Tundu Lissu Live from George Washington University

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
Jun 26, 2014
545
684


Lissu azungumza George Washington University, Chama cha Republican na Human Rights Watch Washington D.C.

Human Rights Watch wamemuuliza Mh. Lissu “Are you planning to run 2020”? Lissu: “ I didn’t take sixteen bullets for nothing”

Mh. Lissu amekuwa na majadiliano ya kina juu ya changamoto za demokrasia nchini Tanzania. Walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali walio hudhuria mazungumzo haya waliweza kumsikiliza Mh. Lissu akielezea mwenendo wa demokrasia Tanzania na namna alivyo shambuliwa kwa risasi Dodoma, Tanzania.

Majadiliano yalikuwa mapana huku wahudhuriaji wakionyesha ufahamu mkubwa juu ya kinacho endelea Tanzania. Walimu na wanafunzi wameonyesha kuelewa juu ya matukio yaliyo tokea Kibiti, na jinsi demokrasia inavyo kamdamizwa Tanzania.

Pia, Mh. Lissu ameelezea namna sheria ya uchochezi inavyo tumika kuwafungulia mashtaka wana siasa wa upande mwigine wa siasa. Zaidi katika maongezi haya Mh. Lissu ameongelea sheria ya mitandao jinsi inavyo kandamiza Uhuru wa Mtanzania aliokua nao siku zilizo pita.

Leo vilevile, Mh. Lissu amezungumza na Human Righs Watch. Mada ya mazungumzo ilikua ni Haki za Binadamu, watoto wa kike mashuleni na mazingira ya Mh. Lissu alivyo pigwa risasi. Vile vile, wamejadili suala la kuondolewa kwa Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania na uhusiano wa siasa za Tanzania.

Katika majadiliano hayo, Human Rights Watch wamemuuliza Mh. Lissu swali lifuatalo: “Are you planning to run 2020”? Mh. Lissu alijibu: “ I didn’t take sixteen bullets for nothing”

Kikao kilicho fuata alikutana na Chama Cha Republican (International Republican Institute). Masuala yaliyojadiliwa ni yafuatayo; jinsi Rais Magufuli anavyo tumia nguvu zake za kiutawala kushawishi viongozi wakuu wa Bunge upande wa chama tawala.

Vilevile wamekadili jinsi watuhumiwa wanao wekwa ndani bila ya kufikishwa mahakamani. Baadhi ya watuhumiwa walio ongelewa katika majadiliano hayo ni Mashekhe wa Uamsho, Mh. Mbowe, Mh. Matiko na watanzania wenye mashtaka ya kimtandao. Kikubwa zaidi, wamezungumzia sheria Mpya ya vyama vya siasa iliyo pitishwa wiki jana.

Kesho, Mh. Lissu ataendelea na ziara kwa kukutana na viongozi wa juu wa wizara ya mambo ya nje (Department of State)-Deputy Assistant Secretary, Sauti Ya America (Voice of America- Shaka - Straight Talk Africa)

george.PNG

Mh. Lissu akita George Washington University- Washington D.C.- USA​
 
Last edited:
Tanzania's Democratic Challenge: A Conversation with Opposition Leader Tundu Lissu

Description
Please join the Elliott School Institute for African Studies for a conversation with Tanzanian Opposition Leader and chief whip Tundu Lissu.

Once heralded as a peaceful and generally democratic U.S.-partner in East Africa, Tanzania has seen a decline in civil liberties and human rights in recent years. The country has seen attacks on journalists and opposition activists, a raft of restrictive laws, and allegations of politically motivated killings and disappearances.

Mr. Lissu, chief whip in Parliament for opposition party Chadema and a vocal critic of government corruption, was gunned down in his driveway after returning home for a parliamentary session in 2017, shot 16 times by machine-gun wielding assailants. He has been recovering in Belgium since the attack but is determined to return to Tanzania to champion democracy and civil liberties.
Jennifer Cooke, IAfS director, will moderate the conversation.
 
Back
Top Bottom