Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Tundu Lissu amesema mali isipokombolewa baada ya kuzuiliwa, itapigwa mnada ili kufidia deni linalodaiwa. Kwa muda gani, inatagemea mkataba Serikali uliongia.

Tundu Lissu alikuwa anajibu swali la mdau aliuliza nini kitatokea kama Serikali itashindwa kulipa deni lililopelekea ndege kukamatwa.

Lissu amesema Serikali inadhani inaweza kuvunja sheria/mikataba na kusiwe na consequences wakati imeingia mikataba ya kimataifa, Lissu amedai Serikali inajiona ina nguvu ndani ya nchi na kudhani inazo nguvu hizohizo nje ya nchi matokeo yake wawekezaji wanasubiri mali zitoke nje ya nchi kwakuwa hawawezi kukamata mali za kidiplomasia kama majengo ya ubalozi.

Kuhusu mtu aliyefariki kushtakiwa, amesema kama kesi ya jinai, kesi za jinai ni kwaajili ya walio hai. Ikiwa ni madai wanaweza kushtakiwa warithi lakini baadhi ya madai yanakufa na aliyekosea.
 
Lisu meno yote nje kwa furaha ndege za Tanzania zikikamatwa!
Watanzania tudai kodi tuliyotumia kumsomesha Lisu hana faida yoyote kwa taifa.

Kama ndege hazikupigwa mnada enzi ya Magufuli hazitapigwa mnada tena
 
Mkataba uingie wewe, mkataba uvunje wewe kwa kukurupuka, ndege ikamatwe unataka tuliepamoja? Lawama ziende kwa Lissu ili iweje? Pambaneni na madeni yenu sio kujificha wakati mambo mmeboronga wenyewe
 
Lisu meno yote nje kwa furaha ndege za Tanzania zikikamatwa!
Watanzania tudai kodi tuliyotumia kumsomesha Lisu hana faida yoyote kwa taifa.

Kama ndege hazikupigwa mnada enzi ya Magufuli hazitapigwa mnada tena
Kama wewe na wenzako mngekuwa na uchungu, msingeendelea kufanya maamuzi ya hovyo! Halafu mwisho wa siku mnakuja kuwaumiza walipa kodi.

I wish kungekuwa na sheria ya kuwafilisi wale vilaza wote mnnao liingizia Taifa hasara za kipuuzi kama hizi.
 
Mkataba uingie wewe, mkataba uvunje wewe kwa kukurupuka, ndege ikamatwe unataka tuliepamoja ? Lawama ziende kwa lissu ili iweje? Pambaneni na madeni yenu sio kujificha wakati mambo mmeboronga wenyewe
Hiyo mikataba ilikuwa na faida gani kwenye Nchi yako.

Huyo Lisu kama anaakili angetafuta namna ya kuinusuru nchi yake otherwise ni msaliti tu.
 
Hizi tetesi za ndegr kukamtwa sijasisikia bado Wala hakuna Uzi jamani

Kama una Uzi naomba. Link nisome
 
Lisu meno yote nje kwa furaha ndege za Tanzania zikikamatwa!
Watanzania tudai kodi tuliyotumia kumsomesha Lisu hana faida yoyote kwa taifa.

Kama ndege hazikupigwa mnada enzi ya Magufuli hazitapigwa mnada tena
Kwanini usidai pesa zilizotumika kuwasomesha viongozi wako wanaoingia mikataba ya kifisadi inayoligharimu taifa?

Kwako wewe anayecheka baada ya ndege kushikiliwa ni mbaya zaidi ya aliyeingia mkataba uliosababisha ndege kuzuiliwa?

Una shida kichwani.
 
Ngoja aje bwana Mayalla
Tundu Lissu amesema mali isipokombolewa baada ya kuzuiliwa, itapigwa mnada ili kufidia deni linalodaiwa. Kwa muda gani, inatagemea mkataba Serikali uliongia.

Tundu Lissu alikuwa anajibu swali la mdau aliuliza nini kitatokea kama Serikali itashindwa kulipa deni lililopelekea ndege kukamatwa.
 
Kwa Hiyo!

Ndege yetu inatelekezwa ili kampuni MPYA ya wajanja ifanye kazi sio!?

Tunasubiri kama itatelekezwa!
Kampuni ya wajanja ndio ipi? laumu culture ya 10% , kutofuata sheria na kuingia mikataba isiyoeleweka, sasa kila mtu analipa, tumekomeshwa kuanzia kwenye dhahabu, gas, Bandari etc hakuna cha ajabu hapo acha wachukue tuu labda tutapata akili ya kuwaondoa CCM
 
Tundu Lissu amesema mali isipokombolewa baada ya kuzuiliwa, itapigwa mnada ili kufidia deni linalodaiwa. Kwa muda gani, inatagemea mkataba Serikali uliongia.

Tundu Lissu alikuwa anajibu swali la mdau aliuliza nini kitatokea kama Serikali itashindwa kulipa deni lililopelekea ndege kukamatwa.
Nasubiri yale mapoyoyo ya ccm mwashambwa na Etwege yaje huku JF
 
Back
Top Bottom