Tundu Lissu ni vema angewalaumu ACT-Wazalendo na akina Halima Mdee akiwa nchini lakini siyo Ubelgiji

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,747
141,613
Nilimsoma Tundu Lissu akiwalaumu akina Halima Mdee na wenzake kwa kukubali kuapishwa kuwa wabunge ilhali Uchaguzi haukuwa huru na haki.

Nimemsoma tena Tundu Lissu akiwalaumu ACT-Wazalendo na Maalimu Seif kwa kukubali kujiunga na serikali ya Umoja wa kitaifa na kwamba wamewasaliti wananchi.

Nionavyo mimi hoja za Lissu zingekuwa za msingi kama angeziongea akiwa kwenye mapambano hapa nyumbani lakini siyo aongelee akiwa Ubelgiji.

Yeye amekimbia lakini anataka wenzake wafanye yale ambayo yeye ameshindwa kuyafanya akakimbilia ubalozini.

Tundu Lissu aache ubinafsi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuwalaumu ni sahihi kabisa bila kujali aliko.Hivi mdee asingekuwa mbunge miaka mitano asingeishi? Vipi maalim seif kuwa makamu wa kwanza wa rais kunasaidia vipi kutekeleza Sera za act zaidi ya ugali?
 
Nilimsoma Tundu Lisu akiwalaumu akina Halima Mdee na wenzake kwa kukubali kuapishwa kuwa wabunge ilhali uchaguzi haukuwa huru na haki...
We jamaa mara useme Lissu amefilisika kisiasa mara Lissu hakuwa mgombea sahihi mara Lissu anatumiwa na mabeberu yani ni vurumai tupu cha ajabu sasa kila uchwao thread zako ni Lissu Lissu Lissu au kakuachia kibendi mzee?
 
We jamaa azikutoshi kichwani mara useme Lissu amefilisika kisiasa mara Lissu hakuwa mgombea sahihi mara Lissu anatumiwa na mabeberu yani ni vurumai tupu cha ajabu sasa kila uchwao thread zako ni Lissu Lissu Lissu au kakuachia kibendi mzee?
Hahahaaaa....... Mbona una kimuhe muhe manka!
 
Tundu lissu ndo mwenye akili kuliko chadema wote anachoongea mkuu wetu ndo sahihi nani kama tundu lissu
 
Nilimsoma Tundu Lisu akiwalaumu akina Halima Mdee na wenzake kwa kukubali kuapishwa kuwa wabunge ilhali uchaguzi haukuwa huru na haki....

Ukweli ni ukweli, uuongelee China, Ulaya, Amerika, Ivory Coast, itigi au hata Mwananyamala ni ukweli tu. Angesubiri aongelee huo ukweli hapa angeshapoteza uhai.
 
Mlikua na mpango wa kum Restisha In Peace, asingeweza kutoa lawama.
Alitunishiana misuli na polisi akisema nifanyeni lolote hata kunipiga risasi nipigeni!

Akarusha chopa bila kibari kutoka KIA to dar akisema haogopi chochote!

Alitaka kulala pale bagamoyo road akisema haogopi chochote.

Wafuasi wake mkasema Lissu anaulinzi usioonekana toka kwa beberus.


Huyu Lisu tukisema ni debe tupu hatukosei
 
Ukweli ni ukweli, uuongelee China, Ulaya, Amerika, Ivory Coast, itigi au hata Mwananyamala ni ukweli tu. Angesubiri aongelee huo ukweli hapa angeshapoteza uhai.
Huyu huyu alierusha hadi chopa bila kibari ndio amekimbia kisa kitisho cha kwenye simu?
 
Huyu huyu alierusha hadi chopa bila kibari ndio amekimbia kisa kitisho cha kwenye simu?

Angekuwa hajapigwa risasi, huu utetezi wako ungekuwa na nguvu. Lakini hadi sasa hata waliomshambulia kwa risasi hawajakamatwa.
 
We jamaa mara useme Lissu amefilisika kisiasa mara Lissu hakuwa mgombea sahihi mara Lissu anatumiwa na mabeberu yani ni vurumai tupu cha ajabu sasa kila uchwao thread zako ni Lissu Lissu Lissu au kakuachia kibendi mzee?
Teh teh teh.... Nimecheka kwa sauti nikakimbia nitoke nje kumbe nimesahau napitia pazia la dirishani nikidhani mlango hadi naandika hapa ni baada ya kufutwa damu.
 
Back
Top Bottom