Noel Shao
Member
- Jan 19, 2017
- 89
- 185
Uchaguzi wa Tanganyika law Society (TLS).
By; Noel C Shao.
Kampeni za nani anaenda kuwa rais wa TLS tarehe 17 pale jijini arusha, zimeanza huku kila upande ukijaribu kupinga upande wa pili hata kwa hoja zisizo na nguvu za kutosha.
Nilisoma andiko la Wakili Lekaita Edward huyu ambaye ni advocate of high Court nikapata Shaka kubwa na grounds zake alizo simamia kumpinga mgombe Tundu Lissu.
Hoja anazo simamia ni mbili;
#1. Majukumu
Anadai Lissu ana majukumu mengi hivyo atashindwa kumudu kuiongoza TLS, akiainisha anasema ni mbunge, mwanasiasa, mwanasheria mkuu wa chama cha siasa. Ndugu Edward kwa hii hoja yake anaonekana ameshindwa hata kusoma katiba ya TLS au ameisoma akaamua kuipuuzia. Nimepitia rules and regulations za uchaguzi sikuona kipengele chochote kinacho mzuia mtangaza nia mwenye majukumu mengi kutogombea nafasi ya urais wa TLS, hivyo hoja yake ni hafifu au haina mashiko kuhalalisha alicho sema.
Suala la kuwa na majukumu katika uongozi ni jambo la kawaida ambalo katika TLS linaweza lisiwe na madhara, akiwemo Lissu pale hataongoza kwa Sheria za lissu Bali za taasisi za TLS. Mbona jpm anayo majukumu chungu nzima, amiri jeshi Mkuu, mwenyekiti wa Ccm, mwenyekiti wa EAC, bado anatamani kuwa IGP akiamini anaweza kufanya yote hayo. Iweje kwa Lissu ashindwe?
2. Siasa.
Hoja yake ya pili anadai rais wa TLS hatakiwi kuwa mwanasiasa "ajabu" in this era? umpate mgombea asiye na upande wowote kwa hakika ni ngumu. Ni sawa utafute mtanzania anayependa mpira halafu asiwe Yanga wala simba.
Wakili Edward anamzungumzia lissu tu kuwa ndiye mwanasiasa, kwanini asinge muongelea Lawrence Masha? Mbona hajasema chochote kuhusu mgombea anaye ungwa mkono na kupigiwa debe na wana ccm ndugu Francis Stolla? Sitaki kuamini anazo hoja nyingine anazo jaribu kuzificha ndani ya hoja hizi mbili.
Kama ni insu ya kutokuwa political affiliated angerejea kwenye katiba yao inasemaje? Kadhalika hakuna kifungu kinacho mzuia kugombea katika Sheria za uchaguzi wa TLS as far as ni eligible member anaweza kusimama Kama mgombea ndio maana TLS wameridhika na sifa zake na kuamua kumpitisha.
Na swali la kumuuliza Wakili Lekaita, kwa uongozi uliopita wa John Seka na makamu wake Dr. N. Mvungi ambao hakuwa na chama chochote, wameifikisha wapi TLS, kipindi cha uongozi wao si ndio tumeshughudia marosoroso ya uvunjifu Mkubwa wa utawala wa Sheria? Katka uongozi wao si tuliona mawakili, wabunge wakiwekwa ndani? vitisho n.k
Vipi kuhusu kutoa matamko ya kukemea kukiukwa kwa Sheria wazi wazi? Walifanya? na yalikuwa na positive impacts gani?
Sina maana kwamba hakuna mazuri waliyo Fanya, la hasha, yapo na ya kukumbukwa ila ni wakati wa kuongeza nguvu zaidi hasa katika zama hizi.
Rais alitoa kauli ya mawakili wanao nenda kutetea wahalifu, nao kama kuna uwezekano wajumuishwe kwenye kesi? TLS imefanya jambo gani La heri juu ya jambo hili? Njia bora na ya pekee ya kupima uwezo wa uongozi ni kutazama mafanikio yake.
Nadhani Wakili Lekaita angezungumzia mapungufu ya katiba ya TLS, jinsi ilivyo shindwa kutenganisha suala la siasa na active laws. Kama katiba ya TLS ingetenganisha ingeweza kupunguza hii migongano.
Pili, kama angekuwa "fair" angechambua sifa za wagombea wengine siyo kumlenga Lissu pekee yake, angesema kuhusu Vitoria Mandari, Lawrence Masha, Francis Stolla, na Godwin Mwapongo. Na atoe hitimisho lake.
[HASHTAG]#Mytakes[/HASHTAG].
TLS Mpo katika mapambano ya uongozi tofauti, uongozi mpya katika historia, TLS mnahitaji rais mithili ya Lissu, mwenye ujasiri, asiye ogopa mapambano, anayekemea palipo paovu. Tangu TLS ianzishwe 1954 ni wakati wa kumsimamisha rais makini kuliko vipindi vyote vilivyo pita, vinginevyo ipo siku mtakuwa wa hanga wa nyakati hizi.
Jamii inawategemea nyinyi, bila nyinyi dhuluma, udhalimu vitatawala. Nyingi ndio watetezi wa haki mahakamani. Bila nyinyi wanasheria, all we are guilts vs the Court.
Rai wangu, TLS kuweni makini msijiwe weka uongozini kibaraka (puppet), taifa litaja lia kilio cha kupasua anga.
Noel Shao.