Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mzee Robert Mugabe katika uzee wake akiwa na miaka 91, ameona ni jambo la hekima kuandika kitabu kwa ajili ya kumuenzi muasisi wa taifa letu marehemu Julius Nyerere. Mzee Mugabe ameona ni bora awakumbushe wanasiasa wa kizazi cha sasa, kuhusiana na uwezo aliokuwa nao Marehemu Nyerere kisiasa na katika mambo mbalimbali yenye mahusiano na maisha ya mwanadamu. Mwalimu Nyerere anaheshimika kote ulimwenguni, alijaliwa busara na akili yenye kufanya kazi kama kisu kilichonolewa vizuri.
Binafsi niliduwazwa na kauli za kejeli alizozitoa bungeni mheshimiwa Tundu Lissu wakati wa bunge maalum la Katiba. Wala hakuonyesha kwamba labda aliongea kwa makosa, alizungumza kwa kujiamini kabisa. Namshauri awe na tabia ya kusoma vitabu vingi na sio vile vya mambo ya sheria peke yake. Akitafute kitabu hiki kilichoandikwa na Mzee Mugabe ili aweze kutambua mchango wa Mwalimu Nyerere kimataifa kama mwanasiasa, mwanazuoni na mwanajamii. Kiburi cha kisiasa hakiwezi kumjenga kama mwanasiasa ikiwa hatajenga tabia ya kuuelewa ulimwengu mwingine mbali kabisa na masuala ya kisheria.
Mzee Mugabe ni msomi mahiri na mwanasiasa mwenye misimamo mikali, wapo wenye kumdharau na wapo wenye kumpenda. Ameona ni bora wakati nguvu za mwili wake zikizidi kupungua, aandike kitabu cha kumuenzi mtu ambaye aliyagusa maisha yake kwa namna ya kipekee. Tundu Lissu akisome kitabu hiki, naamini ujumbe atakaokutana nao utampatia nafasi ya kumuelewa Hayati Mwalimu Nyerere katika mtazamo wa kimataifa zaidi.
Na sio Tundu Lissu pekee mwenye kutakiwa kukisoma kitabu cha Mzee Mugabe kumhusu Mwalimu Nyerere, wanasiasa wa kiafrika wengi ambao bado wanazo ndoto za kufanya makubwa maishani, wajitahidi kujifunza mengi kupitia kitabu hiki.