Tundu Lissu na Wakuu Wapya wa Wilaya

Lissu mwanasheria,

Nae analalamika wakati anazijua sheria, kwa nini basi asiwaburuze mahakamani wahusika? au ushahidi hautoshelezi?

Mfano suala la Milion 5, hadi zinaingizwa kwenye account au kupewa cash ilitakiwa wakamatishwe na technologia iliyopo

sasa kwa nini wasirekodi mahojiano ili wafikishwe mahakamani?

Huu ndio udhaifu wa hawa wanaojiita wapinzani, kazi kulalamika tu hata kama wana uwezo wa kitaaluma.

Shame!

Shame on you!!!!!!!!!!

Ni kawaida mbuni kuficha kichwa wakati kiwili wili chote kinaonekana. Hiyo ndiyo tabia na hulka ya magamba; kwa sasa mkakati wao ni kutumia mahakama ambayo inachakachua sheria kwa manufaa yao ili wacheleweshe au kubaka haki.

Wenye akili wanalijua hilo na wanazijua mahakama zinazotoa haki nazo ni wananchi wapiga kura. Ndicho anakifanya Tundu Lisu na sisi wananchi watoa hukumu tunafarijika na taarifa hizi na tutazitolea hukumu.

Mziki na mkakati wa M4C unaojibu upuuzi wako unaleta kizaa kwa magamba na kutekelezwa kikamilifu na wananchi.

HAPO HUKUMU YA WANANCHI IMECHUKUA MKONDO WAKE
 
Mkuu wangu angalia fact!

Kama lissu nae analalamika, basi itakuwaje kwa watanzania wa kawaida ambao hata sheria hatuzijui?

Mimi mtanzania si lalamiki na taarifa ya TL inanihusu mimi si wewe gamba. Mlalamikaji #1 kwa niaba ya chama cha magamba ni vuvuzela linaitwa Nepi ambaye akionekana tu kwenye vyombo vya habari inabidi uondoke maana harufu atakayoimwaga ni mbaya na chafu.
 
namkaribisha HASSAN MASALA kilombero, ila anapaswa kuwa mpole la sivyo tunaweza kumlambisha udongo.
 
Lissu mwanasheria,

Nae analalamika wakati anazijua sheria, kwa nini basi asiwaburuze mahakamani wahusika? au ushahidi hautoshelezi?

Mfano suala la Milion 5, hadi zinaingizwa kwenye account au kupewa cash ilitakiwa wakamatishwe na technologia iliyopo

sasa kwa nini wasirekodi mahojiano ili wafikishwe mahakamani?

Huu ndio udhaifu wa hawa wanaojiita wapinzani, kazi kulalamika tu hata kama wana uwezo wa kitaaluma.

Shame!
Sasa wewe Gamba zee, hivi Mkwerrrreee aliposema hawajui watu wa Richmond na wala hajawahi kukutana nao ulimuelewa? Yaani yeye pamoja na vyombo vyote vya dola na intelijensia uchwara anasema hawajui watu waliowahujumu Watz, na kwa maana nyingine hana hata mpango wa kuwafuatilia ili wajulikane wafikishwe mbele ya sheria. Pia, Uingereza imerudisha chenji ya Rada, na kuwataja baadhi ya WanaMagamba kuhusika ktk wizi huo lakini Mkwerrrreeee anapiga porojo tu kama wewe unavyofanya. Tatu, watu waliowacharanga mapanga Wabunge wawili wa CDM kule Mza walitajwa na PoliCCM wanawajua ila wanasubiri kupelekewa ushahidi badala ya kutafuta ushahidi na kuwashikilia wahusika waliotuhumiwa. Mpaka leo ni story tu! Nne, Mawaziri wa Magamba wametajwa kuhusika katika ubadhirifu na wengine kuelezwa mchana kweupe kuwa wanamiliki majumba ya zaidi ya Tshs. 1 Billion. Kilichofanyika ni kuwapa likizo ya kwenda kutumbua walichovuna. Tano, ishu ya Jairo na kuchangisha fedha za kupitisha bajeti, ni mwaka sasa unakaribia kupita lakini kama ilivyo ada naye kapewa likizo ya kwenda kula bata huku uchunguzi dhidi yake haujulikani uliko! Achilia mbali EPA, Meremeta, Tangold, Richmonduli, Dowans, Blandina Nyoni na tenda za wizi pale Wizara ya Afya, n.k.

Sasa ulitaka Lissu, asiye na dola wala intelijensia kama mnavyoiita wenyewe afanyeje? Hivi ni jukumu la Lissu kuwakamata wala rushwa? Hata akienda kuwashtaki, Magamba wako tayari kutafuna ngozi yao wenyewe? Mbona yule mzee kalishwa sumu, pamoja na Waziri wenu mmoja kupiga kelele hadharani bado Magamba yameziba masikio? Sasa kama Waziri katendewa vile na Magamba yanachekelea, sembuse Lissu?

Kweli wewe unafikiria Kimasaburi. Mpuuuuzi na mshenzi sana wewe, usije ukaleta ujinga wako hapa kwa Great Thinkers. Hizi si enzi za ujima na ujinga mliotupandikiza miaka ile. Magamba oyeee???? Anayejiona ni msafi kwenye Chama cha Magamba na awe wa kwanza kunijibu! Pambaf!
 
Cost-benefit analysis...
Naomba mtu afanye research kuangalia kama garama za kutokuwa na mkuu wa wilaya/mkoa ni kubwa kuliko garama za kuwa nae (mishahara, marupurupu, ofisi na matumizi mengine).

Nadhani ipo mikoa mingi imekaimiwa (haikuwa na wakuu) kwa muda wa kutosha ku-analyse impact.

Nadhani utafiti wa hivyo utatuwezesha kujenga hoja ya kuwaondoa hawa watu kwenye katiba mpya...
 
Wewe acha upungu, yaani anende mahakama hizi za JK? sio mwanasheria Lissu; tafuta mtu mwingine; hoja yake ilikuwa kusema ukweli ujulikane kama wanaona wamesingiziwa waende wao kunaka mahakama za JK; lissu atathibitisha.

Uelewe sio kila kitu upeleke mahakamani, hata kama unajua jambo kuhusu mkeo sio mpaka uende mahakamani unamwambie ajue unajua na zaidi aache uupuuzi huo. hata mahakama zinapendekeza suluhu nje ya mahakama; sasa iweje kila kitu waende mahakamani??? Lissu kasema analollijua kama mtu kaonewa ajibu au aende mahakamani.
 
Huyu Raisi Jakaya Mrisho Kikwete tumemchekea sana ameharibu mfumo mzima wa utawala na kugeuza nafasi za uongozi na taasisi kuonekana kama ni maeneo ya watu kufanyia mazoezi kwa vituko vyake ameshusha hadhi ya taasisi ya uraisi hivi leo kila mtu hapa Tanzania anadhani anaweza kuwa raisi awe mwizi ,mla rusha,nyang.anyi,vivyo kwenye nafasi za uwaziri,katibu mkuu,ukurugenzi,ukamishina,ukuu wa mkoa na ukuu wa wilaya

Mtindo huu wakudhoofisha nafasi umetufikisha mahala ambapo hakuna tena utawala wa sheria nchi inajiendea tu kama wacheza mdundiko kila mtu na staili yake Jakaya Mrisho Kikwete ni Raisi mbaya sana kuliko raisi yeyote aliyetawala nchi yetu ameharibu sana mfumo wa utawala kuanzia yeye mwenyewe kuingia madarakani kwa njia ya mtandao

Nadhani hata wananchama wenzie wa CCM wanamasononeko miyoni mwao kwa mambo wanayoyaona ,kipindi kilichopita amewapindisha wa kuu wa wilaya kuwa wakuu wamikoa waliotumikia ukuu wa wilaya chini yamiaka miwili kwa kweli huyu ni mtambo wa uchafuzi
 
Sehemu tamu kuliko zote katika hii picha ni kwamba...

Wote walifanyiwa vetting na TISS..

What a joke
 
Mkuu wangu angalia fact!

Kama lissu nae analalamika, basi itakuwaje kwa watanzania wa kawaida ambao hata sheria hatuzijui?

Upeo wako wa kuelewa ni mdogo plus ufinyu wa kufikiria ulionao, matokeo ni kibuyu tupu pole, kama ungefikiri, pengine ungeelewa ujumbe au nini anachotaka Mb Lissu. hoja hapa si kulalamika bali ni "tuhoji busara za uteuzi wao" je kuna tija kwa taifa? au ndo mwendelezo wa ufisadi.
 
AENDE MAHAKAMANI? Tundu ameonyesha ni kwa namna gani alivyo mwanasheria makini. LISSU aliyoyaeleza hapo ni makosa ya jinai (criminal offences), ambapo kwa mujibu wa sheria ni DPP 'pekee' anayeruhusiwa kushitaki mahakamani au watu/vyombo kama polisi na TAKUKURU alivyovikasimu au vilivyokasimiwa na BUNGE madaraka ya DPP kupitia sheria mbalimbali. Katika hili, yeye ni shahidi siyo mwenye kesi. HAYA ndiyo mambo ya CCM: u DC au u RC ni cheo cha CCM kinacholipiwa mishahara na marupurupu kwa pesa za serikali, kwa sababu watu hawa hawana kazi yoyote wanayofanya, na natangaza kuwa anayejua kazi za hawa watu kisheria zinazosaidia wananchi ajitokeze aniambie kuwa ni hizi ... (LISSU KAMA MTU BINAFSI anaruhusiwa tu kufungua kesi za madai, siyo jinai hivyo hakuna suala la kwenda mahakamani)

Mh.Lissu,
KJwa hilo la pili nadhani unatakiwa kwenda mahakamani na ushahidi huo maana kama hivyo ndivyo JK au Pinda wangefahamu vipi?..Kisha kincachotakiwa sasa hivi ni kupiga vita uteuzi wa Ma RC na DC isipokuwa wachaguliwe na wananchi wakazi wa sehemu hizo kupitia vyama vya siasa ama ushirika ambavyo vitaongoza kusikamia haki za wananchi wa majimbo hayo.

Nina hakika mkuu wa mkoa akiwa mkazi na kiongozi wa ushirika wa machimba madini basi Tarime hawatadhulumiwa mali ama ardhi yao pasipo kushikana mashati. Kubadilishwa kwa ma DC hakuwaathiri kitu hawa ma DC kwa sababu wameisha iba vya kutoka na kujiwekea msingi tayari kuanza maisha mapya. Walioliwa ni wananchi wa wilaya walioachwa watupu wakati DC kesha rudi makwao kujiendeleza zaidi na kama umewahi kufuatilia utagundua kwamba Ma RC na Dc wengi sana hujiimarisha makwao wakifungua biuahsra na kununua mashamba ambapo wananchi wa wilaya anayoongoza hawawezi kuyaona wala kuajua kinachoendelea. - Mungu tusaidie.
 
CCM kama vile wamepigwa ganzi. Yaani pamoja na kelele na viliio vya ubovu wa serikali yao, bado CCM inasimamia ilani yake isiyotamkwa ya kuifilisi na kuifisadi nchi hii. Mfano mzuri ni mada ya teuzi mbovu kama hizi.

Ni kweli kwa muda mrefu sasa wadau wengi tumepaza sauti kuwa hivi vyeo vya RC, DC na Meya na vingine kama hivyo
vifutwe. Mara nyingi sana vyeo havina tija kwa Taifa wala kwa jamii ya watawaliwa. Kutibu tatizo hilo michango ya sisi kujaribu kwenda kwenye mifumo mingine mfano utawala wa majimbo imetolewa. Hawasikii, nahawatasikia hata ikitokea maoni ya tume ya katiba nayo kupendekeza hilo. Maana wanaangalia ulaji wao tu.

Hivyo jukumu la ukombozi wa Tz ni bayana kabisa sasa ni la kwetu wenyewe. Inabidi tusisubiri 2015, tuanze sasa na kumaliza ikifika 2015
 
kwa kifupi ccm ndio inaenda kufia mkononi mwa hawa ma DC maana sijaona kabisa wakuu wa wilaya wengi tunao siri zao nyingi sana kwa mfano kuna mkuu wa wilaya moja amehamishiwa wilaya mpya kutoka Serengeti anamtoto anasoma sehemu flani ni aibu ya mwaka naona alichukua cheti kwa mtu au kilitegenezwa maana nilifuatilia hata high level sijui kamaliza lakini kwa sasa anasoma undergraduate ni hewa kabisa.
 
Lissu mwanasheria,

Nae analalamika wakati anazijua sheria, kwa nini basi asiwaburuze mahakamani wahusika? au ushahidi hautoshelezi?

Mfano suala la Milion 5, hadi zinaingizwa kwenye account au kupewa cash ilitakiwa wakamatishwe na technologia iliyopo

sasa kwa nini wasirekodi mahojiano ili wafikishwe mahakamani?

Huu ndio udhaifu wa hawa wanaojiita wapinzani, kazi kulalamika tu hata kama wana uwezo wa kitaaluma.

Shame!
Mahakama gani uliyotaka awapeleke ? yaani unakuwa kama huielewi system ?
 
Ndg wanaJf
Tanzania imegeuzwa Mali ya familia fulani na Marafiki zao
Tusipokuwa makini na kudadisi na kuchukua hatua hili litatutesa sana hasa katika uwajibikaji wa viongozi wetu.
Utamaduni huu wa kubebana hauishii tu kwenye uongozi pia tunauona hata kwenye Matumizi mabaya ya ofisi na pesa za umma.
Lt. Col. Benedict Kitenga-Kyerwa (mpya) huyu mteule alikuwa mkuu kikosi cha field engenier kati ya mwaka 2006 hadi 2008.Akiwa mkuu wa kikosi cha ujenzi alipewa kazi barabara moja kwao na Rais wakati anaendelea na ujenzi huu wa kirafiki alisafisha craper zote za vifaa chakavu vya kivita kikosini.Ananamjengo wa haja mji kasoro bahari kutokana na uhujumu huo.Usalama kikosini walijaribu kumfuata lakini hawakufanikiwa kumbe aliahidiwa ukuu wa wilaya ya Rolya leo fadhira zimempeleka KYERWA.ZMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA
 
Kusukuma maendeleo kunahitaji fedha kutelekeza mipango mizuri yanayobuniwa. Je, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wana mafungu ya shughuli za maendeleo. Kama siyo, basi mjadala ungeelekezwa namna ya kuwawezesha vinginevyo wanaweza kubakia mzigo kama wengine wanavyotaka kutuelewesha humu jamvini. Kukosoa tu wakati katiba inaagiza wateuliwe ni kupindisha mwelekeo wa majadiliano yasiyokuwa na tija. Tujaribu kuwa na majadiliano yenye tija.
 
Nimeangalia baadhi ya majina ya wateule hawa na kinachoonekana sio tu kwamba Ukuu wa Wilaya ni maalum kwa ajili ya makada wa CCM waliokosa pa kwenda bali pia mwendelezo wa mambo ya kifisadi ndani ya Serikali ya JK. Nitatoa mfano wa wateule wawili, Wilson Elisha Nkhambaku (DC mpya wa Kishapu) na Hassan Mazala (DC mteule wa Kilombero). Mwaka 2010 Wilson Elisha Nkhambaku alitaka kugombea ubunge kwa Kupitia CCM katika Jimbo la Singida Magharibi.

Katika kura za maoni alishinda kwa kishindo cha tufani lakini kama ilivyo jadi ya chama chao, alichakachuliwa kwenye NEC na mpinzani wake aliyemshinda, Mohamed Missanga, ndiye aliteuliwa kuwa mgombea. Baada ya uchakachuaji huo, Nkhambaku alijiuzulu uanachama wa chama chao na kuhamia CHADEMA ambako tulimteua kuwa mgombea wetu wa Jimbo la Singida Magharibi. (Nitazungumzia busara zetu au ukosefu wetu wa busara katika maamuzi yetu hayo wakati mwingine!)

Baada ya kuteuliwa kama mgombea na kampeni kuanza rasmi, Wilson Elisha Nkhambaku alirubuniwa na Lazaro Nyalandu (Mbunge wa Singida Kaskazini na, tulikuja kujua baadae, mlezi wake wa kisiasa wa miaka mingi) na kurudi tena CCM. Kwenye kampeni za uchaguzi huo, Nkhambaku alitumiwa sana kwenye kampeni dhidi yangu katika Jimbo la Singida Mashariki. Wakati ule tuliambiwa kwamba aliahidiwa ama kupewa pesa nyingi sana au kupewa Ukuu wa Wilaya baada ya uchaguzi. Of course hatukupatiwa ushahidi wowote wa kuthibitisha makosa hayo wakati huo.

Uteuzi wa jana wa Wilson Elisha Nkhambaku ni ushahidi tosha kwamba JK na chama chake ni watoa rushwa za uchaguzi wa wazi wazi. Sheria yetu ya Uchaguzi inakataza mtu yeyote kurubuni mgombea ili ajitoe katika kinyang'anyiro cha uchaguzi. Kosa hilo ni moja ya matendo haramu (illegal practices) ambayo adhabu yake ni pamoja na kupigwa marufuku kugombea na kufutwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, kosa la kutoa hongo (iwe ya kazi ama ajira, fedha, chakula, n.k) kwa mgombea au mpiga kura ni mojawapo ya matendo yaliyokatazwa (prohibited practices) na adhabu yake kwa mujibu wa sheria ni hiyo hiyo ya kufutwa kwenye Daftari na kupigwa marufuku kugombea. Kwa uteuzi huu Waziri Mkuu Pinda ajiandae kukabiliana na maswali ya papo kwa hapo juu ya uteuzi huu na kwenye mijadala itakayofuata Bungeni.

Kuhusiana na uteuzi wa Hassan Mazala, kwa wasiomfahamu bwana huyu, hadi anateuliwa kuwa DC wa Kilombero alikuwa Katibu wa Mbunge wa Singida Mjini kaka Mo Dewji, cheo ambacho amekishikilia tangu Dewji achaguliwe Mbunge mwaka 2005. Bifu langu mimi na yeye ni kwamba kwenye kesi ya kupinga uchaguzi wangu iliyomalizika mwezi uliopita Hassan Mazala ndiye aliyekuwa mgawa ngawila kwa mashahidi wa uongo waliokuja kutoa ushahidi dhidi yangu mahakamani.

Yeye mwenyewe alimpelekea shahidi namba 22 wa upande wa walalamikaji Hussein Musuna Mwangia (Katibu wa CHADEMA Jimbo la Singida Mashariki na wakala wangu kwenye uchaguzi Mkuu wa 2010) shilingi milioni tano cash ili awatolee ushahidi dhidi yangu. Bahati mbaya yao tu ni kwamba hawakujua wanadeal na wanaCHADEMA wa aina gani kwani mahela yaliliwa na wakapigwa bao mbele ya Jaji!

Siku chache tu kabla ya hukumu ya kesi yangu ya uchaguzi, Hassan Mazala na Mwigulu LM Nchemba (Mweka Hazina wa CCM) waliandaa mpango wa kumrubuni Diwani wa CHADEMA Kata ya Mungaa, Jimbo la Singida Mashariki, Bw. Matteo Alex Kiongo ahamie CCM baada ya kulipwa shilingi milioni ishirini! Mpango huo umekwama baada ya Diwani Kiongo kuwataka wampelekee mapesa hayo mchana kweupe nyumbani kwake. Hao tu ni maDC wawili wateule wa JK. Nadhani haitakuwa vibaya kwa wanabidii na wanamabadiliko kutupa taarifa zinazowahusu wengine katika orodha hii ya wateule ili tuhoji busara za uteuzi wao.

Wasalaam,

Tundu

(akiwaandikia WanaMabadiliko)

Source: wavuti - wavuti

Mh kiama chao hawa jamaa kinahesabika hivyo usihofu kabisa muda sio mrefu Mungu muumba wa dunia akitujalia maisha marefu tutawaona hawa jamaa wanaojulikana kama wakuu wa wilaya wateule wakiwa mbele ya mahakama kama walivyo wenzao leo walioshiriki kwa namana moja au nyingine katika mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1984. Tuko pamoja kamanda mpambanaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom