Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Tundu Lissu anasema atalipa malimbikizo yote ya mishahara na kupandisha vyeo vyote vilivyosimama toka mwaka 2015 mpaka leo 2020.

Anasema lazima wafanyakazi walipwe fidia na Serikali yake.

Anasema atawalipa pia fidia wote waliofukuzwa kazi na Serikali ya CCM ndani ya hii miaka 5.

Anasema atarudisha makato ya loan board kutoka 15% na kuwa 3%

Na yatakuwa kwa wale tu watakao kuwa na kazi za kueleweka ndani ya serikali yake.

Anasema atafumua mfumo wa elimu ili utoke kwenye kujibu mithihani na kuwa elimu ya maarifa na kujitegemea na kuajirika kirahisi.

Anasema ataifumua TRA na kuanzisha mfumo wa Kodi moja ili nchi zote zilizo tuzunguka zije kununua bidhaa bandarini na kwenye maduka yetu ya ndani.

View attachment 1552154View attachment 1552155
 
Back
Top Bottom