Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Tusubiri, ukweli ukidhihiri uongo hujitenga. Kumbuka juzi, Sitta ingawa yupo busy bungeni lakini kaitwa na Pengo na kaenda mbio-mbio, jiuliize kunani?

Sita hakuitwa na Pengo.
Yeye mwenyewe ndio alimtafuta.
Na sio Pengo tu alenda pia kuonana na Mufti.
Unafaidika nini hasa na chuki zako za kidini Lakini ?
 
Ntazitafuta post zako za kumponda FaizaFoxy kila alipokuwa akiyasema hayo aliyoyasema Lissu jana na mengine. Nyerere niliwahi kusema humhumu JF ni ndumila kuwili.

Nyerere kuhusu Muungano wa Zanzibar alifata maelekezo ya Kanisa. Ngoja na Tundu Lissu aitwe na Kanisa muone kama hajabadilika, mtakuja kunambia humuhumu JF.

Kama leo mnavyodiriki kukubali maneno ya FaizaFoxy kwa kuwa tu yametoka kinywani mwa Tundu, basi iko siku mtayakubali na haya ya shinikizo la Kanisa. Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.

Wewe sasa ushahamia kwenye udini, sisi huko hatupo tunajadili muungano sie.
 
Ntazitafuta post zako za kumponda FaizaFoxy kila alipokuwa akiyasema hayo aliyoyasema Lissu jana na mengine. Nyerere niliwahi kusema humhumu JF ni ndumila kuwili.

Nyerere kuhusu Muungano wa Zanzibar alifata maelekezo ya Kanisa. Ngoja na Tundu Lissu aitwe na Kanisa muone kama hajabadilika, mtakuja kunambia humuhumu JF.

Kama leo mnavyodiriki kukubali maneno ya FaizaFoxy kwa kuwa tu yametoka kinywani mwa Tundu, basi iko siku mtayakubali na haya ya shinikizo la Kanisa. Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.
Pengo msimamo wake binafsi ni serikali mbili na kashamwambia Sitta...bado Lissu na yeye kupewa maagizo
 
Mkuu, nani amesema hapa kuwa Mwl. Nyerere hakuwa mwanadamu?.

Tukubaliane tu kuwa, Mh. Tundu Lissu amepasua jipu ambalo wengi waliogopa na wanaendelea kuogopa kulipasua. Kwa lugha inayoeleweka na wengi, amemchana chana Mwl. Nyerere na pamoja na kitabu chake cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania.

Hapa sasa mutaanza kuamini na kujua nini MZEE MUHAMED SAID anacho kiandika na kukisema kuhusu JKN
 
hivi watu wanajua maana ya kutukan kweli?walio hoji uhalali wa muungano enzi za ticha wote walipotezwa.
 
Wakuu, hotuba ya Kamanda Lissu Bungeni jana nina uthubutu wa kusema, tena kwa ujasiri kwamba tangu Tanganyika huru iwepo hatujawahi kushuhudia hotuba kali kama ile. Ni hotuba ya kisomi iliyojaa kila aina ya vielelezo na ushahidi, zaidi ya vielelezo 70 (footnotes), sio mchezo.

Ili kukata mzizi wa fitna nawaomba advocates wa Serikali 2 waje na ushahidi na vielelezo visivyo na shaka kukanusha paper ya Kamanda Lissu na sio kupayukapayuka bila mpango wala hoja za maana. I can see kwanini jamaa wanang'ang'ania Serikali 2 kwa udi na uvumba lakini bahati mbaya kwao kadiri wanavyozidi uking'ang'anizi wao ndivyo wanavyozidi kuharibu na kuachwa uchi wa nyama.

Poleni watetezi wa Serikali 2 ambao mnadhani mna akili na uzalendo kuliko Jaji Joseph Warioba, the former Attorney General of the Republic, Prime Minister and VP; kuliko Dr. Salim A. Salim, the former Minister for Defence, Primer Minister, and OAU Chief; kuliko Judge Brig. Gen. Augustine Ramadhan, the former high ranking member of the People's Armed Forces, NEC Chair, and the Chief Justice of the Supreme Court of the People of Tanzania; kuliko magwiji wengine lukuki waliokuwa wamejazana kwenye Tume ya Warioba. Jengeni hoja mueleweke kama Kamanda Lissu alivyofanya na sio kupayuka kama wendawazimu.

Nilistuka sana kusikia eti Nape Nnauye, W. J. Malecela, na Madabida eti wanazunguka huko na huko "kumjibu" Warioba na timu yake iliyojaa vichwa! Are we serious? Kafulila aliuliza Bungeni, hivi Warioba ni binadamu wa kutukanwa nchi hii? Hata kama alifanya makosa anapaswa kukosolewa kwa staha sio kwa matusi ya dhahiri au ya kificho. Kama kweli ni waungwana, CCM wanapaswa kumwomba msamaha Mzee Warioba na watanzania kwa ujumla.

Nakala: Pasco, Chris Lukosi, et. al.
Unaweza kuwa sawa kutokana na umri wako hiyo hotuba ukaipa hiyo hadhi.

Kulikoni leo umeshindwa kumtetea Nyerere kisa aliyesema hayo maneno ni mtu unampenda Tundu Lissu.

Punguza unafiki siku ingine watu wakieleza mapungufu ya Nyerere usitokwe na povu.
 
Mkuu.
Mbona ya Shivji , Mwakyembe na ya ma Proff. Hukuyasema.
Wale wale ambao hamsomi bible nzima, mnarukia viji mistari tu ili kujenga hoja zenu mfu.
By the way Lissu kaongea uongo kwani ?
Mkataba wa Muungano ni lini Serikali ya Kuanzia Nyerere mpaka JK ulipelekwa UN ?
Kuanzia janq binafsi nimeanza kumtizama the late Julius kwa jicho la tatu.
No wonder all the Problems we have now source yake ni yeye.

sasa kama mtu hadi vyombo vya habari alizuia mi namuona ka dicteta kwan alichotaka yeye ndo kifanyike kazuia maendeleo kwa muda mrefu
 
Sita hakuitwa na Pengo.
Yeye mwenyewe ndio alimtafuta.
Na sio Pengo tu alenda pia kuonana na Mufti.
Unafaidika nini hasa na chuki zako za kidini Lakini ?

Mkuu huyu FaizaFoxy ni mdini balaa! Yaani kamwona Pengo tu; Mufti kwake sio issue. Sometimes huyu ni wa kupuuza tu.
 
Last edited by a moderator:
sasa kama mtu hadi vyombo vya habari alizuia mi namuona ka dicteta kwan alichotaka yeye ndo kifanyike kazuia maendeleo kwa muda mrefu

Kwa kipindi chake kulikuwa na mantiki. Bila udhibiti ingekuwa vigumu kujenga misingi ya umoja wa kitaifa ukizingatia wakati ule hangover ya ukoloni na usultani ulikuwa bado dhahiri.
 
na pale alipomnukuu nyerere aliyoyasema gazeti la observer? Na baadae nyerere akawatia ndani waliohoji muungano? Huo si uongo wa nyerere?

mkuu uwe mkweli nachelea kukuita mtumwa wa mawazo yako mwenyewe! Wapi lisu alisema" nyerere aliishi kwa uwongo na udanganyifu" nukuu ya gazeti la observer ndo imekamilisha uongo wako? Kumbuka hata lisu anamheshimu na kuthamini mchango wa baba wa taifa.lete ushahidi onesha wapi lisu kasema hayo.vinginevyo ww ndo unamtusi mzee wa watu muacheni apumzike huko aliko kwa amani usimtumie baba wa taifa kummaliza na kumgombanisha lisu na watanzania. Kama huna cha kuandika kaangalie mambo mengine. Najua utakereka ila jaribu kuwa mkweli na unisamehe kama nimekukosea.leo ni siku ya kuabudu acha uongo
 
Lissu hajamtukana Nyerere amesema ukweli !

Mimi ni mtanzania na ninamuheshimu Nyerere na ninaamini alikuwa kiongozi mzuri na so far sioni kiongozi yeyote aliyekuja baada yake unayeweza kusema anafikia viwango vya Nyerere !

Lissu ameonyesha kwa USHAHIDI kwamba Nyerere alichokisema 1968 alikuwa anasema uongo. Nyerere alisema 1968 kwamba wanzanzibari wakitaka kujiondoa yeye hatawazuia, lakini baadaye (1984) imeonyesha kwamba alichokisema 1968 ilikuwa ni ulaghai/uongo ! Sasa kosa la Lissu ni kitu gani ? Kama Nyerere alisema uongo na Lissu amelionyesha hilo kwa ushahidi, kosa lake nini ?

Huu upuuzi wetu waTz wa kuacha kuambiana ukweli kwa kuogopana ndio unaoangamiza taifa letu !

Lissu omba radhi. Kumtukana Nyerere ni kuwatukana watanzania
 
Hakuna lolote linalo wapa msukumo wa kumjadili t.lissu bali ni upeo finyu wa kutafakari mambo.
Mimi mwenyewe ni mfuasi na mkereketwa wa siasa za j.k nyerere lakini kwa uchambuzi makini wa jana inanipa muono fulani kuwa uongozi unapande mbili.
1.mema kwa umma kwa manufaa ya wengi.
2.ubaya kwa wachache ili kujenga taifa lililo imara.
Hivi ndivyo mwalimu nyerere alifanya na kwa kipindi hiki cha kutoka kwenye makucha ya wakoloni wa ulaya na arabuni ili kuwa ni sahihi.
Wakati kwa kipindi hichi cha kupambana na mkoloni mweusi c.c.yem pia tundu lissu yuko sahihi kurejea mapungufu yaliyojitokeza ili kuweka mambo sawa kwa watanzania,
na itusaidie kupata katiba bora itakayoweza kudumu zaidi ya miaka 100.
Viva tundu lissu.
Tatizo unataka kuchukua vyote kwa maana kuwa unataka kukubaliana na hoja ya upande wa Mh. Lisssu. Vile vile unakubaliana na kile ambacho alikuwa anakijengea hoja ya kukiua katika fikra na mitazamo ya watu. Haiwezekani!.

Mh. Lissu anasema kimantiki kuwa, Mwl. Nyerere alitutapeli sisi Watanganyika na Wazanzibari kuhusiana na Muungano kwa maana kuwa, hata huu unaoitwa Muungano siyo muungano kwa sababu hauna hata hati maalum kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa. Hiyo hati hata Tanzania haipo na wale waliohoji, walifukuzwa na Mwl. Nyerere katika uongozi wakati alishasema huko nyuma kuwa hawezi kumpiga mabomu mtu yeyote anayehoji muungano kwa mapenzi yakena nchi.
 
Hakuna lolote linalo wapa msukumo wa kumjadili t.lissu bali ni upeo finyu wa kutafakari mambo.
Mimi mwenyewe ni mfuasi na mkereketwa wa siasa za j.k nyerere lakini kwa uchambuzi makini wa jana inanipa muono fulani kuwa uongozi unapande mbili.
1.mema kwa umma kwa manufaa ya wengi.
2.ubaya kwa wachache ili kujenga taifa lililo imara.
Hivi ndivyo mwalimu nyerere alifanya na kwa kipindi hiki cha kutoka kwenye makucha ya wakoloni wa ulaya na arabuni ili kuwa ni sahihi.
Wakati kwa kipindi hichi cha kupambana na mkoloni mweusi c.c.yem pia tundu lissu yuko sahihi kurejea mapungufu yaliyojitokeza ili kuweka mambo sawa kwa watanzania,
na itusaidie kupata katiba bora itakayoweza kudumu zaidi ya miaka 100.
Viva tundu lissu.

Sahihi kudanganya? sahihi kuwatia kizuizini wanaohoji? sahihi kuwaondoa nchini wanaokukosoa?

Tuweni wakweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom