Tundu Lissu Katugeuza kuwa Wapinzani

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,872
109,169
Ukweli mchungu.

Tukio la Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi kwa waliotaka kumuua ni tukio ambalo sikutarajia maishani mwangu kama nitalishuhudia kwenye siasa za Tanzania.

Sikuamini hapo kabla na mpaka leo hii siamini kama kuna mwana siasa au kiongozi yeyote wa Tanzania anaweza kufikia hatua ya kupanga na kuamuru mauaji ya kutisha (terror) kama yale.

Siamini kama kuna mwendawazimu ndani ya CCM anaweza kubadili neno "siasa" kuwa mauaji.

Nilikuwa sipatani na siasa za Mwalimu Nyerere kwa sababu nyingi tofauti, moja wapo ilikuwa ni hiyo ya kufunga upinzani na kubaki na chama kimoja bila upinzani ambao ungeweza kukosoa na kufungua macho ya Wananchi anapokosea.

Uliporudishwa tena upinzani nilifurahi sana na nikawa nnauhakika 100% sasa Tanzania itaendelea.

Mazingira niliyokulia Dar yalikuwa ya ushindani kuanzia majumbani, shule ya msingi niliyosoma mpaka sekondari, tulikuwa tunashindana kweli kuanzia darasani mpaka kwenye viwanja vya michezo. Nilipobahatika kwenda nje ya Tanzania nako nikakuta ushindani kuanzia darasani, viwanjani na mpaka kazini na kwenye biashara. Niliamini na nnaamini mpaka leo hii, kuwa na ushindani mwema kunaleta maendeleo. Ni bahati mbaya kwenye siasa za Tanzania ushindani umeitwa "upinzani".

Nani leo hii Tanzania aliyekuwepo kabla ya upinzani (tulipokuwa na chama kimoja) na baada ya kuruhusiwa "upinzani" (vyama vingi) ambae atakataa kuwa tumepiga hatua kubwa na ndefu zaidi baada ya kuruhusiwa upinzani.

Nakubaliana na Tundu Lissu anaposema kuna "nguvu kubwa" nyuma ya shambulio lake. Najiuliza, nguvu hizo ni za kisiasa? Kiserikali? Kibiashara? Kidini? Siamini mpaka sasa kama nguvu hizo ni kiserikali ndiyo maana nilifungua uzi huu: Tundu Lissu ni fursa kwa Serikali kuonesha ubora wake - JamiiForums.

Yeyote aliyemshambulia Tundu Lissu ametufanya CCM kuwa kama upinzani.

Naomba Serikali na wote wanaoitakia mema Tanzania wafanye kila njia kuwapata wabaya wetu, maana wametuumiza sana.

Tanzania bila upinzani tutarudi miaka ya foleni za chakula.
 
Tuanzie hapa
Nyerere hukumpenda si kwa sababu ya hayo usemayo, ila nyerere hukumpenda kwasababu ni mkatoliki ambaye hakuvumilia ujinga wa dini nyingine hata yake ikiwamo, bahati mbaya mkatumia uelewa usio wa weledi mkidhani amewakomoa waislamu tu, kumbe woote hata wa Luther na wa anglikana tulipata msuko suko,

Pili, Suala la Lissu kushambuliwa ni suala linalochonganya sana, kuna mda nataka kuamini mbowe anahusika lakin nikajiuliza maswali nikaona wenda namtuhumu tu,

Kuna muda nahisi watu wa nyumba nyeupe lakin nikiangalia mazingira ya utakelezaji wa ishu hiyo imefanyika kishamba bila weledi nao pia nawatuhumu baadae nawaacha

Lakin keep in Mind kwamba katika siasa
TRUST NO BODY SUSPECT ANYONE,

Britannica
 
Ukweli mchungu.

Tukio la Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi kwa waliotaka kumuua ni tukio ambalo sikutarajia maishani mwangu kama nitalishuhudia kwenye siasa za Tanzania.

Sikuamini hapo kabla na mpaka leo hii siamini kama kuna mwana siasa au kiongozi yeyote wa Tanzania anaweza kufikia hatua ya kupanga na kuamuru mauaji ya kutisha (terror) kama yale.

Siamini kama kuna mwendawazimu ndani ya CCM anaweza kubadili neno "siasa" kuwa mauaji.

Nilikuwa sipatani na siasa za Mwalimu Nyerere kwa sababu nyingi tofauti, moja wapo ilikuwa ni hiyo ya kufunga upinzani na kubaki na chama kimoja bila upinzani ambao ungeweza kukosoa na kufungua macho ya Wananchi anapokosea.

Uliporudishwa tena upinzani nilifurahi sana na nikawa nnauhakika 100% sasa Tanzania itaendelea.

Mazingira niliyokulia Dar yalikuwa ya ushindani kuanzia majumbani, shule ya msingi niliyosoma mpaka sekondari, tulikuwa tunashindana kweli kuanzia darasani mpaka kwenye viwanja vya michezo. Nilipobahatika kwenda nje ya Tanzania nako nikakuta ushindani kuanzia darasani, viwanjani na mpaka kazini na kwenye biashara. Niliamini na nnaamini mpaka leo hii, kuwa na ushindani mwema kunaleta maendeleo. Ni bahati mbaya kwenye siasa za Tanzania ushindani umeitwa "upinzani".

Nani leo hii Tanzania aliyekuwepo kabla ya upinzani (tulipokuwa na chama kimoja) na baada ya kuruhusiwa "upinzani" (vyama vingi) ambae atakataa kuwa tumepiga hatua kubwa na ndefu zaidi baada ya kuruhusiwa upinzani.

Nakubaliana na Tundu Lissu anaposema kuna "nguvu kubwa" nyuma ya shambulio lake. Najiuliza, nguvu hizo ni za kisiasa? Kiserikali? Kibiashara? Kidini? Siamini mpaka sasa kama nguvu hizo ni kiserikali ndiyo maana nilifungua uzi huu: Tundu Lissu ni fursa kwa Serikali kuonesha ubora wake - JamiiForums.

Yeyote aliyemshambulia Tundu Lissu ametufanya CCM kuwa kama upinzani.

Naomba Serikali na wote wanaoitakia mema Tanzania wafanye kila njia kuwapata mabaya wetu, maana wametuumiza sana.
Duh.......

Hata wewe mama FaizaFoxy una ujasiri wa kuandika post hii??

Isije kuwa hii account yako imekuwa hacked??

Hata hivyo tunashukuru kwa jinsi "wachezaji" wa timu pinzani mnavyozidi kuikimbia hiyo timu yenu, kutokana na udhalimu wa hali ya juu unaofanywa na viongozi wa serikali hii!

Nina hakika hatimaye huko CCM atabaki Jiwe na wapambe wachache wakolomije wenzake, waliobaki wote watakuja upinzani!
 
Duh.......

Hata wewe mama FaizaFoxy una ujasiri wa kianfika post hii??

Isije kuwa hii account yako imekuwa hacked??

Hata hivyo tumashukuru kwa jinsi "wachezaji" wa timu pinzani mnavyozidi kuikimbia hiyo timu yenu, kutokana na udhalimu wa hali ya juu unaofanywa na viongozi wa serikali hii

Nina hakika hatimaye huko CCM atabaki Jiwe na wapambe wake wakolimojiee mwenzake!
Tutawapata wahalifu. CCM ni zaidi ya unavyoijuwa. Si chadomo.
 
Safi sana sio kama watu wa kariba ya Mropokaji wa zamani wa wanachi fc, wanakosa hoja za kuongea na kuleta mambo ya Personal Character assasination, sio tukio la kawaida ndani ya nchi yetu
 
Bahati mbaya ndiko ambako tulipo ushindani umeitwa upinzani na mbaya zaidi upinzani wa kuuana....ukitaka tu kuiondoa serikali kwenye jambo hili waseme tu zilipopelekwa CCTV camera? walinzi walienda wapi? Nani aliyewaamuru waache lindo?

Maswali haya Watz wenye nia njema tutaendelea kuyahoji kama si hadharani basi mioyoni mwetu
 
Ushindani katika kila jambo ikiwemo siasa huleta maendeleo na fikra mpya zenye mwelekeo chanya! Ushindani wa kisiasa hufanya wengi kuogopa kutenda maovu yakiwemo wizi wa mali ya umma, rushwa na ufisadi!

Kuondoa au kufifisha upinzani au ushindani katika siasa za nchi ni kudumaza Taifa!
 
I like what i just read..Thinking out loud always huwa na positive outcomes..Waambie wenzio

Sent using Jamii Forums mobile app
Wenzio ni kina nani??

Mbowe Nina mashaka nae sana, ni mchagga anaeweza kuuza hata utu wake kwa pesa.

Kwani tumesahau mnayoyaongea ya Wangwe, Zitto, Slaa?

Tunafahamu kuwa hata Lowassa ni mpango wake.

Tundu Lissu baada ya kuulizwa kama atagombea urais alipojibu do you think "I took 16 bullets for nothing?" Ina maana pana sana.
 
Ha ha humu hata nikimtetea yoyote siku ya kupiga kura huwa siendi maana ni kumpa kura mraji hivyo pande zote ni upinzani wa mwenzake na wanataka kitu kimoja.. sifa kubwa ya kiongozi ni kujitambua nakutambua na kufanya maamuzi sahihi wakati sahihi awe wa mpito asiwe lkn hizo ni sifa mahsusi
 
Back
Top Bottom