Tundu Lissu, kufanyiwa upasuaji wa mwisho tarehe 4/6/18, awapa salamu Watanzania

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji wamwisho tarehe 4/6/2018 Maendeleo yake ni mazuri azungumza na Mwanahabari Huru
IMG-20180527-WA0098.jpg
IMG-20180527-WA0099.jpg




=========

Hello wapendwa wangu.

Ninaamini wengi wenu, kama sio wote, mnafahamu kwamba Jumatatu tarehe 4 June nitafanyiwa operesheni ya mwisho kwenye mguu wa kulia.

Ni operesheni kubwa inayotazamiwa kuchukua takribani masaa nane kwa taarifa nilizopewa tangu mwanzoni mwa wiki hii. Hivyo madaktari wangu wametumia muda mrefu kidogo kuniandaa kwa ajili ya Jumatatu.

Napenda niwajulishe kwamba ninajisikia vizuri kiafya, na baada ya kuangikwa kitandani tangu tarehe 11 Aprili niliyofanyiwa operesheni ya pili, sasa niko tayari kwa ajili ya hii ya mwisho. Madaktari wangu wako vizuri. Nina imani watafanya kazi nzuri ya kitabibu.

Kwa ninyi marafiki na ndugu zangu. Mmekuwa na mimi na familia yangu tangu tarehe 7 September ya mwaka jana. Mmetusaidia kwa maombi na kwa majitoleo yenu ya hali na mali.

Bado safari ni ndefu lakini ninaweza kusema nimeanza kuona mwanga katika hili tanuru refu. Nimesema mara nyingi kwamba ninaona fahari na faraja kwamba Watanzania wenzangu na wasio Watanzania wamenitibu na wanaendelea kunitibu. Najua mtaniponya kwa nguvu za Mola wetu na kwa upendo na ukarimu wenu.

Nawaombeni msichoke.

Nawashukuruni sana.
 
Mwanahabari Huru ukiongea naye tena mwambie huku nyumbani Chama "twawala" ni mtifuano baada ya kugundulika kuwa viongozi wao walikuwa wanakomba mpaka viwanja na nyumba za chama kuhongea michepuko. Watu wametafuna hadi shule!
Heh,hizo ndio salamu gani sasa kwa mgonjwa!!badala ya kumwambia kuwa tunamuombea heri apone haraka wewe unazidi kumzidishia maumivu ya ugonjwa..
 
Mwanahabari Huru ukiongea naye tena mwambie huku nyumbani Chama "twawala" ni mtifuano baada ya kugundulika kuwa viongozi wao walikuwa wanakomba mpaka viwanja na nyumba za chama kuhongea michepuko. Watu wametafuna hadi shule!
Baada ya kumpa taarifa kuna msiba chadema na baada ya siku tisini jimbo linaondoka,unazungumzia mali za ccm zilizo mikononi mwa wana ccm!
 
Back
Top Bottom