Tundu Lissu: Legacy ya hayati Magufuli imeanza kusambaratika,uchunguzi usiishie TPA na ATCL

Tena kwa kutumia vyombo vya habari hasa magazeti, kwasababu magazeti kipindi kile yalikuwa huru na hivyo kuwawezesha kufanya utafiti wa hali ya juu bila hata restrictions zozote zile.

Nakumbuka magazeti kama, Mwanahalisi, Mawio, Mseto, Freemedia n.k
Madudu ya akina Mkapa yalikuwa yanawekwa wazi, tofauti na tulivyoamishwana miaka hii mitano.
 
Pitia post yangu uliyoniquote kama nimemtaja Lisu popote, ni aidha umepanick au unajishuku. Kuhusu Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti zaidi ya miaka 15, suala sio kuwa matured maana alikuwa hagombei na Lisu.

Hilo la kwamba Lisu ni mwanaharakati ni tafsiri ya huko ccm, na hii tulilisikia hata Slaa alipokuwa mwiba kwa ccm kuwa ni mwanaharakati. Alipotoka cdm akawa anamwagiwa sifa kuwa alikuwa mpinzani wa kweli! Linapokuja suala la busara sioni kama ni tatizo, maana kama Magufuli alikuwa hana busara na Kawa rais, sijui utaniambia nini. Hakuna anayemfikia Mbowe? Au ni kwakuwa huwa anawakubalia ccm porojo zao kirahisi? Nasema hivi, unafiki huwa una mwisho wake. Ww tapika propaganda zako mfu za ccm lakini nimekufahamu vizuri, hutaki kunywa sumu ufe fullstop.
Sasa mimi na wewe alie panic nani?usikimbie, usininunie, kadi ya CCM ulinipa lini? unaamini speculations zako unataka nizikubali? wacha utoto.

Call it propaganda or anything, I repeat, this is my personal decision, Lissu kwangu sio mwanasiasa ukubali ukatae.

Mmemjaza amekuwa na kichwa kikubwa hasikii tena anachoambiwa, anajidanganya ana wafuasi wakati wakihitajika rodi hawatokei, now amebaki kuandika tu twitter, anatakiwa ajifunze kwa kina Bobi Wine.

Halafu huyo Mbowe huko Chadema huwa hajiweki mbona mgumu sana kuelewa hili? huwa anapigiwa kura yule, najua Lissu ni kipenzi chako ukubali/ukatae.

Lissu ndio alikufanya ukaenda kupiga kura, bila yeye kugombea usingepiga kura, ulisema mwenyewe maneno haya usiwe mnafiki, ndio maana hii move yangu imekuuma hadi unaropoka maneno ya ajabu ajabu coz nimegusa kipenzi chako unataka kulia, au sijui umeshaanza kulia!. pole.

Then again, sijui Mbowe amekubali porojo gani za CCM, unapenda kuendeshwa kwa mihemko ya Lissu ndio maana, yule Mbowe busara iko pale.

This is politics, kama ulikuwa huijui ndio uijue sasa, and above all, this is democracy sio lazima tufanane kila kitu kila wakati, ukipenda kuendelea ku-shout the choice is yours dude, take a glass of water and get on with your life, usijitese.

Now kama Mbowe hafai ukaambiwa sema unataka nani awe mwenyekiti lakini hukuwahi kujibu hili swali, mpaka leo bado umekariri tu Mbowe hafai, mbadala huna!
 
Kupitia ukurasa wake wa Twita ndugu Tundu Lissu amedai kuwa sasa kuwa kile watanzanianwengi walidhani watarithi mambo mazuri yaliyoachwa na JPM ni kama hakuna. Maana mengi yana uozo na yameanza kusambaratika. Kama uchunguzi ukifanyika mengi sana yataibuka.


Anatuchezea akili lisu ,sababu ya marehemu magu kutumbuka kila mala ni upigaji kama huo unataka kutuaminisha kwamba angekuwepo asingetumbua watu leo , ebu mpe heshima magu kafanya mengi makubwa
 
Kupitia ukurasa wake wa Twita ndugu Tundu Lissu amedai kuwa sasa kuwa kile watanzanianwengi walidhani watarithi mambo mazuri yaliyoachwa na JPM ni kama hakuna. Maana mengi yana uozo na yameanza kusambaratika. Kama uchunguzi ukifanyika mengi sana yataibuka.


Legacy yake imeisha vip? Kwa sababu ya hizo issue mbili ambazo hazina lolote jipya?
 
Alikubali lini kuwa kashindwa urais? Kila siku anadai alishinda.

Washirika wake mpaka wakapeleka malalamiko yao huko Uholanzi kuwa wameibiwa kura!
Wewe kimekuuma nini mpaka useme hawezi kuwa rais?, tatizo mnajiona mko sawa na Mungu, na Mungu hatakubali kuwa sawa na binadamu aliowaumba yeye mwenyewe.
 
Wapi alisema amemaliza ufisadi au rushwa,nenda YouTube usikilize maneno yake 2020 alipokuwa akizindua bunge, alisema tutaendelea kupiga vita vitendo vya ufisadi/rushwa kwa nguvu zetu zote,wewe kauli hiyo ya kumaliza rushwa na ufisadi aliisema lini?acha porojo hii ni serikali ya ccm,na Samia alisema ataendeleza yote yalioachwa na Magufuri
Amechoka akili huyo muache apumzike.
 
Imeanza kusambaratika.

I thought everything must survive the test of time before people can make a conclusion?
Mwinyi alisema ila akaja kupata sifa zake baadae. Mkapa hivyo hivyo. Hata JK pia.
TL ana shida zake binafsi na JPM. Ndio maana angependa kuona hivyo ingawa sidhani kama itakuwa hivyo.
Tukumbuke aliyeshikwa na ngozi ndio amekula nyama. Hawa wajinga wengine hawana kinga yoyote, halafu wanaiba wakidhani wataogopwa wanachekesha sana. Tena ikithibitika waadhibiwe vitali. Iwe fundisho
 
Tujadili hoja zaidi kuliko watu.

Hata watu wenye matatizo ya ubongo wanaweza kutoa hoja nzuri mara mojamoja.

Na watu unaowaheshimu wakakosea.

Waingereza wanasema hata saa iliyosimama huwa inakuwa sawa angalau mara moja kila siku.
Nimekuelewa, nina sababu yangu nje ya siasa inayonifanya kufanya hiki ninachokifanya hapa, nivumilie tu kwa wakati huu.
 
Lissu atambue kwamba hakuna miradi ya Magufuli labda Kama anamaanisha miradi ya nyumbani kwake Magufuli pale alipozikwa
 
I thought everything must survive the test of time before people can make a conclusion?
Mwinyi alisema ila akaja kupata sifa zake baadae. Mkapa hivyo hivyo. Hata JK pia.
TL ana shida zake binafsi na JPM. Ndio maana angependa kuona hivyo ingawa sidhani kama itakuwa hivyo.
Tukumbuke aliyeshikwa na ngozi ndio amekula nyama. Hawa wajinga wengine hawana kinga yoyote, halafu wanaiba wakidhani wataogopwa wanachekesha sana. Tena ikithibitika waadhibiwe vitali. Iwe fundisho
Unataka kuambiwa nini kujua Atcl imefeli? Ipate hasara miaka kumi?
 
Lissu anadhani Magufuli alikuwa malaika? hebu atuambie ni Rais yupi ambaye wakati wake akiongoza hapakuwa na kasoro kwenye utendaji wake.

Naona ameshasahau Katiba Mpya, wenzie wamkumbushe, Magufuli is no more.

Madudu yalikuwepo toka enzi za Mkapa, akaja Kikwete, na Magufuli akafanya kwa kiasi chake mpaka pale alipoishia, vyema atafute ajenda nyingine kabla 2025 haijakaribia.
Mataga mmepatwa kisawasawa
 
Alikubali lini kuwa kashindwa urais? Kila siku anadai alishinda.

Washirika wake mpaka wakapeleka malalamiko yao huko Uholanzi kuwa wameibiwa kura!
Wafiwa acheni nongwa, malizeni matanga kwanza ndo mje kumwaga mapovu yenu JF.
 
Phew, sasa kama ni hivyo, huko CHADEMA atakuwa amebaki nani hasa, kama hata Mbowe atakuwa ni pandikizi la CCM?

Halima na Ester Matiko, sikuamini wawe kama walivyogeuka kuwa..., yaani hadi sasa sielewi mchezo huu ulikwenda vipi!

Lakini itashangaza sana kama Mbowe atakuwa ni sehemu ya mchezo huo..., kwa manufaa yapi kwa chama?; au kwake binafsi?

Mkuu sijakuambia tunza hii post kwa bahati mbaya. Tutaichakata vyema hapo baadae.
 
Wapi alisema amemaliza ufisadi au rushwa,nenda YouTube usikilize maneno yake 2020 alipokuwa akizindua bunge, alisema tutaendelea kupiga vita vitendo vya ufisadi/rushwa kwa nguvu zetu zote,wewe kauli hiyo ya kumaliza rushwa na ufisadi aliisema lini?acha porojo hii ni serikali ya ccm,na Samia alisema ataendeleza yote yalioachwa na Magufuri 😁😁😄
Kimsingi hakuwa na consistance kwenye kauli zake, ila kuwa kamaliza ufisadi hilo alikuwa halisemi mara moja, yeye au wapambe wake. Acha serikali ya ccm hata ingekuwa ya Republican hakuna anayejali, tunachojua Mungu kaamua kufanya mabadiliko bila kumwaga damu. Huyo Mama Samia aendeleze yale sahihi yaliyoachwa na mtangulizi wake hatuna tatizo na hilo maana hii ni Tanzania, yaani ni zaidi ya serikali ya ccm. Lakini sio kuteka na kuua wapinzani kisa anajenga daraja, sijui reli. Akienda kinyume na haki atafurahia show.
 
Back
Top Bottom