Tundu Lissu: Madaktari hawakupaswa kufukuzwa kabla ya kujitetea kwa mujibu wa sheria

Simba mnyama

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
348
129
Mbunge machachari, msema ukweli na muwazi, mheshimiwa Tundu Lissu amesema bungeni jioni hii kuwa madaktari hwakupaswa kufukuzwa bila kuwapa nafasi ya kujitetea kama inasema sheria. Huu ni uonevu mkubwa. Aidha Lissu ameponda kitendo cha kufukuza madaktari hao ambao wamesomeshwa kwa kiasi kikubwa kabisa cha pesa za walipa kodi wa nchi hii na matokeo yake baadhi yao wamekimbia na kwenda nchi nyingine ambako wanalipwa vizuri. Mbunge huyu amesema kuwa inabidi serikali ibadilike na iwalipe vizuri ili kuwafanye madaktari kufanya kazi hapa nchini.

Aidha, Mheshimiwa Tundu ameponda kufungiwa gazeti la Mwanahalisi ambalo kabla ya kuandika chochote hufanya kwanza utafiti. Sauti ya watanzania ni kama imefungwa.
 
Hiyo ndo Tanzania yetu..

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Tundu Lissu mzee wakuwekewa posho kwenye account yake bila mwenyewe kupenda.
 
Hii thread inahusu mchango wa Lissu dhidi ya kufukuzwa madaktari. Wadau seniors kama wewe ni vema mkasaidia hili jukwaa likarudi kwenye mstaari unaoeleweka badala ya kujikita kwenye personal vandetta. Uliona shida gani kujadili sakata la madaktari badala ya mfumo unatumika kulipa posho kwenye account ya Lissu?
 
Mbunge machachari, msema ukweli na muwazi, mheshimiwa Tundu Lissu amesema bungeni jioni hii kuwa madaktari hwakupaswa kufukuzwa bila kuwapa nafasi ya kujitetea kama inasema sheria. Huu ni uonevu mkubwa. Aidha Lissu ameponda kitendo cha kufukuza madaktari hao ambao wamesomeshwa kwa kiasi kikubwa kabisa cha pesa za walipa kodi wa nchi hii na matokeo yake baadhi yao wamekimbia na kwenda nchi nyingine ambako wanalipwa vizuri. Mbunge huyu amesema kuwa inabidi serikali ibadilike na iwalipe vizuri ili kuwafanye madaktari kufanya kazi hapa nchini.

Aidha, Mheshimiwa Tundu ameponda kufungiwa gazeti la Mwanahalisi ambalo kabla ya kuandika chochote hufanya kwanza utafiti. Sauti ya watanzania ni kama imefungwa.

Tunashughulikia suala la Mgomo wa waalimu kwa sasa. Hilo la madaktari tulishalimaliza. Tunajipanga kuwafukuza waalimu kwa style ileile ya madaktari baada ya kummapwepande kiongozi wao. Bado tunachukua data!
 
Tundu Lissu mzee wakuwekewa posho kwenye account yake bila mwenyewe kupenda.

Wewe ni miongoni mwa watu ambao siku nchi hii tukiikomboa utakuwa mkimbizi.Wewe endelea ipo siku hawa mabwana zako watakuoa
 
Tundu Lissu sasa anataka kujiaibisha. Aliyemwambia kuwa madaktari hawajapewa fursa ya kujieleza ni nani?

huwa anakurupuka huyu jamaa sijui kama huwa anathink big, watu wameamua kusema liwalo na liwe yeye anasema hawakupewa nafasi ya kujitetea au kujieza walipewa ila haohao wakina tundu ndio wamewaponza madaktari saizi anajaribu kujisafisha kwa aliowaponza
 
uwe na aibu ndugu yangu.
 
Wajitetee vp wakati mahakama ilisema mgomo ni batili? Hata kama wakisema wale madaktari bingwa waligoma so wasingeweza kufanya kazi bt wangeenda tu kazini wakae pale waonekane wako pale.. Wote wana makosa maana kwa serikali kwenda mahakamani hiyo pia walikosea
 
right to be heard?lissu anaseme hawakusikilizwa hao madaktari.?yani mwanasheria huyo anasahau kua madaktari were given not only right to be heard but also an adequate oportunity.kama anakumbuka Mwakyembe wakati anatoa report ya Richmond pia alilalamikiwa na Lowasa kua hakumpa nafasi ya kumsikiliza huku ofisi yake (lowasa)na mwakyembe ni karibu.lakini mwakyembe alimweleza kua alitaka apewe haki ya kusikilizwa ipi zaidi ya alichofanya.?sasa hao madaktari wasipotezwe na lisu kuanzisha hoja ya kua wamefukuzwa bila kusikilizwa.jamaa wamesikilizwa saana.
 
Back
Top Bottom