Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na mfano wa mzungu na mwafrika disco

Cherenganya

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
2,226
2,000
Miaka ile damu ikinichemka, nikiruka fance ya nyumbani na kwenda zangu kuruka majoka Kama tulivyokua tukiita enzi hizo, Disco likiwa linatawaliwa na nyimbo za kina BlackBox, Casanova, Patishange, Bob Marley, Kwenye charanga Kuna watu hatari toka Afrika Magharibi huku kibao Kama Aisha kikileta balaa na kujiona unaitawala dunia na vilivyomo na ni vipuuzi Kama havitii amri yako. Amma ujana maji ya moto.

Ndio kwa mbali nilipomuona MZUNGU mmoja akicheza huku Aki flashback kichwa chake na kwa kweli alivutia kila alipo fanya hivyo. Pembeni yake alikua mwafrika mmoja akaona asipitwe naye ageze ile flashback. Hapo ndipo watazamaji wakaamua kujiuliza mbona huyu havutii na kuonekana akiumia badala ya kufurahia?

Nikiwa Kijana mwenye kupenda kutafakari matukio nikagundua kwamba mzungu anafanya vile ili kuzirejesha nyuma nywele zake ndefu zilizoloana jasho na huyu muigaji na kipilipili chake akionekana Kama kituko.

TUNDU LISSU;
Yeye amepania kumuondoa madarakani Dr. Magufuli kwa kulipiza kisasi cha kudhani kwamba tukio la kupigwa kwake risasi kuna mkono wake na hana jingine nyuma yake.

He has the course to die for! Sasa wewe mwenye kipilipili mwenzangu kwanini unataka kuwa sehemu ya kufanikisha revenge ya Tundu Lissu?

Ndio hili ni lake na Dr. Magufuli na si la Watanzania. Kwakua ukiacha Mob Psychology mtu mmoja mmoja ukimuuliza kwanini hasa anataka Dr. Magufuli na CCM ing'oke madarakani hatakua na jipya zaidi ya kunga'ta kucha.

Labda niwaulize watanzania wenzangu? " Je Tunachohitaji ni kuondoa tatizo lililo ondoa matatizo"

Ndio Dr. Magufuli ni tatizo lililo ondoa Matatizo...

1. Zile nyimbo za Roma tulizozipenda za kubomoka kwa madaraja kwa kufoji wakandarasi (zimepatiwa majibu)

Zile verse za kuzimwa umeme ili mzigo wa magendo upite, magogo ya miti kununuliwa Tanga Kisha kupelekwa Kenya ili yaje Kama import! Wale Twiga walipokua wakipanda Ndege kwenda UAE!

Vimebakia historia.

2. Malalamiko yetu juu ya wafanyakazi wa TRA kuishi Kama miungu watu. Kila mtu kujifanya TISS ubabe na kutambiana. Madaktari kusaini daftari na kwenda kunywa chai hadi saa Tisa mchana anapokuja kutia saini ya kutoka.

Zile panda shuka za wawekezaji pale TIC, Mawaziri na wabunge kupishana angani kwenda Dubai kwa ajili ya vikao, Zile daily routine za vikao vya ndani vilivyokua vikifanyika kwenye mahoteli na au nje ya nchi Kisha kulipana posho!

3. Polisi walipokua wakishirikiana na majambazi, kufanya uhalifu.

4. Yale Madini pendwa ya Tanzanite yakionekana Yana soko kubwa India na Kenya kuliko pale Mererani?

5. Ile migomo ya Madaktari na wanafunzi vyuo vikuu, wale Viongozi wa umma waliokua wakienda kwa full blood picture India na Ujerumani zilikwi?

Je! Hatujifunzi kilichomkuta yule aliyemuiga mzungu ku flash back nywele zake?

NDEGE MMOJA ALIYE MKONONI NI BORA KULIKO WAWILI WA JUU YA MTI.

Nakupenda Tanzania nchi ya Baba na Mama.
 

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,459
2,000
Mnatusumbua sana na huyu mtu. Hatumtaki na hatutamchagua ana mikono ya damu
 

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
3,992
2,000
Yote haya ni sawa kabisa.

Basi fanyeni uchaguzi huru na haki ili Hao wapenda hizo mambo ulizosema hapo juu wamchague.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom