Tundu Lissu: Kwa wasiojua Magufuli sina shida naye, sina mpango wa kwenda ICC kumshtaki, pia alinichangia kipindi cha msiba wa mdogo wangu

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Katika kuyajibu maswali aliyoulizwa kuna sehem kaulizwa uhusiano wake na Magufuli nje ya siasa akasema haya

swali lililotangulia kwamba je ni kweli ana mpango wa kwenda ICC amejibu hapana na akasema si kwamba amesahau kwamba mahakama ya ICC haishughulikii kesi, bali kesi za aina hii haziendi huko hivo hana mpango wa kwenda huko,

Pili kwa wasiojua Magufuli nimesoma naye akiwa anasoma UDSM mi nikisoma Masters., amezoea kuniita mdogo wangu na mi namuita ni kaka yangu hivo ni kaka yangu,

Pia kipindi nimepata msiba wa mdogo wangu rais Magufuli alikuja baada ya kunipigia simu na kunipa mchango sitasema ni kiasi gani lakini ni heshima,
nilitumia robo saa nzima kuusema wema wake bungeni wakati wa hotuba yangu, lakin baada ya kuusema wema nikaanza kumshughulikia kama kazi yangu inavyopaswa,

Hivo sijawahi kuwa na shida na Magufuli kama Magufuli, ila Magufuli Rais ndo Tatizo

 
Kila mtu yuko bize kumjibu Lissu kuanzia Chama makao makuu, mpaka shina na serikali yote kwa ujumla.
50844766_2278981082391003_8208607404077016376_n.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni kichwa sio kilaza kama masisiem!

Sikiliza mahijiano yake na Maria Sarungi kupitia Kwanza tv ndio utajua ni jinsi gani anainga hii serikali kuhusiana na hili tukio.
Kipi kipya kakiongea hapo?? Anaendelea kulalamika tu upande wa serikali utafikir ndio waliomshambulia sjui mwanasheria wa nchi gani huyu !! Sasahv kaanza omba omba marekani!!! Chezea wabongo ww?? Mbowe mmemtelekeza Lupango baada ya kudanganywa kuhsu dhamana yake!!! Wala hamjishughulishi nae ila mmetumia mbinu nzuri mtamuondoa na lissu apate uenyekiti mara baada ya kuukosa ubunge 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kaanza kushituka kuwa approach aliyokuwa akitumia haijampa faida yoyote, he is loosing ground,

Tatizo kubwa la wapinzani ndilo hilo, kila jambo ni hisia tu, they never address issues.

Ukienda kwenye mikutano yao, kamwe hutaweza kujua nini malengo yao kwa watanzania pindi wakishika dola, utakachokisikia ni mazungumzo ya matukio ambayo ama yamepita au ndiyo yaliyopo ambayo kwa kifupi hizo sio sera na chama cha siasa ni kuuza sera sio kuuza versions za maneno kwa matukio mbali mbali.
 
Lissu anawatesa sana buku saba, kila mmoja anajaribu kuonyesha mchango wake kupambana na Lissu ili afikiriwe...
 
Akili zitamkaa sawa tu. Eti hana shida na Magufuli ila Magufuli Rais ndio tatizo...WTF is this!? Au hii ni kama vile kusema Watanzania tulio wengi hatuna shida na Tundu ila Tundu Mhaini ndio tatizo!
Uhaini ni kutaka kuipindua serikali iliopo madarakani bila shaka hujui unachokisema
 
Jamaa kaanza kushituka kuwa approach aliyokuwa akitumia haijampa faida yoyote, he is loosing ground,

Tatizo kubwa la wapinzani ndilo hilo, kila jambo ni hisia tu, they never address issues.

Ukienda kwenye mikutano yao, kamwe hutaweza kujua nini malengo yao kwa watanzania pindi wakishika dola, utakachokisikia ni mazungumzo ya matukio ambayo ama yamepita au ndiyo yaliyopo ambayo kwa kifupi hizo sio sera na chama cha siasa ni kuuza sera sio kuuza versions za maneno kwa matukio mbali mbali.
The fact is, Magufuli wanted him dead.
 
Back
Top Bottom