Tundu Lissu ni muongo au ana alzheimer's?

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
MH TUNDU NI MUONGO AU ANA ALZHEIMER'S?

Na Elius Ndabila

Alzheimer's ni moja ya visababishi au dalili ya mtu kuwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu *(DEMENSHIA)*. Kwa kawaida ugonjwa wa DEMENSHIA kisayansi huwapata zaidi watu wenye umri wa kuanzia miaka 65, ijapo hata chini ya umri huo mtu anaweza kuwa nao. Ugonjwa huu hautibiki, ila dalili zake yaani *ALZHEIMER'S* hutibika.

Nilishawahi kuandika kuwa kwa namna Tundu alivyokuwa amejuruhiwa na Mungu kumunusuru kuwa hai hadi sasa alipaswa apate muda zaidi wa kupumzika kutibu afya yake kikamilifu kuliko kugombea Urais. Nilisema afya ya Tundu ni muhimu kuliko nafasi ya Urais anayoitafuta ilihali anajua na chama chake kinajua kuwa hawezi kupata.

Kuonyesha kuwa afya ya Mh Tundu haijatengamaa akiwa Katavi aliudanganya umma kuwa Katavi walidanganya kuwa kutakuwa na safari ya treni ya Dar -katavi. Akasema CCM waliwadanga hii haiwezekani. Alisema treni haiwezi kuja Katavi kwa kuwa hata reli haijakarabatiwa.

Wakati Tundu akisema hivyo, ukweli wa mambo ni kuwa Katavi kuna safari ya treni ambayo husafiri zaidi ya mara tatu.
Maneno ya Tundu kuwa hakuna safari ya treni Katavi yaliendelea ku-cement hoja yangu kuwa Tundu anatakiwa kupata muda mrefu wa mapumziko kuliko kuhangaika na Urais.

Wakati Watanzania hatujasahau kauli yake ya Katavi, jana akiwa Bunda amesema kuwa Mgombea wa CCM ambaye pia ni Rais wa JMT amewaita Wakurugenzi wa halmashauri nchi nzima kwenda Dodoma. Nilisikitika kusikia kauli hiyo kwa kuwa wakati anasema kauli hiyo mimi nilikuwa mahali nimekaa na Mkurugenzi wa halmashauri moja hapa nchini. Huu nao ulikuwa mwendelezo wa uongo na leo Wizara ya TAMISEM imejibu na CCM imejibu kupitia kwa msemaji wake Humprey Polepole. Maneno haya kutoka kinywani kwa Tundu mimi yananishangaza kwa kuwa tangu nianze kufuatilia siasa za Tundu nilikuwa ninajua ni mtu wa facts, sikuwahi kufikiria kuwa naye ni muongo. Mpaka sasa ninaandika sijui kama Tundu ni *Muongo au ALZHEIMER'S*? Ninaamini wasomaji mtanipa jibu sahihi kuwa Tundu ni Muongo au ana ALZHEIMER'S?

Binafsi ninaendelea kushauri kuwa Tundu anahitaji kuendelea kupata matibabu, kwani mikiki mikiki hii ya Kampeni inaweza kumfanya kupata matatizo ikiwepo tatizo la kupoteza kumbukumbu() na kumfanya kuwa mropokaji kwa kuwa anakuwa hakumbuki.

Afya yake ni mhimu kuliko nafasi anayoitafuta ambayo hata hivyo hawezi kuipata. Kuendelea na hili tatizo linaweza kumfanya kuwa sugu na ikawa shida kulitibu
 
Tarime hiyo mwaka 1984.
tapatalk_1601219974794.jpeg
 
Mgombea wa CCM ambae kwa sasa hivi anahaha kwa hali na mali kutafuta kura za maruhani baada ya kukataliwa hadi na wanachama wa CCM aliwahi kusema haya:

1.Vitambulisho ya wajasiriamali ni hiari wakati alivitungia sheria

2.Lissu alipata ajali akapata huduma ya kwanza kwenye hospital za hapa nchini wakati yeye ndiye aliempiga risasi na wala haikuwa ajali


Kwa ule umri wake nafikiri atakuwa ana ALZHEIMER'S sugu
 
Weee kajinga kweli, kwaiyo baada ya Polepole kuitaka tamisemi kujibu hoja

Ndo umeona kuja utopolo wako ,ukidhan ndo utatuondoa kwenye mstari wa ukweli.

Wee ni tope tu kama walivyo wana CCM wenzako.

Ukweli nikua Wakurugenzi wako Na Jiwe.
 
#TeamJPMOut.

Hata mseme vipi, kura yangu ni against mropokaji, mjivuni, mjuaji, anayejiona yuko juu ya waTanzania wote.

Nitachagua humble person aliye tayari kumsikiliza na kutatua shida za wananchi bila kejeli.

Mtu anajisifia kujenga mabarabara tena kwa mkopo.

#JPMOut28/10
 
Hahahaha Tundu ajenda yake ni ile aliyotumwa na mabeberu nayo ni kuleta vurugu nchini.


Ukisiliza video ya mzungu aitwaye Amsterdam ndipo utaelewa ajenda ya Lissu...Halafu huyu Lissu binafsi sikufahamu awali kuwa mambo kadhaa hayajui maana yake.


Hata neo-colonialism hajui maana yake ni Nini..


Maelezo yake kwenye press conference kuhusu , among other issues, neo colonialism yalikuwa ya kiwango Cha chini kabisa..
Hajui how imperialism and neo colonialism operate...hovyo kabisa..


Anawakumbatia mabeberu asijue madhara yake...halafu anarudia rudia mambo ya the so called The Hague huku yeye mwenyewe akihamasisha ghasia na hivyo kumfanya yeye mwenyewe awe mtuhumiwa wa The Hague...
 
Kwa kuwa Lissu ni mgonjwa wa kupoteza kumbukumbu, hiyo ni fursa adhimu na adimu ya kupokea mwaliko wake wa mdahalo na rais wetu wa wanyonge Dkt. Magufuli, jembe la kuhifadhi kumbukumbu na data kichwani...hadi zinazohusu idadi ya samaki baharini, maziwani, mitoni na mabwawa yooote ya Tanzania. Tena anajua sio kwa makisio (makadirio), ni kwa namba halisi haswa, anataja mpaka mamia yake, makumi yake na mamoja yake.

Duniani kote hutaweza sikia mtu anaejua idadi ya samaki kwa namba yake halisi hata ktk ziwa moja tu. Huo ni uwezo pekee wa Dkt. Magufuli, jumlisha na kipawa chake cha kujua marais wa nchi mbalimbali ikiwemo wale aliowataja kuwa walikuwa wa Kuwait sijui na mwingine alisema wa wapi vile (mie nimepoteza kumbukumbu ya aliowataja na nchi alizowanasibisha nazo)
 
Walioko na wanaogombea CCM ni wasaka tonge tu wala hawana uchungu na WANANCHI na ndio maana wametuletea Sheria za ajabu sana za MAFAO wakati wenyewe washachukua chao ni UBINAFSI WA HALI YA JUU SANA. WOTE MBWA TUU.
 
Yule wa kwenu Alisema yeye Ni kichaa, anacrustration,

Kuna siku alisema maendeleo hayana chama kesho yake akasema hakupeleka maendeleo jimboni kwa kuwa walichagua wapinzani
 
Back
Top Bottom