Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ni mwarobaini wa Upinzani kumng'oa Magufuli

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Chadema kama cha Kikuu cha Upinzania Tanzania kimeiva na kiko tayari kuongoza nchi, Umma kwa asasa unakiamini, na hata wafanyamaamuzi kwa sasa wanakiamini chama hiki.

Kisiasa Chama cha siasa katika Uchsguzi hutembea katika madaraja makuu MATANO hadi kufikia kushika madaraka ya nchi (Kushika Dola), Chadema imevuka Daraja la NNE na sasa iko tayari kuingia Daraja la TANO ifikapo October 2020.

1. Daraja la kwanza huwa ni kuunda chama, Chadema imelivuka hili.

2. Daraja la pili huwa ni kupata wabunge angalau 10 hadi 50 hivi kwenye bunge la viti 264. Chdema imevuka hatua hii,

3. Daraja la Tatu huwa kuongeza idadi ya Wabunge ulionao, Chadema imevuka lengo hili tangu chama kianzishwe idadi ya wabunge huongezeka kila uchaguzi.

4. Daraja la nne huwa ni kulinda wabunge ulionao. Chadema imefaulu hili na Uchaguzi huu italinda status hii. Ni wajibu wa chama iki kiendelee kuwepo.

5. Na daraja KUU la TANO huwa ni Kushika Dola. Hapa ndipo tulipo sasa na tunawajibu wa kuchanga karata vizuri chama Kikabebe dola ama kukirejesha nyuma.

Siasa za Tanzania zimebadilika ghafla tangu Jumatatu na sasa nguvu na mvumo kamili wa kumuondoa Magufuli kwa njia halali za kikatiba na kisheria ifikapo October unajidhihirisha tangu Binadamu pekee mwenye miujiza kamili kurejea katika Ardhi ya kitovu chake imara, Si Mwingine nae ni Tundu Antipas Lissu.

Unaweza kujiuliza kwanini ni Tundu Lissu? Jibu linaweza kuwa moja na fupi, kwamba rekodi za Tundu Lissu tangu Magufuli awe Rais zimekuwa ni za kutukuka daima na hazina mfano. Ukianzia kumtazama kuanzia September 7, 2017 kurejea nyuma kabla hajashambuliwa kwa risasi, utajiridhisha kwamba Tanzania imebarikiwa kupata mtu sahihi wa kuwa Rais wa Nchi ambae ni Tundu Lissu.

Huyu ndie pekee mwenye uthubutu wa kumkabili Magufuli kwa maneno, na kwavitendo, angani, majini na aridhini. Huyu ndie anaweza kuwaambia chochote Watanzania na wakamsikiliza na kutenda. Huyu si yule aliyesema urais wa ghasia na maneno mengine meeengi kisha akatuacha Kisutu hadi leo.

Tunajitaji kuiondoa kwanza ccm madarakani, ndipo tujenge misingi yote imara ya Taifa iliyovunjwa na kuharibiwa, Tunahitaji mgombea mwenye kufanya counter-attack kali ukilinganisha na mshindani wetu. Hulka ya ccm na mgombea wao ni chama ambacho kinaamini Tanzania inaongozwa na Katiba na Sheria, huku wakiamini Ccm na mgombea wao ndio Katiba na Sheria zenyewe.

Sasa katika hali hiyo hamhitaji mgombea diplomatic, mtaumia huku mnaoana, Mnahitaji mgombea mwenye counter-attack mara mbili ya mshindani wenu. Dawa ya Moto ni Moto, sio Maji. Na kwa maoni yangu nikiwaangalia Wagongea Saba waliorejesha fomu, Tundu Lissu ni mwiba mkali kwa mpinzani wetu.

Ziko propaganda za ndani na nje kwamba Tume ya Uchaguzi haitamteu kuwa mgombea, kisa ana kesi ama kisa alivuliwa Ubunge na Ndugai kwa hila, Hizi ni propaganda zinazoenezwa na maadui zetu kisiasa ambazo Chadema tukizipokea kijinga tumeliwa.

Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 39 (d) na (e) vifungu hivyo vinasema wazi sifa za Mgombea Urais, Nanuku,

(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,

(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katikaMahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Kifungu (d) Katika Katiba ndicho kinachotumiwa na wanapropaganda sana, Swali ni Je, Mh Lissu anazo sifa za kuwa Mbunge? Jibu ni Ndio anazo sifa za kuwa Mbunge kwa kuwa mchakato uliotumika kumvua ubunge ni batili, uliamuliwa na Job Ndugai tu bila kushirikisha vyombo vya maamuzi vya kibunge na Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma. Hivyo kufuta uhalali wa maamuzi ya Ndugai.

Kifungu cha (e), Kwamba Lissu atazuiwa kugombea kisa anakesi Mahakamani, hii ni propaganda hii ni nyepesi, Lissu ana kesi 6 mahakama ya Kisutu na kesi zote hazijafikia mwisho, hazijatolewa hukumu, na hazihusiani na Ukwepaji kodi, bali ni za jinai yaani za uchochezi ambazo haziko kwenye vifungu vya katiba vinavyomzuia mtu kugombea urais.

Akitangaza uamuzi wa Kugombea Urais Mh Lissu alizungumza mengi juu ya Uchumi, Utawala wa Sheria, Bunge, Haki ya Kuishi, Uhuru wa Kutoa maoni na mengine mengi.

Na vile vile alizungumza na kufafanua juu ya proaganda kwamba atakatwa jina lake.

Nanukuu:

"Ninafahamu kwamba baadhi yenu mna hofu kubwa na ya halali kabisa juu ya mimi kuwa na sifa za kikatiba na kisheria za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano. Hii ni kufuatia uamuzi wa Spika Ndugai wa kunifutia Ubunge mwezi Juni ya mwaka jana. Nitalitolea suala hili ufafanuzi wa kina wa kikatiba na kisheria endapo utahitajika. Itoshe tu kusema kwamba mtu anayekosa sifa za kugombea Urais (au Ubunge) kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni yule tu ambaye amepatikana na hatia ya kukiuka Sheria hiyo na chombo pekee kilichoanzishwa kwa mujibu wa Sheria hiyo, yaani Baraza la Maadili.

Katika utumishi wangu wote kama kiongozi wa umma, mimi sijawahi kutuhumiwa, kushtakiwa, kuitwa kwenye shauri, kutolewa ushahidi wowote dhidi au kwa niaba yangu, na kuhukumiwa na Baraza hilo la Maadili kwa kosa lolote lile chini ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Aidha, sijawahi kutuhumiwa, kushtakiwa, kuitwa kwenye kesi, kutolewa ushahidi dhidi ya au kwa niaba yangu, kuhukumiwa na kuadhibiwa kwa kosa lolote linaloweza kunifutia sifa za kugombea nafasi yoyote ile ya uchaguzi wa umma kwa mujibu wa Katiba na sheria zetu za Uchaguzi.

Spika Ndugai ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, licha ya dhamana hiyo kubwa ya uongozi aliyonayo kitaifa, yeye sio Baraza la Maadili, na wala sio Mwenyekiti au mjumbe wake. Kwa sababu hiyo, uamuzi wa Spika Ndugai wa kunifutia ubunge haujaniondolea sifa za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au nafasi nyingine yoyote ya uongozi.

Kwa hiyo, wananchi wenzangu, nawaombeni wote mniunge mkono katika safari hii ngumu iliyopo mbele yetu" Mwisho wa Kunukuu.

Nje ya hayo, tunahitaji usalama wa Tundu Lissu, Usalama huu unatakiwa kutazamwa kuanzia Geneva Uswis hadi Ikungi Singida Mashariki. Kwamjibu wa sheria za Tanzania mgombea Urais hulindwa na vyombo vya dola, Usalama wa Lissu utakuwa na nguvu kama atatazamwa kama mgombea urais na si Lissu tu. Tangu alipotangaza kwamba atagombea urais, Dunia inamtazama Lissu kama mgombea Urais sio Lissu yule aliyeshambuliwa kwa risasi, hivyo thamani ya Ulinzi wake kidunia inatazamwa kama Mgombea Urais. Na hata Rais Magufuli kama mkuu wa Nchi kiitifaki hata mtazama kama Lissu, bali mgombea Urais, na hata CCM hawatamtazama kama Lissu bali mgombea urais. Ulinzi wake utakuwa na jicho la dunia zaidi kuliko kama Lissu.

Tundu Lissu ni mwarobaini wa Upinzani kumg'o Magufuli.

Na Yericko Nyerere

IMG_20200731_221830_411.jpg

Screenshot_20200731-210209.png
 

Attachments

  • IMG-20200731-WA0015.jpg
    IMG-20200731-WA0015.jpg
    43.8 KB · Views: 1
Kama Chadema imeshindwa kulinda nafasi za wabunge wake( waliokihama chama hicho), unapata wapi ujasiri wa kusema Chadema imevuka ngazi nne kuelekea kuaminiwa na wananchi? Serikali za mitaa huna utawezaje kushika serikali kuu?

Kwa nini mnataka kuwapotezea muda wanachama wengi wa chama hicho wanaotafakari kama wanazo sababu za msingi kuendelea na Chadema wakati wanaona Chadema imeshindwa kusimamia misingi ya kuanzishwa kwake!?
===
Umebeep nimetuma sms. Ha ha haa ! Tuendelee na mjadala mleta mada.
 
Nimefuatilia maelezo yako sijaona uliposema kwa nini tundulissu anafaa na atafanya nini tofauti na magufuli.

Zaidi umeishia kumsifia tu na kumponda magufuli na ndugai.

Kwa mtaji huu mnaenda kuchezea pesa za walipa kodi tu.

Pili naona umeikanyaga demokrasia kwa kuanza kumnadi tundu lissu kabla hata ya mchakato wa kidemokrasia wa kamati kuu. Hapa inaonyesha ni jinsi gani demokrasia ilivyokuwa ngumu kuitekeleza kuliko kuitajataja.

Hao ndio think tank ya chadema.
 
Kama Chadema imeshindwa kulinda nafasi za wabunge wake( waliokihama chama hicho), unapata wapi ujasiri wa kusema Chadema imevuka ngazi nne kuelekea kuaminiwa na wananchi? Serikali za mitaa huna utawezaje kushika serikali kuu?

Kwa nini mnataka kuwapotezea muda wanachama wengi wa chama hicho wanaotafakari kama wanazo sababu za msingi kuendelea na Chadema wakati wanaona Chadema imeshindwa kusimamia misingi ya kuanzishwa kwake!?
===
Umebeep nimetuma sms. Ha ha haa ! Tuendelee na mjadala mleta mada.
Nani aliekudanganya kuwa mwanachama wa chama cha siasa ni sawa na kuhukumiwa kifungo gerezani, kwamba hakuna kutoka mpaka utakapomaliza hukumu yako?

Anyway, sijui kama utakuwa umeelewa mantiki ya swali langu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom