Tundu Lissu: Legacy ya hayati Magufuli imeanza kusambaratika,uchunguzi usiishie TPA na ATCL

Lissu anadhani Magufuli alikuwa malaika? hebu atuambie ni Rais yupi ambaye wakati wake akiongoza hapakuwa na kasoro kwenye utendaji wake.

Naona ameshasahau Katiba Mpya, wenzie wamkumbushe, Magufuli is no more.

Madudu yalikuwepo toka enzi za Mkapa, akaja Kikwete, na Magufuli akafanya kwa kiasi chake mpaka pale alipoishia, vyema atafute ajenda nyingine kabla 2025 haijakaribia.
Ni hatari sana kuwa na Rais mwizi halafu mkali. Ukimsema anakuua, anakuteka, anakutesa! Jk ndiyo kulikuwepo na madudu lakini alikuwa mstaarabu sana na aliyafanyia kazi. Mkapa hivyo hivyo lakini huyu marehemu dah! alibagua majizi ya kushughulikia! na aliua wanaomsema!
Siyo vyema kumsema marehemu lakini nashindwa kujizuia kusema "Rot in Hell" Magufuli
 
Lissu anadhani Magufuli alikuwa malaika? hebu atuambie ni Rais yupi ambaye wakati wake akiongoza hapakuwa na kasoro kwenye utendaji wake.

Naona ameshasahau Katiba Mpya, wenzie wamkumbushe, Magufuli is no more.

Madudu yalikuwepo toka enzi za Mkapa, akaja Kikwete, na Magufuli akafanya kwa kiasi chake mpaka pale alipoishia, vyema atafute ajenda nyingine kabla 2025 haijakaribia.
Angalau wale wengine wote hawakujaribu kutuaminisha kwamba wao ni "masuper men"; kwamba wanayo magic wand au muarobaini wa matatizo yote ya taifa hili kama mwendazake huyu aliyepita. they governed like normal human beings not super humans or demi Gods unlike the immediate past president
 
Kupitia ukurasa wake wa Twita ndugu Tundu Lissu amedai kuwa sasa kuwa kile watanzania wengi walidhani watarithi mambo mazuri yaliyoachwa na JPM ni kama hakuna. Maana mengi yana uozo na yameanza kusambaratika. Kama uchunguzi ukifanyika mengi sana yataibuka.

Muulizeni hiyo ripoti iliandikwa baada ya Magufuli kufariki siku chahce zilizopita?

Ni nani aliagiza kufanya ukaguzi kwenye hayo mashirika na Magufuli au Samia?

Wakati matumizi na ubadhirifu huo ulioibuliwa ijapokuwa sio kwa kiwango cha uhalisia (mengi makaguzi hajabaini) je Samia hakuwepo?

Ni wazi Mh Samia analekezwa kucheza mdundo la TAL ili akamilishe kazi aliyokabidhiwa kunyong'onyeza utawala uliopo.

Mh Samia hawezi kukwepa kwa chochote kile kutokana na matokeo ya ripoti maana ndiye alikuwa mshauri mkuu wa hayati kwa hiyo hapo miluzi tayari iko kazini kutengeneza taharuki.

Inasemekana kuna vyama vya siasa vina hati mbaya kwa mjibu wa ripoti hiyo viwili ni vikubwa ni vipi?

Kinachobadilika hapo ni maumbile tu lakini hatua ni zilezile ila zilizolaini kiasi kwamba zitajenga usugu hatimaye mh Samia kuzungukwa kwa urahisi kabisa.
 
Huyu nae atulie huko aache kulaumu laumu,Rais hakua malaika saaana asikosee
Ungetufahamisha Kifungu gani cha Katiba au sheria ya nchi Kahalifu ingekuwa vyema zaidi, na ningekupongeza na kusaidia kumshitaki ili sheria imshughulikie!
 
Yaani Lisu aache ajira arudi TZ kwani hana akili. Akirudi kwa ndoto zake ni kuingia Ikulu less than that ataendelea na ajira yake akitegemea kuna siku sheria ya madini itabadilishwa makanikia yasafirishwe nje kwa waajiri wake
Niliwahi msikiliza Mwandishi habari mkongwe bw. Richard Mgamba akisikitika kwa nini 'fighter mwenzake dhidi ya wenye migodi ghafla aligeuka na kuwa mtetezi wao? Hiyo ilinipa picha kwamba Lissu ni mtu wa bei nafuu sana! ni mtu anayenunulika kwa ushenzi tu, huku wengine wakimuita shujaa.
 
Huyu nae atulie huko aache kulaumu laumu,Rais hakua malaika saaana asikosee
Leo ndo mnaona alikuwa malaika kidogo eti ilhali miaka yote 5 mmekuwa mkimwimbia mapambio ya kusifu na kumwabudu as if ni fulu malaika. Hadi mnafikia hatua ya kukufuru eti mambo aliyoyafanya hata Yesu Wala Mtume hawakuwahi kufanya hapa duniani kweli!
Eti awe Rais wa milele maana hakuna mwingine badala yake chezea MUNGU wewe badala yake amekuwa Rais wa kwanza kutawala kwa muda mfupi kuliko wote Hadi Sasa.
 
Na nyie mlizidi kumsifia marehemu! Alipoingia madarakani aliwakosoa sana watangulizi wake, alidhani wao walikuwa malaika!?
Methali "Ivumayo haidumu...!" "Mgema akisifiwa..."
Falsafa: Apandae ngazi kwa kasi huporomoka kwa kishindo!!"
 
Kupitia ukurasa wake wa Twita ndugu Tundu Lissu amedai kuwa sasa kuwa kile watanzania wengi walidhani watarithi mambo mazuri yaliyoachwa na JPM ni kama hakuna. Maana mengi yana uozo na yameanza kusambaratika. Kama uchunguzi ukifanyika mengi sana yataibuka.

Utopolo tupu hapo mwambieni yeye aendelee kuhangaika na kazi yake aliyoteuliwa ya Ubalozi wa Mashoga ya Afrika ya Kusini. Tanzania hataweza wameshamdiss siku nyingi. Mwambie aje aone legacy zilizoachwa na Jemedari Magufuli nchi nzima.
 
Niliwahi msikiliza Mwandishi habari mkongwe bw. Richard Mgamba akisikitika kwa nini 'fighter mwenzake dhidi ya wenye migodi ghafla aligeuka na kuwa mtetezi wao? Hiyo ilinipa picha kwamba Lissu ni mtu wa bei nafuu sana! ni mtu anayenunulika kwa ushenzi tu, huku wengine wakimuita shujaa.

Wanaomwita Bwana Lissu kuwa ni shujaa ni wale "nyumbu" ambao maafisa wa wanyama pori wanawaita "no brain". Haiwezekani mtu abadilike degree 180 aache kutetea usafirishwaji wa makanikia na aanze kwa nguvu kubwa na kasi kubwa zaidi aanze kulazimisha na kutetea usafirishwaji ule ule aliopinga mwanzoni halafu mtu aendelee kusema kuwa Lisu ni yule yule. Lazima uwe nyumbu kama huoni jinsi alivyobadilika.
 
Magufuli the late, alijenga kwenye msingi mbovu ulioachwa na Mkapa. Period.

Na hili jinamizi litaendelea kuitafuna Tanzania mpaka tukubali kuwa na katiba mpya
 
Back
Top Bottom