crocodile
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 3,864
- 2,951
Utaniambia walikuwepo Fastjet. Hao hawakuwa na mtandao mpana. Ni kampuni ya nje ilichungulia fursa kwenye route chache wakafanya biashara kwenye hizo route. Wengi wa waliokuwa wadau wa route hizo ndio wanaowasifia . Atcl wana mtandao mpana zaidi..Hii sio opinion ni fact tu hata kwenye mitandao unaweza kuiona..Wakati ATCL ilipokuwa imekufa watu walikuwa wanasafiri vizuri na ndege tena kwa bei nafuu.
ATCL hajaongeza tija yoyote kwenye usafiri wa ndege nchini.
Mataifa chungu nzima yaliyoendela na yanayojielewa yameiachia hii biashara sekta binafsi.
Wanahitaji kuboresha uendeshaji na kuwa aina ya ndege na idadi yenye tija.