Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Mkuu Paskali, hata Tundu mwenyewe anajua kuwa ni mzuri sana kwenye nafasi ya kuongea hovyo na kukosoa lakini si utekelezaji. TLS sasa imeshamshinda,hakuna linalofanyika kwa manufaa ya wanasheria.
Jamaniii hizi ndizo ndoto yaan mtu kachaguliwa majuzi na toka hapo hatjaskia lalamiko lolote toka kwa anaowaongoza lkn tushaanza kusema haja Fanya chochote. Hivi aliyekuwa rais b4 yy alifanya nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lisu asingemnunua wema sepetu hata ubunge angepetwa asubuhi tu na madam wema, hivi utimamu wa akili unautoa wapi kushauri Lisu agombee urais? Au ulimaanisha wa TLS?
 
Saharavoice,
Mkuu habari za Geita , unachotakiwa kutambua ni kwamba URAIS WA MAGUFULI NI MIAKA MITANO TU , AKIBAHATIKA NI MIAKA KUMI , baada ya hapo atakuwa raia wa kawaida tu .

Suala la kusigina katiba ya nchi halijawahi kukubalika hata na mwehu .

Mwalimu Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema hivi , " HATA KAMA TUTACHAGUA ASIYEAMINI MUNGU , TUTATAFUTA NAMNA YA KUMWAPISHA ( maana wakristo wanaapa kwa kushika biblia na waislam wanaapa kwa kushika qoran ) , NA NI LAZIMA AAPE KWAMBA ATAILINDA NA KUITETEA KATIBA YA TANZANIA " Mwisho wa kunukuu .

Nimekuwekea hii ili ufahamu kosa analotenda Magufuli kwa kuchezea katiba ya nchi ambayo ndani yake imeruhusu vyama vingi .
 
Naona kuropoka ropoka ndo kwingi hapa, kwani sifa za mtu kuwa rais kwa nchi kama hii ni zipi, labda tuanzie hapo.

Make kwa uzoefu wangu, sioni kama wapigakura wa nchi hii wana vigezo vyovyote wanavyotumia ktk kumchagua rais ila naona wengi wanafuata mkumbo tu.

Tukiangalia waliotutawala hadi leo, sioni mwenye "Unic Qualities" kando ya Nyerere, ambazo naweza kusema watu walivitumia kama vigezo vya kumchagua, sioni, to be candid.!

Tumeona majuzi kwenye uchaguzi nchini France ambapo mgombea wa chama kisichofahamika Bw. Emmanuel Macron, alishinda urais, bcoz pasipo kujali uchanga wa chama chake lkn bado wapigakura waliweza kumpatia kura nyingi, aidha kwa sababu ya qualities zake au bcoz of what he stood for.

Kwa bahati mbaya hapa kwetu hilo halipo, mtu atachaguliwa tu kisa anatoka labda ccm, hata kama hana ile hulka ya uongozi! Kwa mantiki hiyo, nina-sum up kwa kusema kwamba, kwa Tanzania mtu yeyote anaweza kugombea urais na akapata kwani hakuna cha kuzingatia vigezo. Hata huyo Tundu Lisu, anaweza tena vizuri tu, (Since he is not worse and neither the incumbent nor his predecessors are any better).
 
Nawakumbuka wale wa ulipo tupo, naona kila dalili za mzee kukatwa tena!

Huku hamna kukatwa maana jina huwa moja tu analopendekeza Mbowe. Kwahiyo wale wa ulipo tupo sasa watasema ulipo hatupo na watamwambia kwanza ulikuja huku baada ya kukatwa. sasa sijui itakuwaje maana ameishatangaza kugombea 2020.
 
Jamani tusipoteze muda tuweke vikatio vyetu kwaajili ya 2020
hahahahahahahaha
 
Hahahahaha,asimame tu,yaani CCM inashinda bila jasho.Huyo Lissu hana personality ya kumfanya awe Rais.
Kumbe urais ni personality? he makubwa. Yule mzee wa msoga na personality yake ametufanyia nini cha zaidi?
 
Kumbe urais ni personality? he makubwa. Yule mzee wa msoga na personality yake ametufanyia nini cha zaidi?

Na ushauri wowote kwa mkuu wa nchi na mtu yoyote hautolewi kwa abusive language, lugha za namna hiyo huonyesha ni jinsi gani mtu anayetoa mtoa lugha alivyo. Na mara zote ulimi ndio unao mponza kichwa
 
Tundu Ana faa sana.ila asubiri kwanza.tatizo la kupita nafsi ya juu mapema itakuja mpa shida mbeleni ambako anahitajika zaidi.mf.ni Kabila na hata mzee sumaye.he can do simply as NASA did to raila.raila is the oldest candidate among the nasa.!!so he was given a last chance on the bases to age and energy.!!!wengene bado wana nafasi ya kujaribu tena.jack Chirac rais wa zamani aligombea Mara 4 na ya tank akashinda.vile vile amekuwa mayor wa Paris kwa miaka kumi na tano.

Anahitajika candidate mzuri kushinda hata bila ya katiba mpya.
 
Pascal una akili sana. Mtu anayeweza kusimama na Magufuli kwa sasa ni Tundu Lisu.Magufuli kabadili upepo wa siasa nchini hatari.2020 wapinzani lazima pamoja na mambo mengine watafute mgombea anayelijua vizuri jukwaa....Magufuli sasa hivi ni moto wa kuotea mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Erythrocyte,

Salute Mkuu,

Katiba hiyo hiyo imempa Rais Madaraka makubwa sana. Kumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kulisema hili siku za nyuma pia na alikuwa ana refer katiba hii tunayoitumia.

Sipingi kukosoa, napinga ukosoaji wenye kejeli, dharau na matusi. ukimkejeli Raisi, ukimdharau au hata kumtusi ni sawa na kuwatusi, kuwadharau na kuwakejeli watanzania waliomchagua.

Narudia tena Tundu Lisu will cost Chadema kama alivyowa cost watanzania wengi kipindi cha bunge maalumu la Katiba. 2020 siyo mbali sana.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Back
Top Bottom