Tundu Lissu na Wakuu Wapya wa Wilaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu na Wakuu Wapya wa Wilaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, May 10, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nimeangalia baadhi ya majina ya wateule hawa na kinachoonekana sio tu kwamba Ukuu wa Wilaya ni maalum kwa ajili ya makada wa CCM waliokosa pa kwenda bali pia mwendelezo wa mambo ya kifisadi ndani ya Serikali ya JK. Nitatoa mfano wa wateule wawili, Wilson Elisha Nkhambaku (DC mpya wa Kishapu) na Hassan Mazala (DC mteule wa Kilombero). Mwaka 2010 Wilson Elisha Nkhambaku alitaka kugombea ubunge kwa Kupitia CCM katika Jimbo la Singida Magharibi.

  Katika kura za maoni alishinda kwa kishindo cha tufani lakini kama ilivyo jadi ya chama chao, alichakachuliwa kwenye NEC na mpinzani wake aliyemshinda, Mohamed Missanga, ndiye aliteuliwa kuwa mgombea. Baada ya uchakachuaji huo, Nkhambaku alijiuzulu uanachama wa chama chao na kuhamia CHADEMA ambako tulimteua kuwa mgombea wetu wa Jimbo la Singida Magharibi. (Nitazungumzia busara zetu au ukosefu wetu wa busara katika maamuzi yetu hayo wakati mwingine!)

  Baada ya kuteuliwa kama mgombea na kampeni kuanza rasmi, Wilson Elisha Nkhambaku alirubuniwa na Lazaro Nyalandu (Mbunge wa Singida Kaskazini na, tulikuja kujua baadae, mlezi wake wa kisiasa wa miaka mingi) na kurudi tena CCM. Kwenye kampeni za uchaguzi huo, Nkhambaku alitumiwa sana kwenye kampeni dhidi yangu katika Jimbo la Singida Mashariki. Wakati ule tuliambiwa kwamba aliahidiwa ama kupewa pesa nyingi sana au kupewa Ukuu wa Wilaya baada ya uchaguzi. Of course hatukupatiwa ushahidi wowote wa kuthibitisha makosa hayo wakati huo.

  Uteuzi wa jana wa Wilson Elisha Nkhambaku ni ushahidi tosha kwamba JK na chama chake ni watoa rushwa za uchaguzi wa wazi wazi. Sheria yetu ya Uchaguzi inakataza mtu yeyote kurubuni mgombea ili ajitoe katika kinyang'anyiro cha uchaguzi. Kosa hilo ni moja ya matendo haramu (illegal practices) ambayo adhabu yake ni pamoja na kupigwa marufuku kugombea na kufutwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

  Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, kosa la kutoa hongo (iwe ya kazi ama ajira, fedha, chakula, n.k) kwa mgombea au mpiga kura ni mojawapo ya matendo yaliyokatazwa (prohibited practices) na adhabu yake kwa mujibu wa sheria ni hiyo hiyo ya kufutwa kwenye Daftari na kupigwa marufuku kugombea. Kwa uteuzi huu Waziri Mkuu Pinda ajiandae kukabiliana na maswali ya papo kwa hapo juu ya uteuzi huu na kwenye mijadala itakayofuata Bungeni.

  Kuhusiana na uteuzi wa Hassan Mazala, kwa wasiomfahamu bwana huyu, hadi anateuliwa kuwa DC wa Kilombero alikuwa Katibu wa Mbunge wa Singida Mjini kaka Mo Dewji, cheo ambacho amekishikilia tangu Dewji achaguliwe Mbunge mwaka 2005. Bifu langu mimi na yeye ni kwamba kwenye kesi ya kupinga uchaguzi wangu iliyomalizika mwezi uliopita Hassan Mazala ndiye aliyekuwa mgawa ngawila kwa mashahidi wa uongo waliokuja kutoa ushahidi dhidi yangu mahakamani.

  Yeye mwenyewe alimpelekea shahidi namba 22 wa upande wa walalamikaji Hussein Musuna Mwangia (Katibu wa CHADEMA Jimbo la Singida Mashariki na wakala wangu kwenye uchaguzi Mkuu wa 2010) shilingi milioni tano cash ili awatolee ushahidi dhidi yangu. Bahati mbaya yao tu ni kwamba hawakujua wanadeal na wanaCHADEMA wa aina gani kwani mahela yaliliwa na wakapigwa bao mbele ya Jaji!

  Siku chache tu kabla ya hukumu ya kesi yangu ya uchaguzi, Hassan Mazala na Mwigulu LM Nchemba (Mweka Hazina wa CCM) waliandaa mpango wa kumrubuni Diwani wa CHADEMA Kata ya Mungaa, Jimbo la Singida Mashariki, Bw. Matteo Alex Kiongo ahamie CCM baada ya kulipwa shilingi milioni ishirini! Mpango huo umekwama baada ya Diwani Kiongo kuwataka wampelekee mapesa hayo mchana kweupe nyumbani kwake. Hao tu ni maDC wawili wateule wa JK. Nadhani haitakuwa vibaya kwa wanabidii na wanamabadiliko kutupa taarifa zinazowahusu wengine katika orodha hii ya wateule ili tuhoji busara za uteuzi wao.

  Wasalaam,

  Tundu

  (akiwaandikia WanaMabadiliko)

  Source: wavuti - wavuti
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Lissu mwanasheria,

  Nae analalamika wakati anazijua sheria, kwa nini basi asiwaburuze mahakamani wahusika? au ushahidi hautoshelezi?

  Mfano suala la Milion 5, hadi zinaingizwa kwenye account au kupewa cash ilitakiwa wakamatishwe na technologia iliyopo

  sasa kwa nini wasirekodi mahojiano ili wafikishwe mahakamani?

  Huu ndio udhaifu wa hawa wanaojiita wapinzani, kazi kulalamika tu hata kama wana uwezo wa kitaaluma.

  Shame!
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nathibitisha pasipo shaka kuwa Mazala ndiye mbeba fuko la rushwa la dewiji.
  Njoo Mwenyekiti wa uvccm Amani Nyekele ukanushe, kwani nawe ulibebwa na fedha za rushwa alizokabidhiwa mazala kutoka kwa dewiji na nyalandu, mpango mzima ikiwa mgombea wa kiti hicho kutoka iramba Amani Rai asiwatibulie safu mliyokuwa mkiipanga kumnadi nyalandu (mnyaturu mwenzenu) kuingia kwenye kinyang'anyiro cha urais wa jamhuri yetu tz
  Kilombero mmeletewa balaa na huyu jk, mtanuka rushwa mpaka kwenye masaburi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mdomo unatema!!!!!!
  nenda jf doctor upate angalau maelezo ya dawa!!!!
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Konyagi ndiyo inaongea ama?

  Ama ni chama cha majambazi at work!
   
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu angalia fact!

  Kama lissu nae analalamika, basi itakuwaje kwa watanzania wa kawaida ambao hata sheria hatuzijui?
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mh.Lissu,
  KJwa hilo la pili nadhani unatakiwa kwenda mahakamani na ushahidi huo maana kama hivyo ndivyo JK au Pinda wangefahamu vipi?..Kisha kincachotakiwa sasa hivi ni kupiga vita uteuzi wa Ma RC na DC isipokuwa wachaguliwe na wananchi wakazi wa sehemu hizo kupitia vyama vya siasa ama ushirika ambavyo vitaongoza kusikamia haki za wananchi wa majimbo hayo.

  Nina hakika mkuu wa mkoa akiwa mkazi na kiongozi wa ushirika wa machimba madini basi Tarime hawatadhulumiwa mali ama ardhi yao pasipo kushikana mashati. Kubadilishwa kwa ma DC hakuwaathiri kitu hawa ma DC kwa sababu wameisha iba vya kutoka na kujiwekea msingi tayari kuanza maisha mapya. Walioliwa ni wananchi wa wilaya walioachwa watupu wakati DC kesha rudi makwao kujiendeleza zaidi na kama umewahi kufuatilia utagundua kwamba Ma RC na Dc wengi sana hujiimarisha makwao wakifungua biuahsra na kununua mashamba ambapo wananchi wa wilaya anayoongoza hawawezi kuyaona wala kuajua kinachoendelea. - Mungu tusaidie.
   
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mungu Mkubwa, hawa wezi wote wa kura ambao wameteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya wataumbuka na kuumbuka mchana kweupe! Laana hii itawaandama vizazi kadhaa,watabakia na laana ya wizi! Mwisho CCM itakufa hivi karibuni,ikiacha nyuma uvundo wa viongozi wake!
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nimepetia orodha ya Wakuu wa Wilaya na hasa wakuu wapya na kusema ukweli tunafungua ukurasa mpya na wa kusikitisha. Cheo hiki kimeshuka thamani, kimechafuliwa na mbaya zaidi kimegeuzwa kwa the official CCM corruption platform.

  Sitoshangaa kusikia watanzania wakisema kuwa 'wanadharau' ukuu wa wilaya. Cheo hiki kinageuka kuwa fedheha, kinawapa madoa washika cheo hiki kwani wanaonekana wamekipita kama fadhila baada ya kushikiriki vitendo viovu. Wakuu wa Wilaya wanaonekana kuwa uzao wa utawala mbovu na wa kujuana.

  Na kama tutakumbuka mwaka jana bungeni, wabunge wa CCM walipitisha muswada ambao utawafanya wakuu wa Wilaya wawe ndio wasimamizi wa nidhamu ya mahakami katika wilaya zao! Sasa kama mtu mwenyewe sio msafi, ni mla rushwa atasimamia nidhamu ya mahakama kwa misingi ipi?

  Najiuliza, nani ameandaa hii orodha? Ni mambo gani yanayoangaliwa kabla hawajamteua mtu kushika nafasi ya ukuu wa wilaya? Na kama wananchi hawana imani na wateule hawa serikali inatoa wapi moral authority ya kusema ni 'serikali sikivu?
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mahakama zipi mkuu unazozirejea!
  hizi za majaji kama yule wa mahanga, au lema. hakuna mahakama yenye kuheshimika hapa tz.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Kwenye red: Lissu ameshawaburuza mahakamani - mahakama ya wananchi! Wao watatoa hukumu ya haki kuliko kutegemea mahakama ya ccm!
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu umegusia kuwa wakuu wa wilaya na mikoa wachaguliwe na wananchi wa maeneo hayo. Lakini swali langu kubwa ni kwamba do we really need them? Kuna article moja kwa title: "Wakuu wa mikoa, wilaya hawana tija kwa taifa" imejaribu kusasambua historia ya wakuu wa wilaya na mikoa. Kwenye artcile hiyo mwandishi anasema:

  "Ibara ya 145 ya Katiba ya 1977 (2005) inaweka bayana kuanzishwa kwa Serikali za Mitaa na kazi zake kwa maendeleo wa wananchi. Kwa msingi huu, Serikali za Mitaa zipo kwa mujibu wa Katiba ya 1977 (2005) zina wajibu wa kuwashirikisha wananchi katika kupanga mipango ya maendeleo ya maeneo yao.

  Ibara ya 61 ya Katiba ya 1977 (2005) imetaja kuwapo kwa wakuu wa mikoa, kazi na wajibu wao. Hata hivyo, ukiangalia mantiki ya kuwapo kwao (wakuu wa mikoa) hakuna tofauti sana na kuwapo kwa Serikali za Mitaa kwa jinsi yake. Suala la msingi hapa ni jinsi gani ya kutofautisha nafasi ya kiutendaji ya mkuu wa mkoa na uongozi wa Serikali za Mitaa kwenye ngazi husika.

  Ukiachilia mbali uteuzi na uwakilishi wao kwa Rais Mtendaji anayewateua bado kazi za viongozi hao ni za kisiasa zaidi badala ya kuwashirikisha wananchi katika kupanga na kusimamia mipango ya maendeleo. Kama suala lingekuwa ni kuongeza kasi ya utekelezaji na ufanisi wa harakati za maendeleo ya wananchi, kusingekuwa na haja ya kurudufu kazi za Serikali za Mitaa dhidi ya zile za wakuu wa mikoa! Kwa msingi huu, inawezekana CCM ilifanya makusudi kuanzisha uongozi wa mikoa na wilaya katika kurahisisha mfumo wa kutawala kisiasa kwa vile Serikali za Mitaa zinawajibika kwa watawala wa wilaya na mikoa zilizopo."

  Chanzo: Wakuu wa mikoa, wilaya hawana tija kwa taifa
   
 13. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ndege mjanja hunaswa katika tundu bovu. Let us keep an eye......
   
 14. m

  mdoe mchaina Senior Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo nimeipenda Kamanda Lissu mahakama ya wananchi ndio mwisho wa matatizo asante kwa kulileta kwetu .waache wao wawapeleke nyie kwenye mahakama zao ambako marefa ni wao washika vipendera wao na makamisaa wao ! Kwa nn wasishinde ukiona tumewashinda na huko ujue mabeki wetu wamekabia nje ya eneo la hatari hata penart hawakupata .
   
 15. Y

  Young zee JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 398
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Mkuu Mkandara, Mimi natofautiana na wewe kuhusu hili la Tundu lissu kuwapeleka hawa watu mahakamani. Huu ni mtandao mkubwa sana na siyo kwamba JK hajui, anajua sana ila ndio mfumo wao wa kuishi. Kesi ya Lissu iliratibiwa na CCM mkoa na taifa kwa kuwahusisha Ma DC, Kina Lyatonga mrema na mwanawe, Mkuchika na wengineo. Mungu tu ndo alisimama upande wa Lissu na wale mashahidi wa kununuliwa wakajichanganya na wengine kuogopa Mziki wa Lissu. Hivyo swala la rushwa wanalifahamu na hawatawatia hatiani ndugu/marafiki/mtandao wao tena kwa ushahidi ambao utakuwa hafifu pia.

  Kumbuka kilichotokea Segerea kati Fredy Mpendazoe na Mahanga, Pamoja na ushahidi wa kutosha na vielelezo vya kutosha, Jaji kaamua kesi infavour of mahanga. Hivo huu ushauri sio relevant, mwacheni Mbunge awatumikie watu wake.
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuwateua walioshindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM au walioshindwa kwenye uchaguzi mkuu, ni matusi kwa wananchi. Haiwezekani wapiga kura wamkatae mgombea halafu bado Rais aone kwamba anafaa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya na huku Rais akijua wazi kwamba Wakuu wa Wilaya ni wana siasa na hivyo kwa kiasi kikubwa wana-deal na wananchi moja kwa moja.

  Wakuu wa Wilaya wengi wanashindwa kushirikiana na wananchi na matokeo yake huishia kutoa amri au kutumia nguvu. Wananchi hawaoni sababu ya kushirikiana na mtu aliyekataliwa jimboni kwake halafu anapelekwa wilaya fulani kwamba anafaa kuwa kiongozi.

  Kuonyesha hiyo misuguano, majuzi tu Diwani mmoja wa CCM aliswekwa rumande pale Dodoma mjini kwa maagizo ya Betty Mkwasa. Sasa kwenye mazingira kama hayo hatutegemei diwani au wananchi watoe ushirikiani wa kutosha na mwisho wa siku hakuna lolote la maana wanalofanya zaidi ya kutia hasara.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  kesi ya nyani kula mahindi unampelekea ngedere awe hakimu wapi na wapi?
   
 18. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Sioni kama huyo Katibu wa Mbunge amelipwa fadhila.Iweje mipango yake yote ya kutaka kumwangusha Lissu isizae matunda halafu tudai kalipwa fadhila! Labda mimi mwenzenu sijui maana ya fadhila!!
  Ninavyojua fadhila ama shukrani hutolewa kwa mtu aliyekamilisha kazi aliyotumwa kufanya kwa mafanikio!Sasa huyu mwananchi amekamilisha kazi gani!Kilichokuwa kinamsumkuma kutenda alichokuwa anatenda ni hofu inayotokana na juhudi za Lissu kuipenyeza CHADEMA kwa kasi JIMBO la SINGIDA MJINI.Ni dhahiri alitambua kuwa ,hatma ya maisha yake imefungamana na matokeo ya uchaguzi ya UBUNGE mwaka 2015.Kuhusu Nkhambaku,hapo kweli maana halisi ya fadhila inaonekana wazi!
   
 19. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Misuguano ipo mingi sana. Mfano mwingine, Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Rombo mkoani Kilimanjaro liliwasimamisha watumishi 10 wakiwamo wakuu wa idara, kufuatia ripoti ya CAG kubainisha upotevu wa shilingi milioni 914. Hata hivyo, inasemekana viongozi wakuu watatu wa wilaya na mkoa, walipanga mikakati ili watendaji wakatae uamuzi wa Baraza la Madiwani kuwasimamisha kazi watumishi hao.

  Pia inadaiwa mkuu wa Wilaya aliitisha kikao ofisini kwake na kumshambulia mkurugenzi kwa kushiriki kikao cha madiwani kilichowasimamisha watumishi wa halmashauri. Kikao hicho kilifuatiwa na kingine kilichofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya na kuwashirikisha viongozi wawili wa mkoa na kuwataka watumishi waliosimamishwa na Baraza la Madiwani wapuuze agizo hilo na waendelee na kazi zao kama kawaida!

  Pia mwaka fulani kule Karatu, mkurugenzi wa halmashauri alikataa kumpa fedha kigogo wa serikali kwa maelezo kuwa alikwishapewa fedha za kujikimu tangu alipotoka Dar es Salaam kwa hiyo hakustahili kulipwa tena. Mkurugenzi huyo alipewa vitisho lakini alisimama kidete kutetea uamuzi wake. Alikuwa na bahati pia kuungwa mkono na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wa wakati ule.

  Chanzo: CCM inafuja uchumi wa nchi bila huruma
   
 20. c

  collezione JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mimi nasema,
  Kwenye katiba mpya. Tutoe haya mambo ya mkuu wa wilaya. Its jus wasting of our money.

  Kabla hata Lissu hajaongea, mimi nilishatilia mashaka siku nyingi huu uteuzi.

  CCM na serikali nzima ya JK hawana huruma na hela zetu, kufukuza mawaziri ilikua danganya toto tu. Wanakuja kuamishia ufisadi kwenye ukuu wa wilaya. This country should end by now
   
Loading...