Tundu Lissu: Prof. Kabudi anajipendekeza na kujikomba kwa wanasiasa walioko madarakani miaka yake yote

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,439
50,960
*Inaandikwa na Mhe Tundu Lissu*

Katika kitabu chake 'Intellectuals at the Hill' (kilichapishwa miaka ya kati ya '90), Prof. Issa G. Shivji aliwahi kusema kuwa kuna tabia ya wasomi wetu kujipendekeza na kujikomba kwa watawala na kufanya mambo ya hovyo kuliko warasimu wa kawaida, hasa wanapopewa vyeo vya uteuzi na Rais.

Prof. Pala Kabudi ni mfano mzuri wa wasomi wa aina hii. Ni mtu ambaye amejipendekeza na kujikomba kwa wanasiasa walioko madarakani miaka yake yote ya kitaaluma.

Ukiachia msimamo wake akiwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambao mimi binafsi niliushangaa sana, Prof. Kabudi hana historia yoyote ya msimamo huru katika masuala muhimu ya nchi.

Ana akili za kitaaluma nyingi sana, lakini ana tabia ya kujikomba na kujipendekeza inayotia kinyaa na kufuta sifa zote za usomi wake.

Alitumiwa sana na Serikali ya Jakaya Kikwete na ya Ben Mkapa kabla ya hapo kama consultant wa masuala mbali mbali ya kisheria. Kwa hiyo anahusika kwa kiasi fulani na uchafu wa Kikwete na Mkapa ambao yeye na Magufuli wanajifanya kuukataa sasa.

Alikuwa mwandishi habari wa Uhuru/Mzalendo wakati wa Vita ya Kagera na, aliwahi kutuambia akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya LEAT, alitunukiwa zawadi na Mwalimu Nyerere kwa uandishi wa makala za propaganda zilizokuwa zinahusu Vita hiyo.

Prof. Kabudi amekuwa Chuo Kikuu cha Dar, kama mwanafunzi na kama mwalimu, tangu mwaka '80 hadi alipostaafu mwaka '16. Amekaa Ujerumani na kusomea Frei Universiteit Berlin, mojawapo ya vyuo vikuu maarufu kabisa barani Ulaya na duniani, kwa miaka 9.

Amekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar, na mjumbe wa Tume ya Katiba aliyeteuliwa na Rais Kikwete.

Huyu mtoto wa Mchungaji wa Kanisa la Anglican, sio mtu aliyezaliwa kwenye vumbi na kuishi kwenye ufukara. Hakutolewa jalalani kokote na Rais Magufuli. Amekuwa na bado ni sehemu ya top elite ya Tanzania.

Alichokisema mbele ya Rais Magufuli sio cha kweli hata kidogo, lakini ni ishara kamili ya hulka yake ya kujidhalili na kujikomba ili aendelee kutumikia Jimbo lake kuu la uchaguzi: tumbo lake.

Pamoja na kuwa ni Mgogo, Prof. Pala Kabudi ni Msingida mwenzetu. Bibi yake ni Mnyaturu wa kwetu. Baba na Mama yake ni wazaliwa wa Kilimatinde, na yeye mwenyewe amesomea shule ya msingi mojawapo ya Singida mjini.

Kujikomba na kujidhalili mbele ya Rais Magufuli kumechafua sifa na hadhi ya wasomi wetu kwa ujumla. Kwa sisi Wasingida wenzake, ametushushia heshima yetu sana. Tuna kila sababu na haki ya kumzodoa na kumkanya kwa upumbavu wake huu.
 
Kuwa fuatilia wanasiasa ni kazi sana.

Lisu na Kabudi wote ni wale wale, kama ni mbwa wote ni mbwa sema tofauti yao mmoja yupo kwenye nyumba mwingine anaishi na kuokoteza jalalani.
 
Bwaaahaaa bwaaahaa, nimecheka ile mbaya, eti jimbo lake la uchaguzi eti tumbo lake. Nimesema na ninarudia tena hata kwa wale wanaomtetea Kubudi, jamaa anajipendekeza kupita kiasi mpaka rais mwenyewe anajua kwamba Kabudi anajipendekeza, ndio maana anafikia mahali anasema hadharani kuwa huwa anamtukana.
 
Profess kabudi katengeneza ajira kwa watanzania nje wakati Yeye Tundu Lisu anazurura na bakuli kuwaomba walioajiriwa wamchangie pesa ya kula,pango,nguo na ada za kusomesha watoto!!! Anayeaibisha hapo? Ni Nani Ni Lisu.Tabia ya kuomba omba sio ya wanyaturu.Lisu ndie omba omba wa kwanza mnyaturu Mimi kumwona toka nizaliwe.Sijawahi kutana na omba omba wa kinyaturu zaidi ya Tundu Lisu
 
*Inaandikwa na Mhe Tundu Lissu*

Katika kitabu chake 'Intellectuals at the Hill' (kilichapishwa miaka ya kati ya '90), Prof. Issa G. Shivji aliwahi kusema kuwa kuna tabia ya wasomi wetu kujipendekeza na kujikomba kwa watawala na kufanya mambo ya hovyo kuliko warasimu wa kawaida, hasa wanapopewa vyeo vya uteuzi na Rais.

Prof. Pala Kabudi ni mfano mzuri wa wasomi wa aina hii. Ni mtu ambaye amejipendekeza na kujikomba kwa wanasiasa walioko madarakani miaka yake yote ya kitaaluma.

Ukiachia msimamo wake akiwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambao mimi binafsi niliushangaa sana, Prof. Kabudi hana historia yoyote ya msimamo huru katika masuala muhimu ya nchi.

Ana akili za kitaaluma nyingi sana, lakini ana tabia ya kujikomba na kujipendekeza inayotia kinyaa na kufuta sifa zote za usomi wake.

Alitumiwa sana na Serikali ya Jakaya Kikwete na ya Ben Mkapa kabla ya hapo kama consultant wa masuala mbali mbali ya kisheria. Kwa hiyo anahusika kwa kiasi fulani na uchafu wa Kikwete na Mkapa ambao yeye na Magufuli wanajifanya kuukataa sasa.

Alikuwa mwandishi habari wa Uhuru/Mzalendo wakati wa Vita ya Kagera na, aliwahi kutuambia akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya LEAT, alitunukiwa zawadi na Mwalimu Nyerere kwa uandishi wa makala za propaganda zilizokuwa zinahusu Vita hiyo.

Prof. Kabudi amekuwa Chuo Kikuu cha Dar, kama mwanafunzi na kama mwalimu, tangu mwaka '80 hadi alipostaafu mwaka '16. Amekaa Ujerumani na kusomea Frei Universiteit Berlin, mojawapo ya vyuo vikuu maarufu kabisa barani Ulaya na duniani, kwa miaka 9.

Amekuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar, na mjumbe wa Tume ya Katiba aliyeteuliwa na Rais Kikwete.

Huyu mtoto wa Mchungaji wa Kanisa la Anglican, sio mtu aliyezaliwa kwenye vumbi na kuishi kwenye ufukara. Hakutolewa jalalani kokote na Rais Magufuli. Amekuwa na bado ni sehemu ya top elite ya Tanzania.

Alichokisema mbele ya Rais Magufuli sio cha kweli hata kidogo, lakini ni ishara kamili ya hulka yake ya kujidhalili na kujikomba ili aendelee kutumikia Jimbo lake kuu la uchaguzi: tumbo lake.

Pamoja na kuwa ni Mgogo, Prof. Pala Kabudi ni Msingida mwenzetu. Bibi yake ni Mnyaturu wa kwetu. Baba na Mama yake ni wazaliwa wa Kilimatinde, na yeye mwenyewe amesomea shule ya msingi mojawapo ya Singida mjini.

Kujikomba na kujidhalili mbele ya Rais Magufuli kumechafua sifa na hadhi ya wasomi wetu kwa ujumla. Kwa sisi Wasingida wenzake, ametushushia heshima yetu sana. Tuna kila sababu na haki ya kumzodoa na kumkanya kwa upumbavu wake huu.
Wachumia tumbo watanajisi sana tu taaluma na kushusha hadhi ya elimu ndio maana tunaambiwa "WA LA SABA WANATOSHA!!:
 
Ni nani msomi aliyeteuliwa na Rais Magufuli yuko tofauti na Professor Kabudi ? Je ! Dk. Kitila Mkumbo kutoka Singida kama Tundu Lissu ? TUSIINGILIE UHURU WA MAWAZO YA WATU KWA MISINGI YA UBAGUZI.

Nape, Mwigulu, Januari nk, ndio maana akawatumbua hao wawili huku Januari akiwa katika wakati mgumu sana. Kabudi na Makonda wanajikomba mpaka wanatia kinyaa.
 
Bwaaahaaa bwaaahaa, nimecheka ile mbaya, eti jimbo lake la uchaguzi eti tumbo lake. Nimesema na ninarudia tena hata kwa wale wanaomtetea Kubudi, jamaa anajipendekeza kupita kiasi mpaka rais mwenyewe anajua kwamba Kabudi anajipendekeza, ndio maana anafikia mahali anasema hadharani kuwa huwa anamtukana.
Profesa anayejibaghaza!!!
 
Bwana nkubwa keshawashtukia "WAPUMBAVU"
 
Profess kabudi katengeneza ajira kwa watanzania nje wakati Yeye Tundu Lisu anazurura na bakuli kuwaomba walioajiriwa wamchangie pesa ya pango,nguo na ada za kusomesha watoto!!! Anayeaibisha happy Ni Nani Ni Lisu.Tabia ya kuomba omba sio ya wanyaturu.Lisu ndie omba omba wa kwanza mnyaturu Mimi kumwona toka nizaliwe.Sijawahi kutana na omba omba wa kinyaturu zaidi ya Tundu Lisu
Sikufahamu kwamba Kabudi aliwahi kuwa mwandishi wa Gazeti la Uhuru .
 
Similar Discussions

63 Reactions
Reply
Back
Top Bottom