Tundu Lissu: Niliposhambuliwa walisema nimeshambuliwa na waliotumwa na Mbowe sababu ya kugombea madaraka ya chama

Historia yake inaonyesha huwa ni mzushi na muongo.Ndo maana hata mabeberu wamempuuza yupo yupo tu wala hawamshobokei tena kama mwanzo.
Hakuna kitu kiliwaudhi wazungu kama kuponda serikali ununuzi wa ndege za bombardier na Boeing. Mzungu unataka akose pesa? hamtaelewana milele.Upinzani pale ndipo ulipoopoteza dira Zitto akachafua hadi kusema ndege zinazoletwa ni mitumba.Yaani kampuni kubwa inayoheshimika duniani aseme inaleta mitumba!

Sasa hivi wazungu hawauoni upinzani kama rafiki yao wa kweli.SErikali inasema tununue ndege viwanda vya wazungu upinzani chadema, nk unakuja unasema hapana aiseee watacheka na wewe kinafiki lakini hawaji kusimama na wewe
 
Kuna watu humu ndani Lissu anawakera kweli, hampendi kumsikia halafu na yeye kama ameshawajua vile, kila siku yuko hewani.

Na bado.
 
@uinine,
Kwani kazi zote za uchunguzi Tanzania huwa zinafanywa na nani? mtu kapigwa,kaibiwa,katapeliwa nk kwa ujuaji wako koko huwa zinafanywa na nani kisheria?
Waliokuwa wajuaji koko wa Nkurunzinza kama wewe wakati huu wanajuta, na nyie soon mtabaki peupe.
 
Kuna watu humu ndani Lissu anawakera kweli, hampendi kumsikia halafu na yeye kama ameshawajua vile, kila siku yuko hewani.

Na bado.
Issue ni substance ya anachoonge sio tu kuongea kisa na sababu eti domo ni jumba la maneno kwa hiyo lazima aongee!!!!!
 
Maneno yote haya ya hovyo unamweleza nani?
Namwambia Tundu Lisu aliyekuwa akipiga vita Magufuli kununua ndege viwanda vya wazungu.Magufuli anataka kuwapa pesa wazungu akina Tundu Lisu wakawa wanapinga.Safari hii CHADEMA SAHAUNI PESA za wazungu wakati wa kampeni

Mlizuia serikali isinunue ndege wapate pesa mnataka pesa za kuwapa zitoke wapi wakati mnaponda biashara zao za kuingiza pesa?

CCM tukiomba watatupa sababu ni partners wao kwenye biashara tunawapa pesa kwa hiyo kuchota hapo kidogo watupe kazi ndogo kwao nyie wapiga vita biashara zao mtajijua mnadhani wao ndio wana uchungu sana na nyie wakati nyie hamna uchungu wa wao kukosa pesa kwa mauzo ya ndege zao mnataka ziwadodee halafu nyie mambo yenu yaende!!! mna akili nyie?.Uchaguzi huu mtapata majibu ya wazungu hampati pesa
 
Namwambia Tundu Lisu aliyekuwa akipiga vita Magufuli kununua ndege viwanda vya wazungu.Magufuli anataka kuwapa pesa wazungu akina Tundu Lisu wakawa wanapinga.Safari hii CHADEMA SAHAUNI PESA za wazungu wakati wa kampeni

Mlizuia serikali isinunue ndege wapate pesa mnataka pesa za kuwapa zitoke wapi wakati mnaponda biashara zao za kuingiza pesa?

CCM tukiomba watatupa sababu ni partners wao kwenye biashara tunawapa pesa kwa hiyo kuchota hapo kidogo watupe kazi ndogo kwao nyie wapiga vita biashara zao mtajijua mnadhani wao ndio wana uchungu sana na nyie wakati nyie hamna uchungu wa wao kukosa pesa kwa mauzo ya ndege zao mnataka ziwadodee halafu nyie mambo yenu yaende!!! mna akili nyie.Uchaguzi huu mtapata majibu ya wazungu hampati pesa
Leo wazungu wamekuwa partners wa CCM siyo mabeberu tena, kweli ukiwa CCM akili unaziacha mlangoni.
 
Tukumbuke Mnyika alisema wakati tukio linatokea,Mbowe hakuwa peke yake hivyo leo tunaweza kusikia kuhusu ni kina nani walikuwepo na walishuhudia nini au walitenda nini.
Hao waliokua na mwamba tuvushe ndio wa kutuambia,sio huyo mkimbizi wa kiuchumi
 
Wale waliosema Mbowe alikuwa amelewa, huenda wakaumbuka leo hii.

Kama yeye alishambuliwa na alishiwda kutaja aliyemshambulia kipindi cha hard talk na yule mwingereza sasa ya mbowe atayaweza kweli wakati yuko lockdown huko?
 
Eti kwenye ngazi!! Mbona mchezo uliishioa hapa? hili lilikuwa kosa kubwa kutaja ngazi
Kwenye ngazi jibu ni kwamba alisukumwa akaanguka. Kama alisukumwa na INTERNAL au EXTERNAL FORCE hilo ndo la kuchunguza.
 
"Leo Mbowe ameumizwa akiwa kwake na kauli zilezile za kudharau, kukejeli zimeanza kutolewa tena, sasa tunawasikia Viongozi na Watendaji wa Serikali na Wapambe wao ndani na nje ya Bunge wakitoa kauli za kejeli kwamba Mbowe hakushambiliwa"

“Abdul Nondo alipotekwa kuteswa na kutupwa Mafinga, hadithi zikawa zilezile za Azory Gwanda na Ben Saanane, kwamba Abdul amejiteka na kujipeleka kwa mchumba wake Mafinga, Polisi iliahidi kuchunguza kwa kina kuhusu kushambuliwa kwangu na hadi leo taarifa haijatolewa na Polisi hawana Mtuhumiwa wala Mshukiwa, kama ilivyokuwa kwangu na hili la Mbowe tunaambiwa tusubiri uchunguzi"

"Niliposhambuliwa walisema nilijishambulia mwenyewe, nimejipiga risasi, baadae nimeshambuliwa na waliotumwa na Mbowe sababu ya kugombea Madaraka ya Chama, baadae ikawa uchunguzi hauwezi kufanyika kwasababu CHADEMA wamemtorosha Dereva wangu na mimi nimekimbia kesi"

"Kama ilivyokuwa kwangu eneo hilo pia lina ulinzi mkali na wa muda wote, kama ilivyokuwa kwangu Walinzi wote waliondolewa katika eneo hilo, mara hii tumeambiwa ni kwa ajili ya kuwaepusha na corona, mara wanahoji Mbowe alikuwa wapi na anafanya nini usiku wa manane hadi ashambuliwe, wengine wanahoji kwanini alikuwa anatembea peke yake bila mlinzi binafsi, kunywa pombe na kulewa sio kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na halihalalishi mashambulizi"

“Tunawaomba Wananchi wote wanaochukizwa na vitendo hivi kuvipigia kelele kila Mahali, tunashukuru Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Balozi wa Nchi za Nje na Taasisi za Kiraia wameanza kulisema jambo hili kwa kulitolea kauli, tunaomba wazidishe kelele hizi" -Tundu Lissu
 
Acha kushadadia mambo usiyoyajua, huo ni umbea. Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo kwa nini wasipeleke maelezo yao kwa vyombo husika, ili taratibu za kisheria za upelelezi ufuatwe? Halafu Huyo Lissu ni mwanasheria, anafahamu kuwa ni kosa la kisheria kuhukumu jambo pasipokuwepo na vielelezo. Hilo analifahamu, ila ni makusudi tu. Na wewe unashadadia shadadia bila kufanya tafakari! Ovyo kabisa.

Karibu 2020!
 
Acha kushadadia mambo usiyoyajua, huo ni umbea. Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo kwa nini wasipeleke maelezo yao kwa vyombo husika, ili taratibu za kisheria za upelelezi ufuatwe? Halafu Huyo Lissu ni mwanasheria, anafahamu kuwa ni kosa la kisheria kuhukumu jambo pasipokuwepo na vielelezo. Hilo analifahamu, ila ni makusudi tu. Na wewe unashadadia shadadia bila kufanya tafakari! Ovyo kabisa.

Karibu 2020!
Kuna vyombo vya usalama Tanzania ?
 
Dikteta mbowe alikuwa amelewa hili hata mtoto mdogo anafahamu, na waliomshambulia ni watu kutoka makundi hasimu ndani ya chademu yaliyosababishwa na udikteta wa ndugu mbowe
 
Back
Top Bottom