Tundu Lissu katika chujio la moto, muda hausimami, amua kufa kwa ajiri ya wananchi wa Tanzania

Freewine

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
258
250
Salaam,

Hakika ujumbe huu umenichukua Kama wiki mbili kuuleta. Natumai unaenda kuanzisha harakati mpya ya ukombozi wa Tanzania.

Unajua Kama unaongozwa na chama Fulani zaidi ya miaka 50 mfululizo bila mabadiliko lipo tatizo kwenye nchi hiyo.

Turudi kwenye mada, hivi Kuna anayeweza kuamini kwamba Tundu Lissu alipigwa risasi 16 mwilini halafu akapona kifo hicho pasipo kuwepo mpango wa Mungu?

Hakika Kuna Siri ya Mungu katika ukombozi wa TL kwa kuwa Mungu ndie anaeamua Nani afe leo na Nani afe kesho. Daima Shetani mpango wake kwa wanadamu ni kuwaua tu hivyo sitegemei kwamba uponaji wa TL ni mpango wa Ibilisi.

Hivyo kwa pamoja kiimani tunaamini kwamba kupona kwa Tundu Lissu ni mpango wa Mungu

Je, unajua kwamba mpango wa Mungu huwa na kwa ajiri ya ukombozi wa watu wengi?

Tundu Lissu je unajua kwamba kupona kwako ni mpango uliopangwa na Mungu ili wewe uwe shahidi wa makuu ya Mungu kwa kusaidia watu wake?

Je, Tundu Lissu hicho unachokifanya kupita kwenye vyombo vya habari kumlaumu mheshimiwa unadhani kimetosha kuonesha ukuu wa Mungu kwa uponyaji aliokujalia?

Je, umeonesha kutangaza ukombozi wa watu wengi, una mpango?

Lakini Tundu Lissu unajua kitu kinaitwa "diminishing marginal returns?" Kwamba kadri unavyotumia/ kusikia kitu kile kile inafikia hatua unakichoka na kuunza kukipuuza?

Tazama habari zako zisije kuwa nyepesi na zile zile kuongelea upande wako tu zitasababisha upuuzwe na wazungu hao hata baadhi ya watanzania wenzako.

Usikubali kabisa kuonekana wewe ni kibaraka wa wazungu Kama ambavyo umeanza kutangaza nchini daima onekana unapigania ustawi wa watanzania umeponywa ili kulifanya hilo.

Daima wananchi wengi ni wapenzi wa nchi na viongozi wao hivyo daima mtu atakayetoa yaliyoko ndani kwake na kuyapeleka nje ataonekana msaliti wa taifa.

upuka kuonekana wewe ni msaliti wa taifa hili kwa kupinga Kila tuhuma zitazopandikizwa dhidi yako japo ulikuwa na haki ya kusema wazi wazi maumivu waliyokuletea. Najua upo kwenye chujio la moto ambalo kosa moja punishment nzito wakati kuzichanga vyema karata heshima ya kudumu katika taifa letu la Tanzania.

Hivi unajua kwamba Kuna mchakato wa katiba uliogarimu Pesa na muda mwingi wa watanzania lakini kwa hila za watu wachache umefichwa Hadi leo usionekane.
Je unajua kwamba ukipigania upatikanaji wa katiba mpya utakuwa umeleta ukombozi wa taifa hili?

Je unajua kwamba ukiwezesha suala hili utakuwa ni shujaa wa taifa hili? Kwa kupata katiba mpya Kama nchi itakuwa imejikomboa na uongozi muchungu unaoweza kukaa hata miaka Mia madarakani.

Najua utafatiliwa Sasa hivi ili kukupooza ila mapatano yako na wao yawe ni uazishaji wa kupitisha rasimu ya katiba ifike kwa wananchi na wananchi wenyewe ndo waamua either waipigie kura ya ndio au kura ya hapana.

Ukiwezesha suala hili la upatikanaji wa katiba mpya hakika utakuwa umesaidia UKOMBOZI wa taifa hili na uponyaji wa Mungu aliokujalia hautakuwa na makosa.
 

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
3,440
2,000
Ingekuwa nchi nyingine hapo sawa. Watz ni watu makini. Hawako tayari kuona nchi yao ikivurugika ama kuharibiwa kwa sababu ya Lissu kapona risasi 16. Hii nchi inakombolewa kwa mipango thabiti na sio kuropoka tu. Lissu awe makini sana.
 

Freewine

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
258
250
Ingekuwa nchi nyingine hapo sawa. Watz ni watu makini. Hawako tayari kuona nchi yao ikivurugika ama kuharibiwa kwa sababu ya Lissu kapona risasi 16. Hii nchi inakombolewa kwa mipango thabiti na sio kuropoka tu. Lissu awe makini sana.
Bila katiba mpya wote mtakuwa waunga juhudi za muheshimiwa bila kujali maumivu wanayopitia wengine
 

RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
890
1,000
Kama katiɓa hii iliyopo watawala hawaiheshimu hata tukipata mpƴa hawataiheshimu pia!

Tundu Lissu alishasema kazi ƴa kwanza ni kuing'oa CCM memgine yatafuata. Na kuiondoa CCM inahitaji kutengeneza Tufani ƴa kisiasa na si vinginevyo!

Ni ukweli pia kuwa ƙupona kwa TL ni mpango wa Mungu kwa watanzania kujua ukuu wake ili kipitia sauti ya TL angalau waTz wawe na tumaini.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,267
2,000
Siasa za kuuana hazina excuse!
Huwezi kumlaumu mhanga wa kutaka kuuliwa pale anapopambana kuueleza ulimwengu ili ukomeshe udhalimu huu lakini ukawanyamazia waliotaka kuua!
 

sontable

JF-Expert Member
Apr 13, 2018
242
500
Mkuu mbona umeandika kiingereza ili tujue kuwa na wewe msomi ama? Mtu na akili zako unachanganya kiswahili na kiingereza mbona unachanganya vitu bila utaratibu

Kama kweli wewe msomi katika utangulizi wako ungefafanua lugha utakazotumia katika makala yako

Chukua upuzi wako weka mfukoni usituletee hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Freewine

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
258
250
Kama katiɓa hii iliyopo watawala hawaiheshimu hata tukipata mpƴa hawataiheshimu pia!

Tundu Lissu alishasema kazi ƴa kwanza ni kuing'oa CCM memgine yatafuata. Na kuiondoa CCM inahitaji kutengeneza Tufani ƴa kisiasa na si vinginevyo!

Ni ukweli pia kuwa ƙupona kwa TL ni mpango wa Mungu kwa watanzania kujua ukuu wake ili kipitia sauti ya TL angalau waTz wawe na tumaini.
Unajua katiba iliyipo inampa madaraka mengi sana rais? Kuwaong'oa ccm madarakani lazima uwe na katiba yenye kuweza kutenganisha Kati ya tume ya uchaguzi na serikali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom