Tundu Lissu kwa sasa anaishi katika fikra za watanzania wengi kuliko mtanzania mwingine yoyote yule

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,327
Kupitia hapa JamiiForums, niliwahi taja sifa kuu 7 za Tundu Lissu kulingana na mtazamo wangu na moja ya sifa hizo ilkuwa ni uwezo wa Lissu kuona mbali(foresight).

Nilimpa sifa zile sio kwa lengo la kumsifia tu au kumjenga kisiasa,bali niliona mapema sifa alizonazo pamoja na uwezo huo alioanao.

Hata hivyo,kama kawaida ya binadamu,wako walionibeza,wako walio dharau lakini wako pia walioniunga mkono.

Sasa maswali:

Ni kipi kinachotokea leo hii ambacho Lissu hakukisema hadharani?

Ni sifa au tabia gani inayoonyeshwa na bwana mkubwa leo hii ambayo Lissu hakuisema?

Lissu aliposema hakuna aliesalama akinamanisha watu hawa hawana urafiki wa kudumu na mtu alikosea?

Aliemwambia Lissu anayofanya ni "uzwazwa" leo hii nini kina mpata?

Nyani Ngabu aliekuwa anamponda Lissu,leo hii haongelei ukabila aliouongelea Lissu hapa kabla?

Aliyoyaongea Nyalandu,kuna ambalo Lissu hakulisema kabla?

Nakumbuka kwenye ule uzi niliandika kuwa wengi tumesoma historia kama hadithi tu ila mwenzetu(Lissu) mbali ma kuisoma historia, lakini pia anaitumia historia kama kioo cha maisha yake.

Ukimsikiliza vizuri Lissu,kama ilivyokuwa mara nyingi kwa mwalimu Nyerere katika hotuba zake, utagundua anatumia sana historia kama kioo(reference) kuelezea mambo mengi ikiwemo tabia na aina ya watawala wa sasa na nini wanaweza kukifanya hapo baadae kwa kuangalia matendo ya watawala waliiopita na wanaofafana kitabia na watawala wa sasa.

Kwa kifupi ni kuwa,hakuna kiongozi leo hii aneonyesha aina mpya ya uongozi ambayo haikuwa kuonyeshea na watawala tunaowasoma katika historia ya miaka nenda miaka rudi.

Viongozi wazuri na tabia zao hawajaanza kuishi leo hii; halikadhalika, viongozi wabovu wakiwemo madikteta na tabia zao, hawajaanza kuishi leo hii hivyo inakuwa rahisi kujua kiongozi fulani kwa sifa na tabia alizonazo ataongoza au atatawala kwa mtindo gani na anaweza fanya nini katika uongozi/utawala wake.

Kwa kifupi,kwa haya niliyoyasema na haya yanayotokea leo hii,kila siku tutajikuta tunakumbuka maneno ya Tundu Lissu penda tusipende na hivyo fikra zake zitabaki vichwani mwetu kwa muda mrefu unless mambo yanabadilika.
 
K

Nyani Ngabu aliekuwa anamponda Lissu,leo hii haongelei ukabila aliouongelea Lissu hapa kabla?

We nyumbu mzushi uliwahi kusema mimi namtetea Makonda. Nilipokubana ukashindwa kuonyesha hata sentensi moja ambapo nimewahi kumtetea Makonda.

Na msimamo wangu kuhusu ukabila uko palepale.

Huyo Tundu Yesu [courtesy of Al-Watan] naye ni mropokaji tu na kwenye hilo nampinga na nitaendelea kumpinga.
 
mzani mzuri 2020 tumpe fomu agombee,akiweza kumbwaga JPM,basi jamaa atakuwa kaka wa taifa
 
unampa sifa nyingi ambazo hana.
mfano hana uwezo wa kuona mbali.
wakati yeye anaona tanzania mqhakamani kuhusu madini huku yanaonekana makubaliano.
wakati yeye anaona nchi isiyo na mafisadi chini ya chadema sisi tunamuona mtuhumiwa wake namba moja kiti cha mbele.

punguza mapenzi kwa lisu mkuu ili uwe huru. anaweza kuwa na vitu lkn sio ktk viwango vya thread yako na anakidhi viwango vya kupingwa sana tu anapopungua.
 
Umejuaje hayo!!!
Acha kutunga kwa sababu yeye hana analolisaidia Taifa letu kuwezwa kufikiriwa na unaodai.
 
unampa sifa nyingi ambazo hana.
mfano hana uwezo wa kuona mbali.
wakati yeye anaona tanzania mqhakamani kuhusu madini huku yanaonekana makubaliano.
wakati yeye anaona nchi isiyo na mafisadi chini ya chadema sisi tunamuona mtuhumiwa wake namba moja kiti cha mbele.

punguza mapenzi kwa lisu mkuu ili uwe huru. anaweza kuwa na vitu lkn sio ktk viwango vya thread yako na anakidhi viwango vya kupingwa sana tu anapopungua.
Wengine hupenda kusema angali mtu yu hai tofauti na wengi.
 
Wengine hupenda kusema angali mtu yu hai tofauti na wengi.
Anapedwa na mafisadi na wezi si kwa mtu muungwana
Hakuna alicho saidia hii nchi chenye mashiko.sasa nani atamfikiria ?
Mi naonaga yeye lisu ni kama mtu asie na heshima wala staha.
Nikiona domo lake natamaani niuzibe kwa supa glue kwani linatoa kinyesi
 
Mtamchukia sana na bado.
 
Umetaja sifa zoooote za magufuli.
Umekwepesha usijulikane na kainana!
 
Back
Top Bottom