Tundu Lissu: Kushtakiwa kwa uchochezi katika Tanzania ya Magufuli ni "Beji ya heshima"

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,041
1,160
Watu wetu wengi sana wamekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi. Wengi wanaendelea na wataendelea kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa hayo. Kushtakiwa kwa uchochezi katika Tanzania ya Magufuli ni 'beji ya heshima' (a badge of honour.)

Ni kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere, maana Mwalimu pamoja na waandishi habari Robert Makange (mhariri wa gazeti la Sauti ya TANU) na Rashid Baghdelleh (mhariri wa gazeti la Mwafrika) walikuwa watu wa kwanza Tanganyika kushtakiwa, na kupatikana na hatia, kwa kosa la uchochezi.

Sheria iliyotumika wakati huo ni hii hii inayotumika dhidi yetu, miaka 58 baadae. Tofauti pekee ni kwamba wameihamisha kutoka kwenye Kanuni ya Adhabu na kuipeleka kwenye Sheria ya Magazeti.

Na kama ambavyo kuitwa mchochezi na kushtakiwa kwa Mwalimu Nyerere hakukuwa taji la miba kwake, hivyo hivyo kushtakiwa kwetu kwa makosa hayo hayo hakutakuwa taji la miba kwetu.

Sisi ni wajukuu wa Julius Kambarage Nyerere na Robert Makange na Rashid Baghdelleh. Hii ni heshima kubwa kwetu, sio jambo la kuinamisha kichwa kwa aibu. William Rivers Pitt, mwandishi wa Kimarekani aliandika kitabu kìitwacho 'Silence is the Greatest Sedition', yaani 'Ukimya ndio Uchochezi Mkubwa.'

Ukimya wakati katiba na sheria na haki zetu zinakanyagwa na Mtakatifu Rais na watu wake ndio uchochezi mkubwa. Sisi hatujafanya kosa hilo. Kwa sababu hiyo, tunawasubiri watesi wetu wa sasa mahakamani waje watuambie makosa yetu ni yapi. Na tayari wameshaanza kukimbia, maana aliyetushtaki sisi hataki kuja kutoa ushahidi mahakamani. Watakimbia sana. Aluta continua!
 
Aluta continua.

Hata Solomon Kalushi Mahlangu, mpigania ukombozi wa Afrika Kusini alipata kusema"
"Tell my people that I love them, and that they must continue the struggle. My blood will nourish the tree that will bear fruits of Freedom. Aluta continua"
 
Lissu alimponda sana Nyerere wakati wa kutetea muungano wa serikali tatu.

Leo anajifananisha nae.....muda mwingine huwa simuelewi.

BTW hili analolipigania namuunga mkono ila apunguze ukigeugeu
 
Tundu Lissu yupo sahihi kabisa hatuwezi kurudi nyuma hakuna haki inayopatikana kirahisi nadhani kichonaendelea sasa ni kuwapa wanachama wetu hofu kwa kesi za uchochezi.
Tundu Lissu mchango wako mkubwa katika nchi yetu utakumbuka daima naamini hujawahi wala hutorudi nyuma katika kupinga demokrasia kukandamizwa.
 
Nadhani itachukua muda mrefu sana kwa wenye uelewa mdogo wa kufikiri kumwelewa Tundu Lissu.

Lissu alimponda sana Nyerere wakati wa kutetea muungano wa serikali tatu.

Leo anajifananisha nae.....muda mwingine huwa simuelewi.

BTW hili analolipigania namuunga mkono ila apunguze ukigeugeu
 
Anaandika Tundu Lissu.

Watu wetu wengi sana wamekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi. Wengi wanaendelea na wataendelea kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa hayo. Kushtakiwa kwa uchochezi katika Tanzania ya Magufuli ni 'beji ya heshima' (a badge of honour.)

Ni kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere, maana Mwalimu pamoja na waandishi habari Robert Makange (mhariri wa gazeti la Sauti ya TANU) na Rashid Baghdelleh (mhariri wa gazeti la Mwafrika) walikuwa watu wa kwanza Tanganyika kushtakiwa, na kupatikana na hatia, kwa kosa la uchochezi. Sheria iliyotumika wakati huo ni hii hii inayotumika dhidi yetu, miaka 58 baadae.

Tofauti pekee ni kwamba wameihamisha kutoka kwenye Kanuni ya Adhabu na kuipeleka kwenye Sheria ya Magazeti. Na kama ambavyo kuitwa mchochezi na kushtakiwa kwa Mwalimu Nyerere hakukuwa taji la miba kwake, hivyo hivyo kushtakiwa kwetu kwa makosa hayo hayo hakutakuwa taji la miba kwetu.

Sisi ni wajukuu wa Julius Kambarage Nyerere na Robert Makange na Rashid Baghdelleh. Hii ni heshima kubwa kwetu, sio jambo la kuinamisha kichwa kwa aibu. William Rivers Pitt, mwandishi wa Kimarekani aliandika kitabu kìitwacho 'Silence is the Greatest Sedition', yaani 'Ukimya ndio Uchochezi Mkubwa.' Ukimya wakati katiba na sheria na haki zetu zinakanyagwa na Mtakatifu Rais na watu wake ndio uchochezi mkubwa.

Sisi hatujafanya kosa hilo. Kwa sababu hiyo, tunawasubiri watesi wetu wa sasa mahakamani waje watuambie makosa yetu ni yapi. Na tayari wameshaanza kukimbia, maana aliyetushtaki sisi hataki kuja kutoa ushahidi mahakamani. Watakimbia sana. Aluta continua!
 
Back
Top Bottom