Tundu Lissu na karantini, hii imekaaje?

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
888
821
Baraza Kuu la Wanachadema jana walimpitisha Tundu Lissu kwa kura nyingi kuwa mgombea Urais kupitia chama chao.

Baadae nilimuona Tundu Lissu akipeana tano na mwenyekiti wa kudumu wa chama hicho ndg Mbowe. Baada ya kuona yote hayo nikagundua hakika hakuna chenye mwanzo kinachokosa mwisho.

Nahisi Tundu Lissu unaweza kuwa umefika mwisho wake wa umahiri wa sheria. Juzi Tundu Lissu alishindwa kwenda mahakamani kwa madai kuwa alishauliwa ajiweke karantini na daktari wake.

Je, niamini kuwa Tundu Lissu anaiogopa hii kesi? Kwanini aogope kwenda mahakamani kwa madai ya karantini lakini kabla ya wiki mbili za karantini kuisha alihudhuria mkutano wa jana? Siku za karantini ziliisha?

Tundu Lissu tumeanza kuona kuwa hii kesi unaiogopa na imekaa vibaya upande wako. Binafsi nakuombea ule mvua za kutosha, najua hii kesi imekukaa vibaya, na umejitahidi kujinasua lkn umeshindwa.

Usiogope kwenda mahakamani, haiwezekani usingizie karantini lakini mikutano ya chama unaenda. Pambana na khari yako. Ulitukana sana nchi yko huko ulaya, ukatukana Rais, mahakama, police, ukatukana mpaka bunge.

Umerudi kwa nchi hiyohiyo uliyoitukana, rais huyohuyo, mahakama na police zile zile.

Hayo maving'amuzi yako unayotembea nayo hayatakusaidia, unadanganya eti vyuma wakati ni ving'amuzi vya kukulinda havitadumu mzee, na jera utaenda navyo?

Service utafanyia jela?
 
Back
Top Bottom