Tundu Lissu ndani ya Songwe leo ni fungakazi. Wananchi wampokea kwa mapokezi mazito

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
Hakika upinzani upo miyoni mwa wananchi. Muache Magufuli aminye demokrasia, afungie vyombo vya habari, lakini mbegu iliyopandwa na wataka demokrasia nchini kuanzia enzi za akina james mapalala, Komu, Mzee Fundikira, James Mbatia, Maalim seif,Mwalimu Nyerere na wote waliopambana hadi kurudisha mfumo wa vyama vingi haiwezi tena kuzimwa na matendo ya mtu mmoja anayetaka yeye kutawala kama mfalme.

Mapokezi ya Lissu huko Songwe leo ni message kali kwa rais Magufuli kuwa wananchi wanaupenda upinzani, wanauheshimu na wanataka maendeleo na uhuru, maendeleo na demokrasia.

Hebu cheki wananchi wa Songwe walivyompokea Lissu leo

 
Ukweli mchungu kwa wana CCM.

Ukiangalia tangu uanze mchakato huu wa Uchaguzi mgombea aliyepata Mileage ya kutosha na kukubalika mpaka sasa kwa zaidi ya 100% ni Tundu Lissu.

Lissu amefanikiwa kuteka hisia,akili na mioyo wa Watanzania si kwa sababu pekee eti aliwahi kupigwa risasi bali ni kutokana na hoja zake.Anajua kujieleza na kulisimamia jambo kwa ukamilifu mkubwa na ni mtu pekee kwa sasa nchi hii amevuka viwango vya uoga na kuuvaa ujasiri ambao pengine hakuna raia yeyote nchi hii anao au aliwahi kua nao.

Anazungumza ukweli pasipo kumung'unya maneno pasipo kuzusha ,bado najiuliza je, kama vyombo vya habari vingeruhusiwa kutangaza habari kwa uwazi ingelikua ni balaa tupu.Navisihi sana vyombo vya habari viache uoga kwani vinapoteza sana mapato kwa kutoripoti habari za Lissu maana kwa sasa asilimia kubwa watu tunahitaji kujua chochote Lissu anachosema lakini kutokuandika habari hizo basi wanajikomoa wenyewe.

Wana CCM kumbukeni ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka hivyo kaeni mkao wa kula chama kupasuka,,,mlilea na kuyaficha maradhi subiri kifo.

Video hii chini Mh Tundu Lissu akiwa Momba.

 
Tatizo membe alijiaminisha kuwa anapendwa sana sana. Naona kapima upepo hizi week 2 kaona mambo hayapo vile alivyofikiri yeye. Kugombea urais kunahitaji haiba flani ambayo Membe hana. CCM hawakuwa wajinga kumuweka JPM 2015.
Watu huchagizwa kwa mengi. Watu wanaweza kumpenda mtu kwa haiba yake lakini pia wanaweza kusukumwa na mihemko fulani!
 
Tatizo membe alijiaminisha kuwa anapendwa sana sana. Naona kapima upepo hizi week 2 kaona mambo hayapo vile alivyofikiri yeye. Kugombea urais kunahitaji haiba flani ambayo Membe hana. CCM hawakuwa wajinga kumuweka JPM 2015.

Mbona Magufuli hana haiba lakini amekuwa rais?
 
Back
Top Bottom