Tundu Lissu kutogombea tena ubunge?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,204
42,064
Wasalaam wana jamvi!
Wakati wengine wakifurahia kupata ubunge kwa upande wa Mh Tundu Lissu imekuwa ni matatizo makubwa kwani ubunge umemsababishia umasikini kabisa!

Wana jamvi waswahili wanasema ukiona mtu mzima ana lia hadharani ujue kuna jambo.....Mh Tundu Lissu alikaririwa akisema ubunge umemsababishia umasikini na hivyo ana hitaji zile pesa 230+ walizo kuwa wametengewa!

Kwakweli mimi nilisikitishwa sana na kukuguswa sana na kilio chake na niliamini kabisa Lissu ni mtu makini sana anaposema ubunge umemsababishia umaskini ana maanisha kabisa na pengine tusije tukashangazwa kama hatogombea tena maana mtu makini kama Mh Tundu Lissu awezi kuendelea na kitu kinacho mtia umasikini!

Hivyo ndio maana nimepata wasi wasi kama kweli Lissu atagombea ubunge tena lasivyo ni vyema Chadema wakamfikiria zaidi Mh Lissu kwa kumpa hata mshahara wa ziada ili kumuondoa kwenye umasikini alio upata baada ya kuwa mbunge!

Kama kweli Dr.W.Slaa aliweza kusikilizwa na kuwa ana lipwa kama mbunge kutokana na umuhimu wake ni vyema na Mh Lissu akapewa mshahara wa ziada kutoka kwenye chama kutokana na kazi anayo ifanya!

Bado najiuliza kweli Mh Lissu atagombea ubunge tena ikiwa huu ubunge umemletea umasikini hadi ana tangaza hadharani?

Ni vyema ili jambo likatazamwa vyema ili Mh Lissu asije akagomea kugombea ubunge kutokana na umasikini!

Karibuni wana jamvi!
 
Hivi wewe badala ya kujadiri sasa kumeguka kwa chama tawala unaanza kujipa vyeo as if wewe ni msemaji wa CDM! Ama kweli hizo nafasi tano za UDC zinategemewa na wengi. Ndugu yangu thread kama hii haitakuongzea credits kwa bwana Mkulu ili upate angalau ka UDC. Imekula kwako!
 
Unakielewa unacho andika? Wewe maisha yako haya kutii umaskini, usihangaike na maisha ya mwanamume mwenzako jali biashara yako
 
hilo sio muda wake hapa '
ila nikwmbie kitu kama jamaa angejiajiri nadhani asingefanana na wakili yeyote
meaning that even market price yake ingekuwa juuu
 
Tokea ameingia bungeni hakuna tija zaidi ya kuleta vurugu zisizo na maana. Naona kajipima kaona hakubaliki ndio maana kasema ubunge umemtia umaskini na naona ni namna ya kushindwa mpambano. Aendelee na uanaharakati tu kama alivyoanzia tangu enzi zile za kupewa kipindi pale ITV.
 
sijaona tatizo kwenye kauli ile ya lissu kamwe. tatizo la watanzania mnapenda wanasiasa wanafiki na waongo waongo. inawezekana kabla hajawa mbunge alikuwa na njia nyingi za kumuingizia kipato kuliko njia hii ya kutegemea ubunge tu. lissu ni mtetezi wa kweli wa wanyonge. lissu atashinda tu akigombea tena ubunge.
 
Anagombea urais kupitia UKAWA. Upo hapo?
Tokea ameingia bungeni hakuna tija zaidi ya kuleta vurugu zisizo na maana. Naona kajipima kaona hakubaliki ndio maana kasema ubunge umemtia umaskini na naona ni namna ya kushindwa mpambano. Aendelee na uanaharakati tu kama alivyoanzia tangu enzi zile za kupewa kipindi pale ITV.
 
Alichosema Lissu ni kweli kuwa Wabunge wengi ni MASIKINI kasoro Wachache.

Kama Wakili alikuwa na fedha nyingi zaidi. Pia za Ubunge amekuwa akizitumia kwenye kusaidia kampeni za jimboni kwake na kwa sababu hiyo, ndiyo maana Jimboni kwake uchaguzi wa Madiwani na Wenyeviti wa vijiji, aliwatandika CCM sawasawa. Yaani ingelikuwa Bukoba basi tungelisema aliwatandika kale kamchezo ka GULIONI hao maCCM wa Ikungi.

Akihojiwa na Salama kwenye kipindi cha MKASI, alikiri kuwa anapenda sana KUYATANDIKA MA-CCM.

1:02:40 (Mimi napenda Ubunge.... by Lissu)

https://www.youtube.com/watch?v=1m8IRbqFnb0
 
Sikonge,

..u r 100 % correct ktk post yako hapo juju.

..tundu angekuwa mtu wa kutafuta utajiri tungemuona kwa aina ya kesi anazotetea.

..tangu ahitimu udsm, tundu amekuwa akitetea kesi za wananchi wengi wenye kipato cha chini.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom