johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,853
- 141,784
Umemsahau Mbowe!Nimefanya tathimini yangu kwa muda sasa na nimeona kuwa Tundu Lissu na Zitto Kabwe ndio wanasiasa wawili wanaojituma sana kuikabili hii serikali Bungeni,nje ya Bunge na kupitia mitandao kuliko wanasiasa wengine wote wa upinzani hasa katika kupambana na kufanya siasa nje ya Bunge.
Wanasiasa wengi wa upnzani hujituma zaidi ndani ya Bunge katika kuikosoa na kuishauri serikali na Bunge likiishi basi huwasikii tena na hata mitandaoni sio active kama walivyo Zitto na Lissu na hili ni tatizo ambalo wapnzani inawezekana hawalioni.
Ni Zitto na Lissu ndio ambao mara kwa mara wataandika makala ndefu mitandaoni wakati wanasiasa wenzao huishia tu kuandika tweets fupi fupi(baadhi ni wavivu hata kutumia mitandao) lakini sio kuandika makala ndefu na zenye uchambuzi wa kina za ama kukosoa au kushauri hii serikali.
Yaani Lissu alie mgonjwa na aliyoko nje ya nchi ndio wakati mwingine hutumia muda wake kuandika makala mbalimbali mitandaoni ila hawa wazima wa humu nchini wao wakijitahidi sana ni kuandika tweets fupi fupi tu basi!!
Na ukiacha Lissu ambae ni amekuwa mgonjwa,Zitto kwa sasa ndio naweza kusema ni mwanasiasa wa upinzani anaejituma sana kutumia mitandao kuikosoa hii serikali na hii ni moja ya sababu ya Zitto kwa sasa kuonekana ni mwiba kwa hii serikali kama alivyo Lissu.
MfanO,hivi sasa hata ukiingia katika account yake ya twitte, utakuta teyari ameshafanya uchambuzi(kama alivyowahi kufanya kupitia hapa JF) na kuonyesha mapungufu ya makubaliano baina ya serikali na Barrick, jambo ambalo hata wanasiasa wengine wa upinzani wanapaswa kulifanya ili kukabiliana na propaganda za sasa kuwaaminisha watanzani kuwa makubaliano yaliyofikiwa ni ushinda kwa JPM na Taifa kumbe ndani yake kumejaa mapungufu kibao tena ya kusikitisha.
Naelewa wanasiasa wengine wa upinzani watahoji na kukosoa makubaliano haya kati ya serikali na kampuni ya Barrick lakini wengi watafanya hivyo zaidi ndani ya Bunge na Bunge likiisha ndio basi huwasikii tena japo kuna wachache nao hupenda ku-tweets mara moja moja ila sio kuandika makala ndefu mitandaoni mfano facebook,Instagram na hata hapa JF.
Kwakweli Zitto na Tundu Lissu wanajituma sana katika kutumia mitandao kukosoa na kushauri serikali kama wanavyofanya ndani ya Bunge na kwa hakika kwa sasa wanasiasa hawa wawili ndio wanabeba upinzani nje ya Bunge na CCM kwa kulijua hili, ndio maana wameanzisha propaganda za kutaka kuwavuruga/kuwachonganisha na zaidi kutaka Zitto asiaminike na upinzani kwa ujumla kwa kutuletea habari za zilipendwa kuhusu Zitto.
Hongereni sana Zitto na Lissu mnafanya kazi kubwa sana kubebea upinzani na kuwafanya watanzani waelewe ni nin kinaendelea awamu hii ambacho pengine bila nyinyi na wapinzani wenzenu tusingeyajua, mfano kukamatwa kwa ndege yetu huko Canada wakati ule,utata kuhusu matumizi ya shlingi trilioni 1.5 na mengine mengi.
Bahati mbaya sana, upinzani kwa sasa mnapata support ndogo sana ya media na isingekua mitandao ya kijamii,basi mengi tusingeyajua au tungeyajua juu juu tu.