Tundu Lissu kwa sasa nyamaza,acha muda uongee

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,668
149,840
Ndugu yangu nakushauri kwa sasa unyamaze tu na wala usimjibu mtu yeyote kwani watakaokuelewa ni wachache kama ambavyo hukuelewaka miaka ile ya 90.

Uzuri hujaishia kukosoa tu bali umependekeza na nini cha kufanya ila wengi hilo hawalioni either kutokana na uelewa mdogo au ni makusudi tu.

Ndugu yangu,kwa utamaduni wa nchi yetu, kuwa na mtazamo tofauti na wakubwa ni kama kutenda mosa la jinai na jinai hiyo ndio ilikufanya upate shida miaka ile ya 90 ila ni bahati mbaya hatutaki kujifunza.

Ni kweli kabisa inawezekana viwango vya madini katika makinikia vikawa ni vikubwa kuliko ambavyo imekuwa ikiripotiwa lakini approach tuliyotumia ndio inaweza kutugharimu huko baadae kutokana na sheria na mikataba tulioingia lakini bila kusahau na sisi kama nchi tulikuwa na vyombo vyetu vilivyokuwa na jukumu la kusimamia maslahi ya nchi.

Kitu kingine cha kujiulia ni je,kama serikali yetu inavyodai kutokujua kama tulikuwa tunaibiwa,uongozi wa juu wa ACASIA nao hawawezi kujitetea kuwa walikuwa hawajui kama kuna wizi unafanyika kwani hilo jukumu waliwakabidhi waajiriwa wao kulisimamia kama ambavyo serikali ilivikabidhi vyombo vyake visimamie kwa niaba ya nchi?

Vile vile leo hii mnapomsikia Waziri Mkuu anaongelea swala kukaa na hawa mabwana kutatua tatizo hili, mnapaswa mjiulize imekuwaje leo hii wameona hiyo busara ya kufanya nao mazungumzo ili hali mwanzoni hawakufanya hivyo kabla ya kuchukua hatua walizochukua?

Isitoshe panapotokea mgogoro baina ya pande mbili tulipaswa kufanya nini na kama tungefuata taratibu kuna upande wowote ungelalamika kupata hasara?

Uzuri mambo ya kisheria na mahakamani kila mtu anayajua kwahiyo tusubiri wakati ufike..

Hivyo basi,maadam umeshaongea na maandishi yako yapo,nakushauri sasa ukae kimya na uache muda ndio utaongea.
 
Anaye muunga mkono huyu jaamaa apimwe akili kwanza

Ukweli wa hili suala ni kukiri kosa kwa wanaccm na kuweka mikataba wazi ili tujue nani ni adui yetu. Kuna watu walikuwa wanaunga mkono upuuzi wa mrahaba wa 3%, leo wanajifanya wazalendo. Nyie mmejitosa kutetea upuuzi na kumlaumu mtu aliyepiga kelele kuhusu wizi huu toka miaka ya 90. Sasa ndio mnaamka na uzalendo uchwara. Ni hivi wizi wa dhahiri mpaka sasa sio wa hiyo michanga bali ni katika huo mrahaba wa 3% kwani mpaka sasa ndio unatamalaki.
 
Lissu Aendelee kugawa dozi tu..
Wajinga ni wengi sana kwenye kile Chama..
Lolote wao wanagonga meza..
Dawa ni dozi, dozi, dozi.
 
Kwani hata akiongea anakukera??kama anakukera usimaikilize.. Tunaopenda kumsikia tutamsikiliza
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndugu yangu nakushauri kwa sasa unyamaze tu na wala usimjibu mtu yeyote kwani watakaokuelewa ni wachache kama ambavyo hukuelewaka miaka ile ya 90.

Uzuri hujaishia kukosoa tu bali umependekeza na nini cha kufanya ila wengi hilo hawalioni either kutokana na uelewa mdogo au ni makusudi tu.

Ndugu yangu,kwa utamaduni wa nchi yetu, kuwa na mtazamo tofauti na wakubwa ni kama kutenda mosa la jinai na jinai hiyo ndio ilikufanya upate shida miaka ile ya 90 ila ni bahati mbaya hatutaki kujifunza.

Ni kweli kabisa inawezekana viwango vya madini katika makinikia vikawa ni vikubwa kuliko ambavyo imekuwa ikiripotiwa lakini approach tuliyotumia ndio inaweza kutugharimu huko baadae kutokana na sheria na mikataba tulioingia lakini bila kusahau na sisi kama nchi tulikuwa na vyombo vyetu vilivyokuwa na jukumu la kusimamia maslahi ya nchi.

Kitu kingine cha kujiulia ni je,kama serikali yetu inavyodai kutokujua kama tulikuwa tunaibiwa,uongozi wa juu wa ACASIA nao hawawezi kujitetea kuwa walikuwa hawajui kama kuna wizi unafanyika kwani hilo jukumu waliwakabidhi waajiriwa wao kulisimamia kama ambavyo serikali ilivikabidhi vyombo vyake visimamie kwa niaba ya nchi?

Vile vile leo hii mnapomsikia Waziri Mkuu anaongelea swala kukaa na hawa mabwana kutatua tatizo hili, mnapaswa mjiulize imekuwaje leo hii wameona hiyo busara ya kufanya nao mazungumzo ili hali mwanzoni hawakufanya hivyo kabla ya kuchukua hatua walizochukua?

Isitoshe panapotokea mgogoro baina ya pande mbili tulipaswa kufanya nini na kama tungefuata taratibu kuna upande wowote ungelalamika kupata hasara?

Uzuri mambo ya kisheria na mahakamani kila mtu anayajua kwahiyo tusubiri wakati ufike..

Hivyo basi,maadam umeshaongea na maandishi yako yapo,nakushauri sasa ukae kimya na uache muda ndio utaongea.
Bila Lissu kuongea usingejua kama kuna muda. Shukuru umepata fulsa ya kutafakari na kuja na hoja.
 
Ukweli wa hili suala ni kukiri kosa kwa wanaccm na kuweka mikataba wazi ili tujue nani ni adui yetu. Kuna watu walikuwa wanaunga mkono upuuzi wa mrahaba wa 3%, leo wanajifanya wazalendo. Nyie mmejitosa kutetea upuuzi na kumlaumu mtu aliyepiga kelele kuhusu wizi huu toka miaka ya 90. Sasa ndio mnaamka na uzalendo uchwara. Ni hivi wizi wa dhahiri mpaka sasa sio wa hiyo michanga bali ni katika huo mrahaba wa 3% kwani mpaka sasa ndio unatamalaki.
Wizi ulianza siku nyingi na mkapa aliongoza wizi kwa kupita kila Mgodi akijifanya kukagua uwekezaji ili apate nafasi ya kupewa Zawadi pande la mkate wa Dhahabu wenye thamani ya mabilioni kwa kifupi mkapa alivuna mapande ya dhahabu na madini mengine kwa wingi sana na huenda akawa ni Rais mwenye utajiri mkubwa wa madini Duniani akifuatiwa kikwete ambaye pia alikuwa akivuna humo humo kijanja zaidi ikiwemo mengine kutoka congo yalipo majeshi ya Tanzania. Tokea miaka hiyo wazungu wameliubia Taifa lakini washirika wao yaani watanzania waliowasaidia kupata mikataba mibovu nao wamefaidika na madini mengi ikiwa ni Rushwa ya kufanikisha mikataba na kupitisha Sheria mbaya.
 
Mola piga kiberiti hizi family!
 
Wajinga ni wengi sn Tanzania.

Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana.
 
Dili la sasa la kontena za michanga limesukwa na mkapa na JK walimchochea magufuli wakijua atakurupuka na kutoa maamuzi ya ajabu ajabu pasipo kutafakari kwanza na kweli kakarupuka Dili lao linaenda vizuri wakiamini kuwa wazungu watakimbilia mahakamani na lazima washinde kesi ili walipwe fidia kubwa na wao watapata 10% zao humo humo pia endapo Tanzania itaanza kuwekewa vikwazo vya kimya kimya wana uhakika wa kutumwa wao kwenda kuomba vikwazo vilegezwe na hapo watatengeneza pesa pia kwa sasa magufuli kawatengenezea mchongo Wajanja watakula pesa humo humo pasipo yy kujijua.
 
Huko CCM wengi IQ ni zero wamekariri zidumu fikra za Mwenyekiti pekee ndiyo maana hubariki mikataba mibovu na wabunge wake kupitisha sheria mbaya kwa hati za ghafra hata usiku.
 
Back
Top Bottom