Tundu Lissu kurudi nchini tarehe 7 Septemba, 2019

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Sasa ni rasmi kuwa mh. Tundu Lissu aliyekuwa nje ya nchi kwa matibabu kwa takriban miaka miwili anatarajiwa kutua nchini tarehe 7/9 mwaka huu siku ya Jumamosi. Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe amesema wanaandaa mapokezi makubwa ya mh. Lissu ambayo hayajawahi kutokea ukiacha mapokezi ya Mandela, Papa na mapokezi ya mwili wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.



Ikumbukwe Lissu alishambuliwa kwa risasi tarehe kama hiyo 7/9/2017.

Kauli ya Mhe. Tundu Lissu.

"Nitatua tarehe 7 Septemba, 2019 kwenye ardhi ya Tanzania, kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nitakuwepo" Mhe. Tundu Lissu.

“Septemba 7 niliondoka Tanzania nikiwa nusu mfu, kuna watu walitaka nife hivyo nimeamua Septemba 7 iwe safari yangu ya kurudi Tanzania nikiwa mzima ili kudhihirisha hao waliotaka kuniua kuwa niko hai.”

“Nitarudije, itakuwaje, safari itakuwaje hizo ni taratibu ambazo hatuwezi kuziweka wazi kwa sababu muda ukifika Watanzania watajulishwa,” alisema Lissu.

Kauli ya Mkiti wa Chadema Mhe. Mbowe.

“Septemba 7 ni siku maalumu sana, ilikuwa pigo kwa demokrasia, uhuru wa wapigania haki za binadamu kwa kushuhudia tukio la mwenzao anashambuliwa hadharani tena mchana kweupe, ndio sababu Lissu anarejea Septemba 7,” alisema Mbowe.

“maandalizi yanafanyika ya ujio wake, muda ukifika Watanzania wataelezwa itakuwaje lakini kwa sasa itoshe kujua tu kuwa Lissu atarudi Septemba 7.”

"Tutatangaza mapokezi ya kitaifa kumpokea Mhe. Tundu Lissu" Mhe. Freeman Mbowe.

======

Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema atarejea Tanzania Septemba 7, 2019 kutoka nchini Ubelgiji anakoendelea na matibabu.

Lissu amekuwa nje ya Tanzania tangu Septemba 7, 2017 aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa eneo la makazi yake Area D, Dodoma.

Mara baada ya kushambulia, mwanasiasa huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikopata matibabu hadi Januari 6, 2018 na kuhamishiwa Ubelgiji kuendelea na matibabu zaidi.

Lissu ambaye kwa sasa anatembea kwa msaada wa gongo moja akizungumza na wapiga kura wake mwishoni mwa wiki kupitia simu ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema anarudi nchini Septemba 7, 2019.

Rais huyo wa zamani wa Chama cha Wanasheria Tanganyila (TLS) amesema katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba, 2019 atakuwepo Tanzania.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Mei 22, 2019 Mnadhimu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema, "Narudi nyumbani Septemba 7 ya anniversary ya kushambuliwa kwangu."

Chanzo: Mwananchi
 
Hapa lazima siku hiyo bwana yule mwenye chuki mbaya dhidi ya Lissu na watu wake wajaribu kuandaa tukio kubwa ili wajaribu kufunka mapokezi ya Lissu,na wakiona wameshindwa,basi watatafuta sababu za kuzuia mapokezi hayo kwa visingizio kama vile usalama,kutokwamisha shughuli za watuamiaji wengine wa barabara,n.k ingawa haya hatukayaona wala kuyasikia katika mapokezi ya mwili wa Ruge,Mengi na katika matukio mengine.
 
Hahaaaa... Just hahaaaa... Just bwahahaa! Jamaa mishavu dodo, kijitambi cha kizushi maana si kwa nyama choma na mvinyo wa Belgium kwa michango ya Ufipa. Kweli mjini shule!
 
Hapa lazima siku hiyo bwana yule mwenye chuki mbaya dhidi ya Lissu na watu wake wajaribu kuandaa tukio kubwa ili wajaribu kufunka mapokezi ya Lissu,na wakiona wameshindwa,basi watatafuta sababu za kuzuia mapokezi hayp kwa visingizio kama vile usalama,kutokwamisha shughuli za watuamiaji wengine wa barabara,n.k ingawa haya hatukayaona wala kuyasikia katika mapokezi ya mwili wa Ruge,Mengi na katika matukio mengine.
Nani wa kuwazuiyeni kumpokea huyo ndugu yenu?
 
Siku hizi hatumsikii tena vip ziara zimekwisha au mialiko hakuna siku hizi!!!
Michango inaendeleaje au makamanda mmeona apambane na hali yake
 
Back
Top Bottom