Tundu Lissu-mwanasiasa mwenye nguvu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Hivi sasa Mashambulizi makali yanaelekezwa kwa Tundu Lissu.Kila hatua anayopiga au kauli anayoitoa inafuatiliwa na kufanyiwa upembuzi na watawala.

Watawala wamejifunza na kutambua hatari ya hatua na kauli za Lissu;Wako bize kujibizana naye moja kwa moja ama kwa kutumia mawakala wao waliowaajiri kwa kazi hiyo.Ukweli ni kwamba,Lissu si hatari kwa taifa hili,bali ni hatari kwa watawala.Watawala watapita,taifa litaendelea kuwepo.

Ukifuatilia Saikolojia ya watawala na hata lugha yao ya picha wanapohutubia wanaotuonesha jambo moja tu:Tundu Lissu ni mwana siasa mwenye nguvu na uwezo katika historia ya upinzani nchini.Mapito aliyopitia kufikia alipo sasa ndicho kilichomzidishia nguvu na uwezo.Lissu amevuka viwango vya mapambano.

Kielelezo cha hili ni heshima anayopewa duniani na coverage inayofanywa na media za kimataifa ili dunia imsikilize.Huyu mwana siasa anayesikilizwa sana na duniani anawapa taabu watawala.Watawala wanataabika na kuteseka.Naam,wataendelea kutabika na kuteseka kwa sababu Tundu Lissu amenusuruka kimuijiza ili kuangusha tawala.

Watu waliopona kimuujiza kama Tundu Lissu Kupona kwao si kwa ajili kuishi kwa ajili yao na familia zao bali ni kwa ajili ya maisha ya kupambana ili ku- achieve Mission yenye faida kwa wengi.

Tundu Lissu anajitambua;kuanzia jinsi alivyojitolea kuishi maisha kufanya struggle.Mapito ya kukamatwa na kuwekwa ndani ni mengi.Lakini Yale Mapito ya political assassination yalikuwa makubwa kwani alikuwa anapoteza maisha.Mungu amekataa asife.

Siku fulani kabla ya kushambuliwa Dodoma Lissu aliwahi sema "tutanyamza tukiwa wafu"

Baada ya kushambuliwa,kule Nairobi alipozinduka kauli ya kwanza aliyoongea ni " I have survived to tell the tale" yaani "nimenusurika ili niwaambie hadithi" (kwa tafsiri yangu).

"To tell tale" bila shaka ni kuendelea na mapambano.Kwa hiyo,Lissu anajua kazi iliyoko mbele yake na hana mpango wa kuiacha kwa sababu yoyote ile.Hiki ndicho kinachotesa watawala na vibaraka wao.

Haya ni maneno ya mtu jasiri yanayothibitisha Lissu ana mambo mengi kwa ajili ya taifa hili.Kunusurika kwake haikuwa bure.Kuna kazi mbele yake.Sasa hakuna wa kumzuia maana Mungu amekataa asife kutokana na kushambuliwa 2017.Hiki ndicho kinachowatesa watawala na vibaraka wao.

Mwanahabari Huru
Magomeni mwembechai
 
Nashauri Tundu Lissu angesitisha sasa hizo ziara za kuingea na watanzania waishio huko kuhusiana na yaliyompata.
Hizo ziara ndefu zinapunguza uzito wake na ule wa hoja zake, atazoeleka na kuanza kuonekana mwepesi na wa kawaida.
 
Jamaa kaona thread za kumuhusu Lissu zimeadimika ameamua afufuke..! Kweli wanamkakati muna mambo mengi gizani (Dark Politics)
 
Wewe unadhani ataishiwa ya kuongea kwa maana watakuwa wameyazoea???!
Pole sana anamengi kama alivyo samaki tu,hayo anayotema niyaliyojaa pomoni kumbe mda ukifika anakuja kivingine na siyo kuendelea kusimulia mashambulio yake tena.
Hapo sasa sera zinahusika zaidi,hivyo nashauli aongeze sipidi yakuzungumza
Nashauri Tundu Lissu angesitisha sasa hizo ziara za kuingea na watanzania waishio huko kuhusiana na yaliyompata.
Hizo ziara ndefu zinapunguza uzito wake na ule wa hoja zake, atazoeleka na kuanza kuonekana mwepesi na wa kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safari za Lissu sio za bure za kimkakati na zina maana yake ,Lissu hatembei bure ana mipango ya uhakika yaani ukitaka uongozi lazima uppate sapoti ya nnje na ndani ,sasa hapo mwenye kuelewa ataelewa .
 
..huyu bwana ana kipaji cha siasa.

..na jambo lingine ni kwamba yale anayoyasimamia na kuyatetea ni WITO wake.

..sasa ni vigumu sana kupambana au kushindana na mtu wa aina hiyo.

..Angalia hiyo Press Conference yake. He spent 3 hrs talking and answering questions bila kuchoka.

..Na hata wasikilizaji wake hawakuchoka na ku loose attention.

..Huko chama tawala CCM mikutano yao utakuta kuna kikundi cha muziki, kikundi cha wachekeshaji, viongozi wa dini, na utitiri wa wazungumzaji, ili kuweza kuendesha mkutano wa masaa matatu.

Cc tindo, Nguruvi3, Malcom Lumumba
 
Back
Top Bottom