Tundu Lissu na "Hard facts" and Werema na "Multi-pronged propaganda"

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,119
2,830
Kwa mwananchi wa kawaida anayetaka kuelewa "Kero za Muungano" atamwelewa zaidi Tundu Lissu kuliko maelezo ya Werema. Sikusudii kusema nani ni mahiri katika fani ipi, ninataka kuangalia tu ni nani amenifahamisha zaidi kero za muungano kuliko mwingine. Ni wazi kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uko katika hali mbaya zaidi sasa kuliko wakati wowote!!

Sheria ya Muungano, Makubaliano ya Muungano ndio yanaleta Katiba ya Muungano. Kukosekana kwa uhalali katika moja ya mambo mawili ya kwanza au yote yanaleta Muungano batili na bila kumung'unya maneno, Tundu Lissu kaonesha hilo. Ni wazi sasa;

a) Zanzibar ni nchi kamili kiutawala, bendera, wimbo wa taifa. Ni kamili kuliko hata siku moja baada ya Muungano 1964!
b) Rais wa Zanzibar ni Amiri Jeshi Mkuu.
c) Ni wazi sasa Katiba Mpya ya Zanzibar inakinzana na Katiba ya Jamhuri katika mambo ya msingi ya Muungano.
d) Baya zaidi hata tafsiri ya Muungano imekufa kabisa sababu nchi ya Tanganyika haipo tena.
e) Katiba mpya ya Zanzibar inatoa demokrasia kamili kwa raia wake kupitia Kura ya Maoni. Jamhuri ya Muungano inazuia hata kujadili jambo la kitaifa na bado inaitwa Serikali sikivu, inayoongozwa kwa utawala wa haki na sheria.

Ni vema sasa kabla hatujashughulikia kero za Muungano, tuandike Katiba ya Tanganyika na kisha tujadili aina na mfumo wa muungano, kama tutataka uwepo.

Saa ya kudai taifa lilioungana na Zanzibar na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefika!!!
 
Back
Top Bottom