Tundu Lissu: Ni wakati wa kufungua ukurasa mpya kama Taifa

Lugodisha

Member
Aug 25, 2018
57
95
Uhuru na haki zipi mlizozikosa wakati wa JPM ambae alikuwa mtetezi wa wanyonge na watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao. Juhudi zake za utetezi wa haki za wanyonge kakomesha ufisadi, ujambazi, wizi, rushwa na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina. Naona haki zinazotofutwa hapa ni za kushibisha matumbo na wala sio kwa maendeleo jumuishi ya watanzania.
 

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,828
2,000
Uhuru na haki zipi mlizozikosa wakati wa JPM ambae alikuwa mtetezi wa wanyonge na watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao. Juhudi zake za utetezi wa haki za wanyonge kakomesha ufisadi, ujambazi, wizi, rushwa na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina. Naona haki zinazotofutwa hapa ni za kushibisha matumbo na wala sio kwa maendeleo jumuishi ya watanzania.
Unamuuliza nani?
 

toughlendon_1

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
2,984
2,000
Wajinga na wapumbavu wanafahamika kwa hoja wanazotoa. Toa sababu hata hafifu ya kuingia gharama kubwa kumweka dereva Nairobi na baadaye Ubeljiji hadi leo hii. Watu walisema kuwa Nairobi alikuwa anafundishwa ajibu nini polisi atakapolazimika kuhojiwa na angerudishwa TZ pale ambapo angeonekana ameiva. Hakuiva na sasa yuko Ubeljiji. Ni sababu gani utakayotoa ili yale maneno yasiaminiwe? Kumbuka pale Dodoma dereva alipohojiwa na waandishi wa habari alisema aliona gari inamfuata kwa nyuma na alipomwambia bosi wake yaani Lissu yeye alimwambia twende tu nyumbani. Ila cha kushangaza kule Ubeljiji alihojiwa na DW Tv akasema alipoona gari inawafuatilia kwa nyuma hakusema chochote kwa bosi wake. Akija TZ kitaeleweka tu na wa kuaibika wataaibika.
Aisee nchi ina watu mabogus hii, hakyamungu, yan umekaa kwene computer yako ukaamua kuandika maneno yote haya na all this is hearsay ? mzee mbona mnatukatisha tamaa, kila siku mbarudisha nyuma hili taifa.
 

Kohelethi

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,187
2,000
aisee nchi ina watu mabogus hii, hakyamungu, yan umekaa kwene computer yako ukaamua kuandika maneno yote haya na all this is hearsay ? mzee mbona mnatukatisha tamaa, kila siku mbarudisha nyuma hili taifa.
Mkuu acha kabisa. Yaani mtu anaandika ujinga Kama kachanganyikiwa. Anakwambia lile tukio la Lisu ni usanii kwa mabichwa mabovu Kama haya unaweza kuililia nchi hii kwa kweli. Ukweli wa Mungu inasikitisha kuona kwenye kizazi hiki bado kuna watu wa aina hii.
 

toughlendon_1

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
2,984
2,000
Mkuu acha kabisa. Yaani mtu anaandika ujinga Kama kachanganyikiwa. Anakwambia lile tukio la Lisu ni usanii kwa mabichwa mabovu Kama haya unaweza kuililia nchi hii kwa kweli. Ukweli wa Mungu inasikitisha kuona kwenye kizazi hiki bado kuna watu wa aina hii.

aisee kazi ipo
 

Meela

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,481
2,000
aisee nchi ina watu mabogus hii, hakyamungu, yan umekaa kwene computer yako ukaamua kuandika maneno yote haya na all this is hearsay ? mzee mbona mnatukatisha tamaa, kila siku mbarudisha nyuma hili taifa.

Yaani ni safi mno. Unakubali kuwa anayeandika maneno kutokana na hearsay no BOGUS. Katika hilo unadhihirisha wewe no bogus wa kutupa. Dereva hakuwa Nairobi?? Mbowe hakusema dereva anatibiwa kisaikologia kule Nairobi?? Na je dereva hakuhamishiwa Ubeljiji hadi leo? Na je Lissu alipofadhiliwa na mabeberu kuja kugombw=ea uraisd hakumwacha dereva Ubeljiji?? Hapo hearsay ni ipi? Na je kule Dodoma dereva alipohojiwa hakusema kwa waandishi wa habari kuwa alipoona anafuatiliwa nyuma alimweleza boss wake lakini akaambiwa waende tu nyumbani?? Hiyo nayo ni hearsay au hukufuatilia vyombo vya habari vilivyoripoti tukio la "kushambuliwa" lisu? Na kule Ubeljiji je dereva hakusema kwa DW tv kuwa alipoona watu wanawafuatilia hakumshirikisha boss wake? Hiyo nayo ni hearsay? Kwa nini abadilishe maneno kama sio elimu aliyofuata aseme nini? Nani ni bogus?
 

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
236
500
Baada ya msiba wa Mpendwa Wetu Daktari John Pombe Joseph Magufuli inaonekana sasa nchi inaelekea kwenye siasa za kistaarabu - yaani UKURASA MPYA UTAFUNGULIWA. WaTanzania hawatapotea au kupigwa risasi hovyo. mishahara itapanda na malimbikizo pomoni, wastaafu watalipwa kwa wakati, fao la kujitoa litarudi upya, sekta binafsi itapewa nguvu na haki yake, wamachinga hawatapewa tena vitambulisho vile watauza free, kodi za kubambika zitakoma, kutumbua tumbua na upendeleo wa vyeo hautakuwepo, taasisi nyingi ambazo bodi zake ziliachwa kuteuliwa sasa zitateuliwa na kutakuwa na ushindani katika kupata kazi za ujumbe wa bodi, n.k. Tunafungua ukurasa mpya na hata ban humu jukwaani zipapungua sana! Karibu ukurasa wa kwanza!
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,359
2,000
Wale waumini wa dini ya Kikristo, wanaijua ile sala kuu tunayoiita Sala ya Baba Yetu. Sala ile tunaiita ni sala kuu kwa sababu tulifundishwa na Kristo mwenyewe ambaye ndiye msingi Mkuu wa imani ya Kikristo.

Sala ile sehemu moja muhimu sana, tunasali, "utusamehe makosa yetu KAMA NA SISI TUNAVYOWASAMEHE WALIOTUKOSEA.

Natambua kuwa Tundu Lisu alifanyiwa unyama na ushetani wa hali ya juu. Alipigwa risasi 16, lakini kwa mapenzi ya Mungu, yupo hai. Sitaki kumtuhumu marehemu maana nikifanya hivyo, nami nitakuwa naingia kwenye mtego ule ule. Lakini sote tunajua tukio lile lilifanyika wakati wa utawala wa marehemu. Si Tundu Lisu pekee, bali wapo pia wengine waliopoteza maisha, waliopotezwa, waliotengenezewa mashtaka hewa, na wengine mpaka leo wapo ndani huku tuhuma dhidi yao zikikosa ushahidi. Sitaki niliongelee sana hili maana nia yangu kubwa, ni kuelezea umuhimu wa msamaha.

Yesu alipopigiliwa msalabani, alitamka, "Baba uwasamehe maana hawajui watendalo".

Papa John Paulo wa 2, alipopigwa risasi na Mehmet Ali Agca wa Uturuki, alipozinduka tu na kupata fahamu, alitamka, "kwanza namsamehe aliyetaka kuniua, nayaunganisha mateso yangu na mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo, nawapa pole wale waliojeruhiwa pamoja nami".

Hayati Rais Mandela, alipotoka gerezani na kisha kuwa Rais wa Afrika Kusini isiyo na ubaguzi, waafrika Kusini wengi wengi weusi waliamini kuwa chini ya Rais mweusi mwenzao, wazungu wangekoma, lakini Mandela aliwaambia, "kama ubaguzi haukuwa mzuri dhidi ya mtu mweusi, hauwezi kuwa mzuri dhidi ya mzungu"

Kuna nguvu kubwa nyuma ya msamaha. Kama tunataka kusamehewa, ni lazima tuwe na uwezo wa kusamehe, tena kwa msamaha wa moyoni, wala siyo kwa msamaha wa kinafiki.

Mtu anapofariki, amemaliza safari yake ya Duniani. Unaweza kumwona alikuwa mwovu sana, lakini hujui dakika yake ya mwisho alikuwa na uhusiano gani na Mungu. Mungubwetu ni Mungu wa msamaha.

Rais Mwinyi aliwahi kunena, "kama ukafanya makosa wakati dhamira yako ilikuwa njema, Mwenyezi Mungu huyatakatifuza yale makosa yako kwa sababu ya ile dhamira yako njema".

Marehemu ni nafsi ya kuonewa huruma. Marehemu asidhihakiwe. Marehemu asihukumiwe. Marehemu asipambwe. Mema ya marehemu yatufanye kuwa na shukrani kwa Mungu aliyetupatia hiyo nafsi na kisha akaichukua. Mabaya ya marehemu yatusaidie kupata msamaha wa Mungu maana ni kwa kusamehe, tunapata neema ya kusamehewa. Tena kwa wale ambao wanahisi walikosewa sana na marehemu, mara waliposikia juu ya kifo chake, neno lao katika nafsi zao lingekuwa, "Mungu wewe ni Mungu wa msamaha. Nilihuzunishwa sana maana marehemu aliiumiza nafsi yangu kwa .........., lakini dakika hii nanena kwa nafsi yangu kuwa namsamehe yote aliyonikosea, namwombea pia na pale alipopungukiwa katika maisha yake ya hapa Duniani kama mimi nisivyo mkamilifu. Naomba msamaha wangu huu, nami unipe haki ya kusamehewa mbele ya mahakama yako, siku yangu itakapofika.

Ombi Langu Kuu:
Maombi yangu kwa Mungu wetu, msiba huu wa John Magufuli uwe sababu ya upendo zaidi, mshikamano zaidi na umoja zaidi.

Waliompenda sana Magufuli wajiulize kama kauli zao wakati huu ni za kutuunganisha zaidi, kupendana zaidi na kushikamaa zaidi.

Waliomchukia Magufuli, wajiulize, kumchukia marehemu, nafsi iliyolala, isiyoweza kutujibu wala kujitetea, kuna faida gani kwa Taifa wakati huu. Je, hakuna jema ambalo tunaweza kumshukuru Mungu kwa kutuletea John Magufuli? Hekima ya Mungu siyo ya mwanadamu. Tumwombee marehemu, tuiombee familia yake.

Waliomkosoa marehemu, mlikosoa sera zake au mbinu zake, akiwa hai, akiwa kwenye nafasi yake kama kiongozi mkuu. Kukosoa siyo uadui, siyo chuki, na hakuna kiongozi atakayepatikana atakayekosa kukosolewa. Ni wakati wa kuonesha upendo utakaodhihirisha kuwa tulikosoa fikra na wala siyo chuki dhid ya mtu.

Namaliza kwa kurudia tena, Tundu Lisu, ifahamu nguvu ya msamaha. Ulipitia magumu mengi lakini ujue kuwa kila tendo Mungu huruhusu kwa sababu fulani. Huwezi kusema ulinusurika kifo kwa sababu ya werevu wako. Aliyekunusuru na kifo, huenda amekupa mtihani wa kuona kama una uwezo wa kusamehe kiasi gani, na kutaka kuona kama una uwezo kuuishi ukristo wako uliooneshwa na Kristo mwenyewe kwa kusema, "Baba wasamehe kwa kuwa hawajui watendalo".
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,629
2,000
Msamaha haulazimishwi

Akitaka anaweza kusamehe akitaka pia anaweza asisamehe yote ni hiari yake

Ila Kristo anafundisha kwa kusema, ..ndugu yako akija kwako akisema nisamehe hata mara sabini kwa siku wewe inakupasa umsamehe....

Kibaya zaidi msamaha kiimini unaunganishwa na maombi yako ya kila siku, kuwa usipowasamehe watu makosa yao hata wewe Baba wa Mbinguni hatokusamehe makosa yako.

Kupanga ni kuchagua ila ni vizuri kusamehe hata kama hujaombwa msamaha. Wanyiramba wanasema, forgiveness is pervasive

Amen
 

julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
951
1,000
sisi hatutasahau jins alivomtaabisha mgonjwa na kumtolea madua mabaya mabaya.hakika watanzania hatutamsahau aluchofanya dhidi ya shujaa wetu
 

mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
970
500
Damn i hate this guy......
Yaah I too hate Makapuku kama Tobo wanaojipendekeza kwa mabeberu1 Toboanafanya hivyo ili apate kamkate kake ka kila siku huko Ubelgiji, vinginevyo ataishia KUD#### mitaani kwani huko there is no FREE KUNCH. You have to "pay for everything".
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom