Tundu Lissu ni jasiri sijapata kuona

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
284
910
Japokuwa sikubaliani na Tundu kwa vitu vingi lakini kitendo cha kushambuliwa kwake kilinisononesha sana

Shambulio lake halikuwa la kibinadamu- ulikuwa ni unyama tena unyama uliopitiliza.

Ingawa_pamoja na madhira yote hayo. Tundu ameendelea kuwa jasiri-haonyeshi hali ya kukata tamaa, majonzi wala masononeko. Sura yake imejawa na tabasamu muda wote. Hadi najiuliza:

Waliomshambulia

Wanajisikiaje kumwona akiwa ni mwenye kujawa na uso wa furaha?
Wanajisikiaje kumwona akiwa hai?
Waliwaza nini juu ya familia yake ambayo angeiacha?
Ungekuwa wewe ungejisikiaje endapo ni ndugu yako anapigwa risasi zote zile?
Wanajisikiaje kumwona akiwa anatembea kwa kuchechemea mguu mmoja huku wao wakitembea kwa miguu miwili?

Ndugu Watanzania wenzangu, tujitahidi kutenda kadri ya inavyompendeza Mungu ipo siku tutahukumiwa sawa sawa na matendo yetu.
images.jpeg
 
MUNGU NI MWEMA SANA! ........

Mungu anamakusudi makubwa sana na Tundu Lissu......

Mungu wa Tz aliyemponya Lissu ndiye aliyeliponya taifa na Corona ila kuna watu fulani washamba na malimbukeni wao wanataka kujifanya ndio wameondoa Corona. Mungu aliyemfanya Lissu hai ndio huyo huyo amemponya jiwe na corona ili ashuhudie matendo makuu kupitia Lissu...

TUNDU LISSSU NI NEEMA YA TAIFA ......OCTOBER 28 TUIONDOE LAANA MADARAKANI NCHI IPONYWE
 
Anafaa kuwa amiri Jeshi Mkuu,anastahili kuwa Mkuu wa Nchi.
Ni Shupavu,Ni Jasiri ,anajiamini,amepita kwenye tanuru la Moto.
Ana sifa za Kielimu,Ufahamu,anajua kujieleza ,kusikiliza na Ana huruma.
Ni mkweli na mzalendo halisi.
Kwa kuaenzi hayo wote kwa pamoja bila kujali itikadi zetu,vyama vyetu,Dini zetu tumchague kwa kura za Ndio.
 
Anafaa kuwa amiri Jeshi Mkuu,anastahili kuwa Mkuu wa Nchi.
Ni Shupavu,Ni Jasiri ,anajiamini,amepita kwenye tanuru la Moto.
Ana sifa za Kielimu,Ufahamu,anajua kujieleza ,kusikiliza na Ana huruma.
Ni mkweli na mzalendo halisi.
Kwa kuaenzi hayo wote kwa pamoja bila kujali itikadi zetu,vyama vyetu,Dini zetu tumchague kwa kura za Ndio.
safi sana !
 
Back
Top Bottom