Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
1. Wapo wanaoshangilia pesa imepungua kwa waume na wanarudi mapema nyumbani , ikimaanisha wanafika nyumbani mapema.
## ila Baadaya muda mfupi tu hao hao wanalalamika mzunguko wa pesa mdogo hakuna pesa ya kusomesha watoto wanaoingia kidato cha tano, madawa bei ghali wamama wanakufa hospitalini.
2 .Haijakaa sawa unasikia mwingine anashangilia makampuni yadaiwa kodi kuliko faida yanayopata, kwa sababu ya uzuri au mwonekano wa ofisi zao, na yakishindwa kulipa kodi Makampuni hayo, wanajaribu kupunguza wafanyakazi kujaribu kuboresha huduma na kubana matumizi,
## Yule aliyekuwa anashangilia anapunguzwa kazi na hapo analalamika ajira ngumu, kila akizunguka kampuni zingine hivyo hivyo zinapunguza wafanyakazi huku zingine zikifungwa.
3 . pia mtu mwingine anashangilia wapinzani wamebanwa bungeni ndani na nje akisubiriwa kwa hamu akamatwe na vyombo vya Dola, ikiwepo vyombo vya habari kutishiwa kufungiwa wakitoa taarifa za mikutano yao,
## baadaye kidogo mtu ananyimwa mafao anakimbilia kwa wapinzani akiomba atetewe bungeni na hapo hapo akidai uhuru wa habari na kuwe na demokrasia kwa wapinzani.
**** Hizo ni baadhi ya changamoto za sasa katika Afrika. Ila tukumbuke upepo wa mageuzi hauzuiwi kwa vitisho.***