Tundu Lissu mtu wa Singida, Constantine Masawe umefuata nini Tarime? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tundu Lissu mtu wa Singida, Constantine Masawe umefuata nini Tarime?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkeshaji, May 25, 2011.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya Bw. Constantine Masawe amesema Tundu Lissu na watuhumiwa wengine watatu ni watu wa Singida hivyo wanawahoji wamefuata nini Tarime.

  Nionavyo mimi watu wa aina hii ya Masawe wanatupeleka pabaya. Iweje leo mtu wa mkoa mmoja azuiliwe kuingia mkoa mwingine ndani ya nchi hii huru isipokuwa kwa ruhusa ya Polisi.

  Kama Tundu Lissu ni mtu wa Singida na yuko Tarime na hilo linaonekana ni jambo la ajabu kwa Masawe, je yeye kamanda Constantine ni Masawe wa Tarime?
   
 2. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,825
  Likes Received: 924
  Trophy Points: 280
  Kwani Huyu Massawe amezaliwa ama ni mkurya wa Tarime?!! ufinyu wa mawazo unamsumbua kama wakubwa wake walivyo hohe hahe kiakili!!! haya mapolisi ndio maana yanalaniwa yanakufa yakiwa na laana..yanaua watanzania wenzao baadae yanageuka kufanya sanaa..mbona yanashindwa kuzuia vibaka!!!
   
 3. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo anamaanisha mtu wa mkoa mwingine haruhusiwi kwenda mkoa mwingine? Watu kama hawa hatuwahitaji kwa maendeleo ya Taifa ni wabaguzi wa kimkoa.
   
 4. N

  Nanu JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hiyo sentensi ya Masawe Constantine ni ya kibaguzi na ya kikabila. Kama ingekuwa enzi za mwalimu na kibarua kingeota majani. Kiongozi lazima uchunge sana ulimi wako. Hata kama kila mtu ana haki ya kuzungumza lakini kwa kiongozi hasa wa serikali kama Masawe lazima uchunge sana ulimi wako!!!! Lakini hata kukemewa inawezekana isifanywe na wakubwa zake!
   
 5. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi alivyokuwa akiongea bila aibu alikuwa akimaanisha kuwa ni kosa kwa mtu wa mkoa mmoja kuonekana mkoa mwingine. Veeeere Strenji.
   
 6. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  huyo IQ yake iko chini sana something below zero, ana matatizo na hiyo inareflect aina ya watu walio katika Jeshi la polisi ambao ni NDIO MZEE na wanatumiwa na CCM kufanya mambo ya ajabu. hiyo dhahabu yenyewe wanakula kwa macho halafu wanakuwa vibaraka.
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kwakweli mimi Ilinisikitisha sana kwa kauli yake hiyo yaani anamaanisha hapa dar wengiwetu hatusitahili kuwepo, twende mikoani kwetu, Halafu ile ulikuwa ni msiba sasa utaulizaje watu wasingida wamefuata nini? KWA HIYO SIKU HIZI HATA MISIBANI TUNAULIZANA UMETOKA WAPI NA UNAFUATA NINI!? AAAH MASAWE ANAAIBISHA GESHI YA POLISHI!
   
 8. M

  Makupa JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hii ndio sumu alichochea Nape
   
 9. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  JWTZ walishirikishwa kushiriki uifsadi wa madini ya nchi hii kupitia Meremeta, Polisi nao wameamua kuwa beneti na wawekezaji ndio maan hata vifungu vya Katiba vinawekwa kando.
   
 10. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kidogo kidogo watu wataombwa pasi ya kusafiria kwenda mkoa mmoja hadi mwingine.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Aliimanisha mfano: wewe mkurya, Mpare hapaswi kukutetea.....Utatetewa na Mkurya mwenzako
   
 12. wasaimon

  wasaimon R I P

  #12
  May 25, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uchunguzi wa miili ya maiti wanne waliopigwa risasi na askari polisi katika Mgodi wa African Barrick North Mara uliofanywa na daktari bingwa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Makatta imebaini kuwa marehemu wote walipigwa risasi maeneo ambayo hayakulenga kujeruhi, bali kuua.

  Uchunguzi huo uliochukua saa 4:27 ulianza saa 5.20 asubuhi hadi saa 9.47 alasiri. Upande wa familia za wafiwa ulisimamiwa na Dk Greyson Nyakarungu kutoka Hospitali ya Wilaya ya Tarime na askari wawili. Taarifa hiyo itakabidhiwa kwa hospitali

  Source Mwananchi

  Dk Nyakarungu alisema Emmanuel Magige mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari namba za PM1/5/2011 (TGH), alipigwa risasi katika nyonga ya kushoto ambako kulikuwa na tundu la duara llilokuwa na upana wa sentimita 0.5 ilipoingilia na sentimita 2.5 ilipotokea.

  “Mishipa ya damu iliharibiwa, kibofu cha mkojo, mishipa ya fahamu, mfupa wa nyonga ulisagika, damu ikavia ndani ya tumbo, lakini chini ya mgongo karibu na risasi ilipotokea kulikuwa na tundu linaloonyesha kuwa alichomwa na kitu chenye ncha kali kama singa ya bunduki,” alisema na kuongeza:

  “Tumebishana sana kwa hilo wenzangu wakidai huenda aliangukia kitu kikamchoma, ikumbukwe kuwa alipigwa kwa nyuma akikimbia hivyo asingeweza kuanguka chali zaidi ya kifudifudi,” alisema.

  Kuhusu Chacha Ngoka mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM 2/5/11 (TGH), uchunguzi ulibaini kuwa alipigwa risasi mgongoni karibu na kiuno na kutokea katikati ya mbavu chini ya titi, tundu la kuingilia likiwa ni sentimita za duara 0.3 na ukubwa wa tundu pa kutokea ikiwa ni sentimita tano.

  Mishipa mikubwa ya damu iliharibiwa, ini likasagwasagwa, damu iligandia kwenye mfumo wa upumuaji hali ambayo inadhihirisha kuwa alipumua kwa nguvu, damu ilikwisha mwilini na kuwa alipigiwa risasi kwa mbali.

  Alisema marehemu Bhoke mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM/3/5/11(TGH) alipigwa risasi ya kichwani karibu na sikio na kidonda chake pakuingilia ni sentimita za duara 0.2 ,pa kutokea sentimita tano za duara kwenye paji la uso hivyo kuharibu ubongo, fuvu na mifupa yote kubomolewa.

  Kuhusu uchunguzi wa Mwikwabe Marwa Mwita mwenye jalada la uchunguzi wa kidaktari PM/4/11 (TGH) alisema alipigwa risasi karibu na nyonga na kuacha tundu la sentimita za duara 3,5 na risasi haikutoka nje na kuharibu mifupa yote ya nyonga, misuli ikawa imeharibiwa na kipande cha risasi kilikutwa katikati ya misuli (PSOAS), damu ikiwa imevia tumboni.

  “Kilichoonekana hapo ni kuwa walipigwa risasi kwa mbali tena kwa nyuma maana wote zimeingilia kwa nyuma na maeneo waliyopigwa risasi ni yale ya kuua si kuwapunguza nguvu kama walikuwa wamegoma kusalimu amri,” alisema daktari huyo.
   
 13. U

  UNDULE ROBERT Member

  #13
  May 25, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani busara inahitajika katika kutoa maoni. Nadhani kuna shughuli ilimpeleka tundu lissu. Lakini kamanda alishindwa kutambua shughuli hiyo.
   
 14. delabuta

  delabuta Senior Member

  #14
  May 25, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa mkuu roho inaniuma sanaaa.inaeleweka
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Unajua kuna polisi wengine hawajui ku-reason vitu akili zao kama ****** ya kuku
   
 16. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Makamanda aina ya akina Massawe ni aina ya akina capten John Komba (waimba ngonjera), nk. Hawa waliingia jeshini kwa kueneza itikadi za siasa ya ujamaa na kujitegemea. Ndo maana utakuta polisi wetu hawa linapotokea tukio la ujambazi wanakuja saa moja baada ya tukio, lakini maandamano ya CDM, CUF wanapata taarifa za kiintelijensia wiki kabla ya maandalio. Wapo pale kisiasa zaidi.
  Polisi fanyeni kazi yenu kama polisi, vinginevyo ieleweke kuwa Tanzania hatuna polisi bali ni green guard. Hivi ukimfuga mbwa halafu akamgeuka mwenye mbwa inakuwaje?​
   
 17. D

  Dr.Mbura Senior Member

  #17
  May 25, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lissu ana majibu mengi mengi anaweza kumwambia Masawe mimi ni mwasheria nimeitwa na wanafamilia waliouliwa ndugu zao kwa ajili ya msaada wa kisheria basi!
   
 18. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  haya sasa,watanzania wanajua kuchambua kauli saivi like never before
   
 19. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  ndo maana ****** wa rugoba hajatoa pole kwa mkurya wa mara.nmemuelewa vizuri massawe.
   
 20. S

  Shamwile Member

  #20
  May 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata mimi nimeshangazwa na kauli ya Massawe, anaonyesha ni jinsi gani alivyo na ufinyu wa mawazo, na hii inaonyesha kuwa ukweli wa tukio zima la mauaji ya Tarime anajua ila kutokana na kupewa maagizo na chama cha magamba anaamua kuchakachuwa ukweli, that's why anakosa hata busara ndogo ya kuingiza hoja dhaifu ya kusema kwamba kwa nini watu wa mkoa mmoja wanaenda kwenye mkoa mwingine katika tukio kama la msiba, shame on you Kamanda Massawe!!!!!!!!!!!
   
Loading...