Tundu Lissu: Legacy ya hayati Magufuli imeanza kusambaratika,uchunguzi usiishie TPA na ATCL

Mimi nilisimamia ukweli bila kupotezwa na propaganda mfu za awamu ya Magu. Na kama huyu mama ataamua kweli kusimamia ukweli bila kuchengesha, utajua misimamo yetu dhabiti dhidi ya utawala katili uliopita, tulikuwa sahihi kwenye mambo mengi. Tunaposema Mungu ameamua kufanya mabadiliko ya kweli bila kumwaga damu hatukosei.
Hawa MATAGA walidhani kila aliyekuwa akimkosoa Magua alikuwa ana issue naye binafsi. Magu alikuwa kiongozi mkandamizaji sana na mbaguzi hilo lipo wazi
 
Mbowe anaendelea kuwa mwenyekiti wa cdm. Tunza hii post yangu kwa ajili ya uchakataji huko mbeleni, na ni nani alipeleka wanawake wa covid19 huko bungeni kinyemela.
Phew, sasa kama ni hivyo, huko CHADEMA atakuwa amebaki nani hasa, kama hata Mbowe atakuwa ni pandikizi la CCM?

Halima na Ester Matiko, sikuamini wawe kama walivyogeuka kuwa..., yaani hadi sasa sielewi mchezo huu ulikwenda vipi!

Lakini itashangaza sana kama Mbowe atakuwa ni sehemu ya mchezo huo..., kwa manufaa yapi kwa chama?; au kwake binafsi?
 
Magufuli alisema amemaliza ufisadi, na hiyo ilikuwa ni sehemu ya yeye kunajisi uchaguzi maana kamaliza wizi. Sasa ukisema wanajua tatizo ni Magufuli unamaanisha nini?
Wapi alisema amemaliza ufisadi au rushwa,nenda YouTube usikilize maneno yake 2020 alipokuwa akizindua bunge, alisema tutaendelea kupiga vita vitendo vya ufisadi/rushwa kwa nguvu zetu zote,wewe kauli hiyo ya kumaliza rushwa na ufisadi aliisema lini?acha porojo hii ni serikali ya ccm,na Samia alisema ataendeleza yote yalioachwa na Magufuri 😁😁😄
 
Muda umefika wa Lissu kupambana na ‘post traumatic stress disorder’.

Asichukulie poa akiacha hiyo condition ita develop into other serious forms of stress and mental disorders.
 
Mara umesahau? Vipi ukubwa wa ubongo wako! Lissu aligombea kuwa rais miezi minne iliyopita! Utasemaje hajawahi kuwa na ndoto za kuwa rais? Sasa wewe utaaminika tena mbele za watu? Au ulikuwa umezirai kipindi hicho?
Tumia akili yako vizuri.

Kwa mwaka jana hakuna mtu CHADEMA ambaye angeweza kuwa na mvuto na kupambana kwenye urais kama Tundu Lissu.

Ilibidi, kubidi haimaanishi ana ndoto hiyo.

Mimi ndoto yangu ilikuwa kuwa rubani lakini ikabidi niwe mwalimu.
 
Kupitia ukurasa wake wa Twita ndugu Tundu Lissu amedai kuwa sasa kuwa kile watanzanianwengi walidhani watarithi mambo mazuri yaliyoachwa na JPM ni kama hakuna. Maana mengi yana uozo na yameanza kusambaratika. Kama uchunguzi ukifanyika mengi sana yataibuka.

JF mngekuwa Watanzania mngemfungia huyu mppuzi ambaye kazi yake ni kuwakoroga watanzania kwa maslahi ya ma-gays wake,, tunataka mani na maendeleo maraisi wote waliopita Tanzania hawakufanikiwa kupata pesa za kuifanya miradi hiyo ambayo ni kinyume na matakwa ya gays,,, Gays hawataki sisi waafrika tuwe na umeme mpaka vijijini wala tuwe na miundombinu ya kisasa kama reli mabarabara na mifumo ya maji safi na salama ili waendelee kutunyonya na Lissu akiwa wakili wao akipata 10% Gays wanataka kutuchimbia visima vijijini akidai wanatusaidia kumbe kutuchelewesha,,Umeme, Maji, Elimu na miundombinu ya usafir na usafirishaji Gays hawataki tuwe navyo bora na kwa kuwepo kwa kina Lissu na Zitto Gays watafanikiwa hivyo tuwakataeni vikali sana watu hawa wawili,,, Lissu anataka kutuambia ati Magu kanufaika kwenye hii miradi ya kimkakati MUONGO mkubwa
 
Lissu anadhani Magufuli alikuwa malaika? hebu atuambie ni Rais yupi ambaye wakati wake akiongoza hapakuwa na kasoro kwenye utendaji wake.

Naona ameshasahau Katiba Mpya, wenzie wamkumbushe, Magufuli is no more.

Madudu yalikuwepo toka enzi za Mkapa, akaja Kikwete, na Magufuli akafanya kwa kiasi chake mpaka pale alipoishia, vyema atafute ajenda nyingine kabla 2025 haijakaribia.
Hivi hii hasara ya mabilioni ya uendeshaji wa shirika la ndege,Hayati Magufuli angekuwepo ingesemwa hadharani hata wewe na mimi tukajua?
 
Dreamliner moja iliyopaki ni sawa na matreka elf 10 mapya na vifaa vyake tena kwa cash, Kama ni kwa mkopo unapata trekta elf 50 za horse power 75.Trekta moja ulima heka 25 kwa siku kwa speed ya kivivu. Trekta moja utoa ajira kwa vijana 100.
So badala ya dreamliner moja iliyopaki kutoa ajira kwa watu 30 zingekuwa ni trekta zingetoa ajira milioni 5 za moja kwa moja achilia wategemezi wao.Ajira zote zilizonunulia ndege zingenunua trekta laki moja ambazo zingetoa ajira milioni 12 nchi nzima.Ndege ugusa wachache,kilimo ugusa wote.Kama Malaysia waliwekeza kwenye michikichi tu ndo wanailisha dunia mafuta ya kula na bado awajalijaza soko. Soko la mazao ya kilimo duniani ni kubwa hata KILA mtu alime tza hatutoweza kulijaza.Hela zilizotupwa kwenye ndege tilioni moja tungepata matreka laki 2 yangeajiri vijana milioni 12 zingemaliza tatizo la ajira nchini kwa kuwekeza kwenye kilimo mkakati na zingesharudi ndani ya miaka 3 tungepata pesa tosha za kigeni kukamilisha miradi yote bila kutegemea kukopa.Kupitia kilimo tu tungekuwa uchumi wa kati.Kama wakoloni wao waliweza maliza tatizo la ajira nchini why tunashindwa?Tangu Uhuru bado atujapata kiongozi sahihi mwenye uchungu anaeguswa na ugumu wa maisha ya watz,zaidi ya kuyafanya maisha yazidi kuwa magumu.Kwann watumishi wasipewe misamaha ya Kodi Ili wajinunulie magari binafsi kuliko kuwa na utitiri wa magari ya serikali ambayo hayazalishi,hayana faida ni hasara kwa mlipa Kodi V8 moja tu ni sawa na matrekta 10 mapya na jembe zake hapo ni sawa na ajira elf 1.
Tuendelee tu kuwalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwetu aliyetupa Mali alitunyima akili. Chagua ccm chagua maendeleo chagua mitano tena ikiisha mitano tena jiandae kwa kumi tena.
Wewe acha ujinga nenda vijijini huko trecta azina soko baada ya msimu wa kilimo kuisha,matrecta yanabaki kusomba maji tu, wakati msimu wa kilimo eka moja wanalima kwa elfu 20,000)tu sasa hayo yote yakipelekwa huko vijijini yatafanya kazi gani? wakati yaliopo hayana kazi ya kufanya, ndio maana Magufuri alikuwa anakazania tujenge viwanda kwanza ili tuweze kusindika mazao yetu.Kilimo akina tija kama una masoko mkuu
 
Wewe acha ujinga nenda vijijini huko trecta azina soko baada ya msimu wa kilimo kuisha,matrecta yanabaki kusomba maji tu, wakati msimu wa kilimo eka moja wanalima kwa elfu 20,000)tu sasa hayo yote yakipelekwa huko vijijini yatafanya kazi gani? wakati yaliopo hayana kazi ya kufanya, ndio maana Magufuri alikuwa anakazania tujenge viwanda kwanza ili tuweze kusindika mazao yetu.Kilimo akina tija kama una masoko mkuu
Ulitaka lifanye Kazi ipi zaidi ya kilimo.
 
Alikubali lini kuwa kashindwa urais? Kila siku anadai alishinda.

Washirika wake mpaka wakapeleka malalamiko yao huko Uholanzi kuwa wameibiwa kura!
Kukimbia nchi ni kukubali tosha regardless anasema nini.

Hoja za ubadhirifu ATCL na TPA chini ya Magufuli hazijajibiwa bado.
 
Hunifahamu, leo ndio nasimama kwa ajili ya marehemu, sikuwahi kumtetea mwanzo nilikuwa na Lissu, mpaka nilivyogundua Lissu ana tatizo la ubongo ndio nimemuacha akatibiwe kwanza.
Tujadili hoja zaidi kuliko watu.

Hata watu wenye matatizo ya ubongo wanaweza kutoa hoja nzuri mara mojamoja.

Na watu unaowaheshimu wakakosea.

Waingereza wanasema hata saa iliyosimama huwa inakuwa sawa angalau mara moja kila siku.
 
Back
Top Bottom