FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,881
- 109,192
Ukweli mchungu.
Tukio la Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi kwa waliotaka kumuua ni tukio ambalo sikutarajia maishani mwangu kama nitalishuhudia kwenye siasa za Tanzania.
Sikuamini hapo kabla na mpaka leo hii siamini kama kuna mwana siasa au kiongozi yeyote wa Tanzania anaweza kufikia hatua ya kupanga na kuamuru mauaji ya kutisha (terror) kama yale.
Siamini kama kuna mwendawazimu ndani ya CCM anaweza kubadili neno "siasa" kuwa mauaji.
Nilikuwa sipatani na siasa za Mwalimu Nyerere kwa sababu nyingi tofauti, moja wapo ilikuwa ni hiyo ya kufunga upinzani na kubaki na chama kimoja bila upinzani ambao ungeweza kukosoa na kufungua macho ya Wananchi anapokosea.
Uliporudishwa tena upinzani nilifurahi sana na nikawa nnauhakika 100% sasa Tanzania itaendelea.
Mazingira niliyokulia Dar yalikuwa ya ushindani kuanzia majumbani, shule ya msingi niliyosoma mpaka sekondari, tulikuwa tunashindana kweli kuanzia darasani mpaka kwenye viwanja vya michezo. Nilipobahatika kwenda nje ya Tanzania nako nikakuta ushindani kuanzia darasani, viwanjani na mpaka kazini na kwenye biashara. Niliamini na nnaamini mpaka leo hii, kuwa na ushindani mwema kunaleta maendeleo. Ni bahati mbaya kwenye siasa za Tanzania ushindani umeitwa "upinzani".
Nani leo hii Tanzania aliyekuwepo kabla ya upinzani (tulipokuwa na chama kimoja) na baada ya kuruhusiwa "upinzani" (vyama vingi) ambae atakataa kuwa tumepiga hatua kubwa na ndefu zaidi baada ya kuruhusiwa upinzani.
Nakubaliana na Tundu Lissu anaposema kuna "nguvu kubwa" nyuma ya shambulio lake. Najiuliza, nguvu hizo ni za kisiasa? Kiserikali? Kibiashara? Kidini? Siamini mpaka sasa kama nguvu hizo ni kiserikali ndiyo maana nilifungua uzi huu: Tundu Lissu ni fursa kwa Serikali kuonesha ubora wake - JamiiForums.
Yeyote aliyemshambulia Tundu Lissu ametufanya CCM kuwa kama upinzani.
Naomba Serikali na wote wanaoitakia mema Tanzania wafanye kila njia kuwapata wabaya wetu, maana wametuumiza sana.
Tanzania bila upinzani tutarudi miaka ya foleni za chakula.