Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitabadili Katiba ili wabunge wawe na maamuzi juu ya fedha za Serikali

Dada RMC, hakuna sehemu yoyote katika uzi wangu nilizungumzia uchumi! Nina mashaka kama wewe ni mchumi, huenda ni mtu uliyesomea uchumi tu. Hiyo haikufanyi kuwa mchumi. Umeshindwa kutambua kuwa mada hapa ni "process flow". Ukisikiliza kampeni za CCM utasikia mbunge wa upinzani akilaumiwa kwa kukosekana kwa barabara, maji nk. Na unachoeleza hapa ni kwanini vitu hivo havitapatikana iwe ni mbunge wa CCM au upinzani kwa sababu ya hiyo "process flow" uliyoieleza (na sijui kama unatambua hilo).

Unajiita umeelimika, I dispute that. Umeenda shule tu na ukatoka na tofauti kidogo sana na ulivoingia (zaidi sana umetoka na umri mkubwa, cheti na kujidai kwingi). Anachosema Lissu (na nikufahamishe mie sio muumini wa vyama vya siasa - i am apolitical) ni kuwa process flows zipelekwe chini kwenye halmashauri ambazo zina madiwani. Watafanya maamuzi locally!! Ungekuwa msomi ungejua kuwa kuna mambo mengine ni ya kitaifa na mengine ni ya kimaeneo. Jambo la kujenga reli, bwawa la umeme, ulinzi, mikopo ya wanafunzi ni ya kitaifa. Swala la kujenga shule, zahanati, madawati, barabara ndogo ni za kimaeneo!! Hayo waachiwe madiwani katika ngazi za halmashauri. Ulichoshindwa kuelewa dada yangu ni hiki - centralization vis-a-vis decentralization!!! Na bado unajiita msomi. Ikiwa hivo, inabaki kuwajibisha madiwani jinsi financial resources zinatumika na hapo ndipo diwani au mbunge anaweza kuulizwa barabara, zahanati, shule na madawayti viko wapi!!!

Ushauri. Jiepushe kujifaya unamfahamu mtu usieyemfahamu. Mimi sio mzururaji kama ulivosema na unaweza kujikuta nakuzidi mbali sana kwa kila jambo. Ni mchumi na umeajiriwa?? My sister, jiajiri na uchumi wako huo na utakuwa a better person financially. Unless ni mchumi wa benki kubwa. Kama umeajiriwa nje ya taaluma yako - wewe sio mchumi, umesomea uchumi tu! Huna experience na chochote kinachoitwa uchumi!! Na ndio maana uelewa wako wa mambo haya ni wa kiwango cha chini. Mada hii ilihusu decision-making!!
Majibu yako hayana hoja za msingi.

Kwanza nikukanushe kuwa mimi sio dada ni mwanaume . Nami nakushauri jiepushe kujifanya unamfahamu mtu usiyemfahamu

Umedai kuwa mimi sio mchumi ingawa nimesomea uchumi! Kwa vigezo vya kichwani mwako kweli sio mchumi, ila kwa mujibu wa accredition authorities za Tanzania na dunia nzima mimi natambulika kama mchumi kwa sababu nimesoma na kuhitimu katika vyuo vinavyotambulika na mamlaka za ithibati Tanzania na dunia kwa ujumla; pia licha ya kusomea nimeajiriwa kama mchumi kwa miaka mingi tu tofauti na unavyobet. Sikushangai wewe na wenzako wa calibre yako kwa sababu mnadhani standard mbali mbali zinazotumika kupima mambo duniani ni zile zinazotokana na mihemko ya mwanasiasa wenu. Ndio maana mnakataa kuwa Tanzania haijaingia katika uchumi wa kati ingawa mmlaka yenye dhamana (World Bank) na ambayo imegwawanya uchumi wa nchi zote za dunia katika makundi manne inaitangaza rasmi Tanzania kuwa ni lower middle income country kutokana na kukidhi kigezo cha kipato kwamtu mmoja. Hii inaonyesha jinsi ilivyo hatari kubwa iwapo itatokea mtu wenu akachukua uongozi wa nchi maana ataivuruga mifumo yote ili kukidhi mihemko yake.

Majibu yako yanaonyesha hujui majukumu ya mbunge na diwani katika mchakato mzima wa kutatua kero au kusukuma maendeleo ya eneo analowakilisha. Unafikiri vile vikao vya madiwani huwa wakikutana wanafanya nini kama hawazungumzii na kupanga mipango yao ya maendeleo na kutatua kero? Unafahamu kitu kinachoitwa D by D (sikutajii kirefu chake hapa kwa makusudi). Nikufahamishe kuwa wananchi huwa wanapata fursa ya kueleza au kuamua wanahitaji nini na kuna miradi mingi tu ya maendeleo imewahi kuibuliwa na wananchi na ikapitishwa na Baraza la Madiwani na serikali ikaridhia na kutoa fedha za utekelezaji wake . Binafsi nimewahi kushiriki na kushuhudia katika michakato ya wananchi kuibua miradi ya maendeleo ila kwa kuzingatia uwezo wa kifedha uliopo kwa wakati husika (ceiling). Tofauti ya Lissu na kinachofanyika sasa ni kuwa wewe na Lissu wako mnadhani kila kitu kinawezekana kufanyika na kuwa pesa sio tatizo maana pesa ya kufanya kila kitu ipo wakati wote jambo ambalo sio kweli kwani nadharia za uchumi na uhalisia ni kuwa resources ziko limited lakini mahitaji ni unlimited.

Unadai sielewi centralization na decentralization! wewe ndio hufahamu na unaimba tu kama kasuku, mimi sio tu naifahamu lakini pia nimeshiriki kufanya kazi ndani ya mifumo hiyo na bado ninafanya kazi.

Kuhusu madai yako kuwa umenizidi, hapa duniani kuzidiana katika mambo mbali mbali kupo na sio kosa mmoja kuzidiwa au kumzidi mwingine, mfano kama umezaliwa kabla yangu maana yake unanizidi na kama umesoma kuliko mimi umenizidi lakini kupitia hayo majibu yako yamenithibitishia contrary na unavyojitapa.
 
yeye si anasema anaheshimu katiba isiyoruhu kuingilia faragha za watu kwa hiyo anatakiwa pia kuheshimu katiba kama inasema hivyo anavyodai asijitie anaweka double standard kwenye katiba
 
Back
Top Bottom