Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Katika miaka hii mitano kila Mtanzania awe ni tajiri au maskini ana hadithi yake ya maumivu

torosi

JF-Expert Member
Aug 12, 2020
788
1,308
Wapwa
Akiwa hapa Ifakara kwenye kampeni zake, Lissu anaendelea kutema cheche

Anasema kila Mtanzania ana hadithi yake ya maumivu. Ameomba kura kutoka vyama vyote na kuahidi mambo mengi ikiwemo kufuta machozi mengi ya wana Ifakara na Tanzania nzima.

Je wewe hadithi yako ni ipi.?

Haki huinua Taifa.
 
Haha Lisu bwana msanii sana,

Kuna binadamu anaweza mfuta machozi mwenzake??

Hapa duniani ni Utawala wa Sheria tu.

Usipofuata sheria unapoteza haki yako.

Mfano huwezi sema eti kwakua umefanya kazi kwa muda flani ndio uachwe hata kama umefoji vyeti.

Au kwakua umeshajenga ndani ya hifadhi ya barabara uachwe tu.
 
Hujui kina lissu ndio Wasaliti wa Nchi? Wanatumiwa na Mabeberu kuiba raslimali zetu
Sheria inasemaje juu ya hilo mpaka msaliti anapewa hadi idhini ya kuchukua fomu ya kugombea uraisi?

Kuna mawili

1. Kwamba usaliti sio ishu wala jambo kubwa la kuididimiza nchi na ndio maana kapewa dhamana ya kugombea bila kushakiwa mahakamani kwasababu wamejihakikishia kwamba hakuna madhara

2. Habari za msaliti ni political propaganda zisizo na chembe ya ukweli na ndio maana hakuna hatua yeyote imechukuliwa dhidi ya kashfa hiyo ambayo amewekewa
 
Haha Lisu bwana msanii sana,

Kuna binadamu anaweza mfuta machozi mwenzake??

Hapa duniani ni Utawala wa Sheria tu.

Usipofuata sheria unapoteza haki yako.

Mfano huwezi sema eti kwakua umefanya kazi kwa muda flani ndio uachwe hata kama umefoji vyeti.

Au kwakua umeshajenga ndani ya hifadhi ya barabara uachwe tu.
Kuteka watu ni kufuata sheria?

Kupiga wabunge risasi ni kufuata sheria ?

Kupora korosho za wakulima ni kufuata sheria ?

Kufungia vyombo vya habari ni kufuata sheria ?
 
Wapwa
Akiwa hapa Ifakara kwenye kampeni zake, Lissu anaendelea kutema cheche

Anasema kila Mtanzania ana hadithi yake ya maumivu. Ameomba kura kutoka vyama vyote na kuahidi mambo mengi ikiwemo kufuta machozi mengi ya wana ifakara na Tanzania nzima.

Je wewe hadithi yako ni ipi.?

Haki huinua Taifa.
Lisu hataki maendeleo.

Role model wake ni Kenyatta wa Kenya.

Angalia namna wanavyoumbuka kwa misaada mpaka SGR wamemkabidhi funder aiendeshe kurudisha pesa yake
 
Back
Top Bottom