Tundu Lissu kimataifa: Akutana na David Mcallister, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashauri ya Kigeni ya Bunge la Ulaya

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
9,431
2,000
Unaongea usiyoyajua. Nina uhakika uelewa wako katika mambo ya kimataifa ni duni sana au haupo kabisa.

Gadaffi alikuwa anaua kila anayehoji utawala wake. Wakati wa utawala wa Gadafi, maisha ungeyaona mazuri sana kama ukikubali kuishi kama perty animal. Ukitaka kuonesha kuwa na wewe ni binadamu, sawa na Gadati, ndiyo mwisho wako wa kuishi Duniani.

Hata wakati wa mapambano ya kuondoa utawala wa Gadafi, wapiganaji wote walipewa maelekezo ya kumkamata Gadafi, wasimjeruhi wala kumwua ili ashtakiwe, lakini yule mpiganaji ambaye hakuwahi kuwa askari alipokutana uso kwa uso na Gadafi, licha ya Gadafi kunyosha mikono ikiwa ishara ya kukubali kukamatwa, alimiminiwa risasi, na askari wengine walipofika walikuta amekwishauawa. Yule askari alikamatwa, alishtakiwa na kuhukumiwa kifo. Lakini katika maelezo yake alisema kuwa alifahamu wazi kuwa hakustahili kumwua lakini yeye aliamua kumwua kwa sababu yeye Gadafi hakuwahi kumpeleka ndugu yake mahakamani, alikamatwa alipelekwa gerezani, na usiku mmoja, yeye pamoja na wenzake waliyltolewa gerezani, wakauawa na kuzikwa kwenye kaburi moja watu 250. Alisema alijua kuwa atauawa lakini angalao ameweza kumwua mtu aliyemwua ndugu yake.

Ghadafi alikuwa mshenzi kwa watu wake hasa wabeghazi lakini pia akajifanya mjuaji kwenye maslahi ya mabeberu.... Ghadafi angesimamia vizuri maslahi ya mabeberu basi angetawala kwa amani kabisa hata kama angekuwa anaua walibya wenzake...

Saadam Iraq aliwekwa madarakani na CIA na akayasimamia vyema maslahi ya USA pamoja na kuwaua waarabu wenzie hakuna aliyemgusa, pale alipoanza kusumbua mabwana zake tu walimshukia faster....Saudia chini ya MBS inasimamia vizuri maslahi ya USA hata MBS afanye nini hakuna wakumgusa ndio maana Kashoghi amekufa kama kuku na iko wazi nani mhusika lakini kimya
 

House of Commons

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,968
2,000
Huwezi kuitoa CCM kwa kutegemea Wazungu ambao nao wanabenefit kwa CCM, kinachofuata watakutumia kuibana CCM kwa wao kupata maslahi zaidi... Nitajie nchi moja ambayo wazungu wameleta demokrasia na stabilization..

Wazungu walishindwa kuwasaidia weusi pale SA dhidi ya kaburu matokeo yake weusi wenyewe wakapambana kujikomboa huku wazungu wakipamban kimyakimya kusaidia kaburu..
Kwa Gadafi
 

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,203
2,000
Kwa hiyo sasa hivi watu wako huru!

Democrasia imetawala maisha ni mazuri sana baada ya mzungu kuleta demcrasia?
Siyo sababu yakutokudai democracy halisi. Siyo hivi viini macho . WaLibya wameharibikiwa kwa sababu ya Gaddafi mwenyewe . Miaka 42 na bado unataka mwao akurithi !!. Hata hapa kwetu sababu ya Ccm kung'ang'ania madarakani miaka 60 bila kuweka mazingira mazuri ya kupokezana vijiti yaweza kuleta hali hiyo ya Libya leo.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,091
2,000
Hivyo sio priority yao, priority yao ni rasimali zako ndio maana wako karibu na CCM na ukiwaoffer kupata zaidi ya hivyo basi kesho tu wanaitoa CCM na wakikuona hauna maslahi nao basi watakutumia kupata zaidi kwa CCM kwa kuitisha dhidi yako na wafuasi wako....kifupi kwa sasa mabeberu wanaitumia CDM kuitisha CCM na CCM inazidi kuwapa zaidi kutoka kwenye cake ya Taifa..

..walipakodi na wapigakura wao hawapendi serikali zao zifadhili tawala za kidhalimu.

..kwa hiyo viongozi wanapata "credit" fulani kama wataonekana wanatumia kodi za wananchi vizuri.

..kwenye suala la rasilimali wanapenda STABILITY na kuingia mikataba na tawala zisizoendekeza rushwa.

..ukiwaahidi stability kupitia demokrasia na haki, na kuwaahidi kuunda serikali isiyoendekeza rushwa, utakuwa umewashawishi vya kutosha.

..makampuni ya mabeberu yanaweza kuadhibiwa ikiwa yatajiingiza ktk vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa haki za binaadamu yanapofanya biashara nje ya nchi.
 

Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
712
1,000
We ndo mjinga kabisa kwa fikra hizo za kitumwa, walimuua Ghadafi hilo limewasaidia nini Walibya, nchi inekuwa uwanja wa vita tangu wamuue. Interest yao ilikuwa ni rasimali mafuta na siyo maslahi ya wananchi wa Libya.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Bora wazungu kuliko kuuawa na mtu unayemjua. Jpm ameua wangapi ndani ya mda mfupi je angemaliza miaka 10 angeua wangapi
 

Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
712
1,000
Ndio maana nakwambia wewe una akili yakitumwa!

Hivi Libya kabla ya wazungu wako kuketa democrasia watu walikuwa wana chinjana kama ilivyo sasa?

Kwa Kagame kuna watu wana chinjana?

Mkilishwa ujinga wa democrasia ya mzungu nasi mnajihisi mko mbinguni
Nenda kwa kagame uone wapinzani wanavyonyanyaswa na kubambikwa makesi ya uhaini na kunyongwa. Yule mdada aliyekuwa mshindani wake mpaka leo yupo selo na bila shaka ameshakufa
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
18,803
2,000
Siyo sababu yakutokudai democracy halisi. Siyo hivi viini macho . WaLibya wameharibikiwa kwa sababu ya Gaddafi mwenyewe . Miaka 42 na bado unataka mwao akurithi !!. Hata hapa kwetu sababu ya Ccm kung'ang'ania madarakani miaka 60 bila kuweka mazingira mazuri ya kupokezana vijiti yaweza kuleta hali hiyo ya Libya leo.
Libya ya Gadafi na hii ya baada ya democrasia ya mzungu ziko sawa?
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,370
2,000
Kwa mawazo yangu hauko sahihi samurai . Tunaihitaji maisha bora na elimu bora. Vyote hivi haviwezi kuletwa na Ccm ile Ile yenye itikadi za ki communist. Bila katiba nzuri inayoruhusu vyombo ya maamuzi kujisimamia , forget . Unapokuwa judges wanaoomba usiku na mchana wafanyiwe favour. Unapokuwa na vyombo vya dola na vya maamuzi ambao viongozi wake hawatokani na ueledi bali mapenzi ya alieko state house sahau. Ukijumlisha na nidhamu ya uogatuliojegewa .

Elimu mbovu ni mtaji wao wa kuitawala nchi hii. Na umasikini ni usalama wao wa kubaki madarakani. Hawawezi kuvitoa hivi.
Kwa hiyo nchi za kikomunisti hazina maendeleo?!!!

Tafsiri ya maendeleo ni pana mno.....na hwenda kila mmoja akawa na tafsiri yake.....
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,370
2,000
Mimi siishi kwa kukariri kama wewe na brazaj. Kama hamuwezi kuona kazi anayofanya Rais SSH basi mumevaa mawani ya mbao.

Siwezi kuungana na nyinyi kama mnataka blindly niandike post za #MboweSiyo Gaidi au #Katiba Mpya. Mimi Nina akili zangu na najitambua
Tatizo huonekana pale WAKOSOAJI wa watawala wakifanya jukumu lao hilo huku wakichagua upande....tena wakiwa "biased" mathalani afanyavyo Askofu Niwemugizi......
 

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
7,577
2,000
Mimi siishi kwa kukariri kama wewe na brazaj. Kama hamuwezi kuona kazi anayofanya Rais SSH basi mumevaa mawani ya mbao.

Siwezi kuungana na nyinyi kama mnataka blindly niandike post za #MboweSiyo Gaidi au #Katiba Mpya. Mimi Nina akili zangu na najitambua
Wewe ni jitu la hovyo tu. Mwanaume unatakiwa uwe na msimamo uwe thabit. Wewe ni wa ovyo kaa ukijua hilo
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,370
2,000
Chama cha CDU kimeshindwa uchaguzi mkuu nchini Ujerumani.....

CDU cha David Mc Allister ni chama rafiki cha CHADEMA....ni hawahawa akina Mc Allister walio MASPONSA wakubwa wa CDM....
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
14,976
2,000
Niko vizuri, ninajutambua. Akili yangu haiwezi kufuata mkumbo wa kumsikiliza Mbowe au Lissu. Mimi nataka changamoto mpya na tunayo na Rais SSH

Hata msukuma ndani ya ping kusema:

"Nduhu I tabu" = "Hamna Taabu."

😂😂!

Hiiiiii bagosha!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom