Tundu Lissu: Mnapoambiwa tumekombolewa, mjue ndani ya miaka 5 tumekopa zaidi ya trilioni 40 na bilioni 500 kutoka kwa mabeberu

Ccm haina muda wa kumpa kiki lissu. Ccm ilishawajibu wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
Umeme kila kijiji, bwawa kubwa kabisa la umeme mto Rufiji , daraja refu kabisa Afrika mashariki na kati pale kigongo ferry, vituo vya afya kila kata, watoto wetu wanasoma bure, treni ya umeme, meli ziwa Victoria na nyasa.

2020-2025 twende na jembe kutoka Chato. John Magufuli.
 
Mwananchi wa kawaida ukimwambia umekopa sijui tunadaiwa hakuelewi
Mwambie utamsaidia vipi kumsafirishia mazao yake au kumpa bei nzuri
Ukianza kumtandika kodi za ajabu, kutompa huduma stahiki kwenye kilimo kama pembejeo nk na kumbambikia kesi uhujumu uchumi ili ulipe lile deni hapo itabidi akuelewe sasa eti ee.
 
Lissu anaishia kulaumu tu bila yeye kusema atafanya nini,hatokopa fedha ama akikopa atakopa kiasi gani na kwaajili ya nini,awe anaweka na mbadala wa yeye nini atafanya kuliko yeye kulaumu bila kuonyesha njia.
Ngoja kampeni zikianza atazungumza yote.
 
Hapa Lisu katoa Boko!

Hatujakopa fedha zote hizo!

Aliyempa data hizi Lissu kamlisha kasa, inabidi kitengo cha takwimu na data cha Chadema kifanye homework yake vizuri au msoma takwimu mwenyewe awe makini kwenye kusoma data
Huyu anayetoa taarifa ndio anachemka.
 
Akiongea na wananchi(probably mkoani Dodoma), Lissu amedai tunapombiwa tumekombolewa, tuelewe mpaka kufikia April ya mwaka huu, serikali ilikuwa imekopa jumla ya shilingi trilioni 40 na bilioni 500 kutoka kwa mabeberu.

Namdi Azikiwe. (@NamdiAzikiwe) on Twitter
Maendeleo yanayoletwa na mikopo hata siku moja hayakuwahi kuwa sustainable,na hiyo ndo inadhirihirisha utofauti wa maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu
 
Nimeisikiliza hotuba ya Lissu akiongelea kuhusu vitu mbalimbali ikiwepo Tsh trilioni 40 ya mkopo. Lissu anasema hii pesa imekopwa kutoka kwa "mabeberu" katika kipindi cha utawala wa Magufuli.

Naomba wana CCM wajibu kama haya yaliyosemwa ni ya uongo.
View attachment 1532081
Walio twambia tumefikia uchumi wa kati tunajisifia hadi sasa ni haohao mabeberu
 
Ccm haina muda wa kumpa kiki lissu. Ccm ilishawajibu wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
Umeme kila kijiji, bwawa kubwa kabisa la umeme mto Rufiji , daraja refu kabisa Afrika mashariki na kati pale kigongo ferry, vituo vya afya kila kata, watoto wetu wanasoma bure, treni ya umeme, meli ziwa Victoria na nyasa.

2020-2025 twende na jembe kutoka Chato. John Magufuli.

Nafikiri CCM haina majibu kuwa pesa yote iliyotumiwa kuleta maendeleo ilikopwa kutoka kwa "mabeberu".
 
Kwamba anataka kusema akiingia madarakani serikali

yake itahakikisha hatutokopa kabisa au nn maana yake?
 
Hana hoja! Watanzani wana mchora tu! Na atapata majibu yao October 2020.
===
Nyakati hizi ni za nchi mbalimbali kuhakikisha kuwa zinajidhatiti kiuchumi na kiusalama. Je. Lissu, anasema nini juu ya hili kimikakati na kadhalika!? Hana hoja juu ya mambo haya mazito.
Hujajibu hoja, kama nchi imekopa hizo au la, tena kwa mabeberu!
 
Kwamba anataka kusema akiingia madarakani serikali yake itahakikisha hatutokopa kabisa au nn maana yake?
La hasha, nchi itakopa, ila itaweka wazi kuwa si fedha za ndani! Unajua wimbo uliopo sasa ni kwamba tunajenga miundombinu kwa fedha za ndani!
 
Lissu anaishia kulaumu tu bila yeye kusema atafanya nini,hatokopa fedha ama akikopa atakopa kiasi gani na kwaajili ya nini,awe anaweka na mbadala wa yeye nini atafanya kuliko yeye kulaumu bila kuonyesha njia.
Tulieni hizo ni salamu tu kampeni ikianza atawaambia awafanyie nini
 
La hasha, nchi itakopa, ila itaweka wazi kuwa si fedha za ndani! Unajua wimbo uliopo sasa ni kwamba tunajenga miundombinu kwa fedha za ndani!
Lakini pamoja na kwamba tunakopa,kwani ni uongo hakuna

miundombinu inayoendelea kwa fedha za ndani tu?
 
Ccm haina muda wa kumpa kiki lissu. Ccm ilishawajibu wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
Umeme kila kijiji, bwawa kubwa kabisa la umeme mto Rufiji , daraja refu kabisa Afrika mashariki na kati pale kigongo ferry, vituo vya afya kila kata, watoto wetu wanasoma bure, treni ya umeme, meli ziwa Victoria na nyasa.

2020-2025 twende na jembe kutoka Chato. John Magufuli.
umejibu swali?
 
Back
Top Bottom