo ambayo tumekubali kuwajibika nayo kimataifa.

4. Mwambieni Profesa Kabudi kwamba Katiba yetu imetupatia 'Haki ya Uhuru wa Mawazo' na 'Uhuru wa Maoni.' Kwa mujibu wa ibara ya 18(1), "... kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati."

Kwa sababu zote hizi, mwambieni Profesa Kabudi kwamba kama yeye na Serikali anayoitumikia hawaamini matakwa haya ya Katibaya nchi yetu, sisi tunayaamini na tutayatekeleza matakwa hayo ya Katiba.

Mwambieni Profesa Kabudi kwamba hatutanyamazishwa na uovu wao, au vitisho vyao, au na ulaghai na propaganda zao, au na hongo na rushwa zao.

Mwambieni Profesa Kabudi kwamba tutaendelea kuyasema hadharani, popote pale, ndani na nje ya Tanzania, maovu ya Serikali yetu, na ya vyombo vyake, na ya viongozi wake na ya watendaji wake.

4 Machi, 2019
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
12,907

Maskini palamagamba,amevuliwa nguo tena.Andhni huko nje atasindikizwa na wasiojulikana?
 
wa mchangani

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
1,419
2,000
huna jipya ndugu na sasa ndiyo utatueleza kinachokufanya uropokeropoke huko uliko au dishi limeyumba tuila kwanza upone
Mkuu ulikuwa usingizini nn mbona umeshtuka utadhani uko ndotoni,anayosema yamo kwenye katiba hajatoa kichwani mwake,yeye sio kama baba jesca anayeamini kwamba matamko yake ndo sheria ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,469
2,000
huna jipya ndugu na sasa ndiyo utatueleza kinachokufanya uropokeropoke huko uliko au dishi limeyumba tuila kwanza upone
Ha ha ha! Propesa wenu anapewa ukweli! serikali kama ni dhalimu kila raia anapaswa kuisema, kuizodoa na hata ikibidi kufanya kila liweekanalo kuiondoa. Ila serikali inayofuata misingi ya katiba na sharia na kuheshimu utu wa watu itasifiwa kuimbiwa na kupongezwa kwa vigelegele.
Lissu endelea kuwapa shule wanafiki wanao ujua ukweli lakini kwa kujipendekeza wanaupotosha.
 
tzkwanza

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,390
2,000
huna jipya ndugu na sasa ndiyo utatueleza kinachokufanya uropokeropoke huko uliko au dishi limeyumba tuila kwanza upone
Kabudi na uprofesa wake wote anawalamba miguu wanasiasa kisa cheo.
Njaa ni mbaya sana.
Halafu hawa maprofesa utasikia wanawambia vijana wajiajiri wakati wao wanaishi kwa uongo na unafiki, ndio kujiajiri huko????!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom